Hii, Serikali ina mpango gani na fedha za wana-DECI?

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,020
576
Serikali ilihamasisha watanachama wa DECI wajiorodheshe na kuhakiki madai yao, wananchi wakatii. Serikali ikatamka kwamba wana-DECI wataanza kupata fedha zao walizowekeza kwa mara ya kwanza ambao hawajawahi kuvuna. Ghafla iongozi wa DECI wakakamatwa na kuwekwa ndani, wakafunguliwa kesi inayoendelea na haieleweki itaisha lini. Serikali nahimiza ujasiriamali ambao hauwezekani pasipokuwapo mtaji. Wananchi hohehahe na yoyoyoyo... walikuwa wanajaribu kuutubisha mitaji kupitia DECI huku serikali yenyewe inaona mchana kweupeeee na kodi inapata. Sasa pesa ya wananchi inarudishwa vipi na seikali iliyofungia accounts zenye pesa ya DECI? Millions of money, bado wanadhani watapigiwa kura Octoba kwa bila kupewa pesa zao? Inawajali hohehahe kweli?

Leka
 
Leka!

Pamoja na huruma niwaoneayo wana DECI lakini nadhani Serikali imekwisha kuchukua hatua ya kuwashitaki viongozi!

Hii habari ya kuonewa huruma na kurudishiwa mitaji yao sio sahihi!

Tujifunze na kuacha njia za mkato
 
Back
Top Bottom