jibu lipo clear tu kwamba watanzania kwa sasa wamechoshwa na porojo,,,,,unamwambia mtu anapaswa kuhesabiwa ili umsogezee huduma,,,ni kama kumdhihaki maana wanayoyasikia kuhusu ufujaji wa pesa za umma hiko kitu kinaumiza mioyo,,,,,pili mtu hawez kuacha kutafuta UGALI wake ukaja kumwambia amsubiri karani,,,,na mwamko huu ndio unaendelea hadi 2015,watanzania wengi zaid hawatapiga KURA sababu ya yale yanayoendelea bungeni,,,,,
sensa ya mwaka huu imejaa griba na ubabaishaji mwingi. Leo hii yamebaki masaa machache ya kuanza zoezi lenyewe lakini cha ajabu vifaa bado havijakamilika, sehemu ya malipo ambayo makarani tulipaswa kulipwa ikiwa ni pamoja na pesa ya nauli, tulitakiwa kulipwa tarehe 22-8-2012 mpaka sasa hakuna. Vifaa vingine ni mabegi, vitambulisho, penseli maalumu, sare, fomu mbalimbali hadi leo hii bado hatuna na kuanzia kesho usiku tunatakiwa kuanza zoezi hivi kweli hii sensa kutakuwa na ufanisi?
Katika zoezi hili wameingiza kipengele cha rejesta kwa ajili ya vitambulisho vya taifa nje ya mkataba na baadhi ya sehemu hatujaambiwa tutalipwa shilingi ngapi sasa hapo tutegemee matokeo mazuri?
Kuna watu wanaenguliwa licha ya kujaza mikataba ili nafasi zao zichukuliwe na watoto wa wakubwa au jamaa zao pasipo utaratibu mzuri hivi tutegemee matokeo mazuri?
Tuliambiwa kuna mabegi maalumu ya kuhifadhia madodoso ili yasichafuke lakini ajabu tumepewa madodoso mikononi.
Tuliambiwa tutapewa pesa kwa ajili ya viogozi wa mitaa kututembeza maeneo yao na wameanza kututembeza jana lakini hadi jioni hii hakuna kinachoendelea. Utafikiri ni dharura kumbe ilipangwa miaka kadhaa nyuma. Ubabaishaji huu utaisha lini?
waislam karibu milioni 35 hawatajiandikisha zoezi hili kwa jinsi hamasa ya waislam inazidi kuongezeka siku hadi siku tusubiri tuone!