Bado hajaliona.....!!
Lengo kumbe ni kuburudisha...Wali kuku ni lugha ya hotelini ama kwa utaalamu zaidi maneno haya huitwa sajili (Register) ni namna ya uzungumzaji kulingana na shughuli inayofanyika mf. Hotelini-wali kuku, hospitali-ASA, PCM 2 mara 3, nk. Yote kwa yote kuna utumizi wa lugha kwa minajili ya kupamba lugha kama hivyo, mf. Hotelini mhudumu anapouliza, Nani wali ng'ombe? Swali hili huburudisha
kisarufi na maana pia!Ngoja nikuchanganye zaidi lakini usipotee! Wewe ulikwenda kwa kuku akakulaki na kukupa wali ambawo ukala, ulitosheka au la! matumizi ya kiunganishi KWA. Si hivyo tu, kuku mlishirikiana kuumonda ule wali. Pale ulipotumiya kiunganganishi NA. Unataka usahihi wa kisarufi au katika maana! Unataka usahihi upi? :drum: