Hii sasa Imezidi: Dr. Kitila Mkumbo kupandishwa kizimbani kwa Uchochezi!

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katika kile kinachoonekana ni vita sasa kati ya serikali na CDM jeshi la polisi nchini limeamua kumfungulia mashtaka mhadhiri wa chuo kikuu cha DSM na mjumbe wa Kamati kuu CDM Dr Kitila Mkumbo kwa kile wanachodai ni uchochezi wake aliofanya siku alipohutubia mkutano katika kata ya Ndago jimbo la Iramba Magharibi.

Wachunguzi wa mambo wanadai mbunge wa jimbo hilo Mwigulu Nchemba ameapa kutumia kila njia kumzuia Dr Kitila Mkumbo asipate nafasi ya kugombea katika jimbo hilo hasa kutokana na kuwa Dr Kitila ni chaguo la wanaIramba wengi na ana heshima kubwa huki kwao hasa kutokana na hekima na busara zake anapozungumza.

Source: ITV (Dondoo za gazeti la Nipashe la Ijumaa)

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Soma habari yenyewe ndani ya NIPASHE:

Kiongozi mwingine wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amehojiwa na Polisi juu ya vurugu zilizotokea katika mkutano wa chama hicho na kusababisha Mwenyekiti UVCCM Kata Ndago, wilayani Iramba, Mkoani Singida, Yohana Mpinga kupoteza maisha.

Aliyehojiwa na kuachiwa kwa dhamana ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Mkumbo Kitila na alitakiwa kurejea Polisi leo asubuhi, kwa ajili ya kupelekwa mahakamani.

Kamanda wa Polisi Mkoa Singida, Linus Sinzumwa, alisema jana kuwa Kitilah atapandishwa kizimbani kwa kosa la kutoa lugha ya matusi kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika Jumamosi iliyopita.

"Kitila tumehoji na yupo nje kwa dhamana na tunatarajia kumfikisha kesho (leo) mahakamani…anakabiliwa na tuhuma hizo hizo za kutoa lugha ya matusi," alisema Sinzumwa.

Juzi jeshi hilo lilimhoji mkurugenzi Habari na Uenezi wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo John Mnyika kwa saa tatu, kuanzia saa 12 jioni, kabla ya kumwachia huru.

Kuhusu kuhojiwa kwa Mnyika, Kamanda Sinzumwa alisema aliachiwa huru baada ya kuridhika na maelezo yake, lakini wakimhitaji watamwita tena, kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Kiongozi wa kwanza kuhojiwa kuhusiana na vurugu hizo alikuwa Ofisa Sera na Uratibu wa Chadema, Mwita Waitara, ambaye ameshafikishwa mahakamani kwa kosa la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba.

Kutokana na hali hiyo, Kitila ataunganishwa katika kesi hiyo, kuhusiana na vurugu zilizotokea Mkutano wa Chadema uliofanyika Ndago, Iramba Mkoani Singida.
 
Msomi mzima hana akili, naye anasimama kwenye jukwaa tena nyumbani kwao anachochea vijana wake wa kazi kuuwa. Kwa nini hao akina Mbowe hatusikii wakiuawa huko kwao?
 
Hizi mbinu chafu zinaashiria kuwa tusitegemee jipya kwenye KATIBA mpya. Kwanini watu wanang'ang'ania madaraka hata kwa damu ya wanaowaongoza?
 
hawawezi zuia moto, moshi ushaanza kufuka mwigulu wewe ni dada tuu mbele ya CM
 
sijawahi kusikia mtu amepatikana na hatia katika kesi ya uchochezi! ni kupotezeana muda na kupeana stess tu!
polisi ni washenzi sana.
 
Msomi mzima hana akili, naye anasimama kwenye jukwaa tena nyumbani kwao anachochea vijana wake wa kazi kuuwa. Kwa nini hao akina Mbowe hatusikii wakiuawa huko kwao?

***** wewee.. Lusinde katoa lugha chafu hukuona.. huyu hujackia unafunga kibwebwe..!!!Bungeni CDM wanaambiwa wanawashwa. Husemi kama ni lugha ya kuudhi Bungeni kwa kua ni CCM.Hata karipio hakupewa..Sasa kwa taarifa yako na yenu.. Raia Milion 35 hawakupiga kura.. Na tambua JKamechaguliwa na Tume na hilo kundi ndilo linaitaka TANGANYIKA YAO!!hata mkamate mamia lakini MTAONDOKA TU NA OKAMPO MTAMJUA!!
 
acha wazidi kumpaisha...
Hebu wanasheria nisaidieni, si tayari kuna kesi kuhusiana na hili tifu la Ndago na kuna wengine wameshafikishwa kotini? kwa nini wamfungulie kesi tofauti na mashitaka yake na wasimjumuishe..... au ndio character assassination????
 
Katika kile kinachoonekana ni vita sasa kati ya serikali na CDM jeshi la polisi nchini limeamua kumfungulia mashtaka mhadhiri wa chuo kikuu cha DSM na mjumbe wa Kamati kuu CDM Dr Kitila Mkumbo kwa kile wanachodai ni uchochezi wake aliofanya siku alipohutubia mkutano katika kata ya Ndago jimbo la Iramba Magharibi.
Wachunguzi wa mambo wanadai mbunge wa jimbo hilo Mwigulu Nchemba ameapa kutumia kila njia kumzuia Dr Kitila Mkumbo asipate nafasi ya kugombea katika jimbo hilo hasa kutokana na kuwa Dr Kitila ni chaguo la wanaIramba wengi na ana heshima kubwa huki kwao hasa kutokana na hekima na busara zake anapozungumza.

Source: ITV (Dondoo za gazeti la Nipashe la Ijumaa)

ningekuwa mi ndo hakimu,ningetoa hukumu kitila mkumbo apigwe miaka 300 na viboko ishirini,kumi wakati anaingia,kumi wakati anatoka akamwonyeshe mke wake.
 
Naona nchemba ameamua kupigana na yeyote anayeonekana kujitokeza kushindana naye.Kwa jitihada hz anazofanya atahatarisha maisha ya yoyote anayejitokeza kumpinga na cdm wanatakiwa kujua kudeal naye wakikosa busara za kumdhibiti atawaharibia sana.magamba wanamulinda sana huyu mnyela
 
Inaelekea huyu jamaa (Mwigulu) atamwaga damu za watu wengi sana kabla hajaondolewa na uchaguzi wa 2015.
 
ningekuwa mi ndo hakimu,ningetoa hukumu kitila mkumbo apigwe miaka 300 na viboko ishirini,kumi wakati anaingia,kumi wakati anatoka akamwonyeshe mke wake.
ni maoni yako kwa akili yako ikipofikia kufikiri!ni heri kukosa mali kuliko kukosa akili
 
Back
Top Bottom