Hii quote yangu ya leo

howard

Senior Member
Feb 21, 2011
188
28
"Huwarubuni wananchi wao wasio na uelewa kwa kuwafanyia sherehe kubwakubwa zisizo na maana yoyote. Wakirusha ndege moja ya kivita angani, wanawaambia wananchi wainue macho yao juu wayaone maendeleo yao. Maisha bora yanaonyeshwa kwa mizinga na vifaru vya kisasa. Mtu huna adui hata mmoja, lakini kila uendeko una panga mkononi. Ukiitwa chizi unakasirika sasa uitweje?
SOURCE: PASCALLY MAYEGA TANZANIA DAIMA JUMATANO 25/01/2012
 
Nice quote
Kweli kabisa wananchi wanarubuniwa na wingi wa magari barabarani na uwepo wa zana ambazo hata hazina maana
Wakati hali zao za maisha ni duni kupindukia
 
Kwa hiyo mayega anataka TANZANIA isubiri ivamiwe ndio ikanunue silaha?
Ongea mengine,hapo siungi mkono hoja!!!
 
Mkuu,hapo natofautiana na wewe unless useme hizo zana zisizo na maana ni zipi!!!
Pamoja na umaskini,suala la kuwa na zana za kisasa za ulinzi ni jambo muhimu mno hivyo kupinga hili ni wendawazimu!!!
 
Wananchi wanazuiwa kuwasiliana nao wakiandika mabango wananyanganywa na pilisi,wanaamua kupiga kunga wakati wanapozuga kuwatembelea wanashangaa:kwa nini wanalia?
 
Kwa hiyo mayega anataka TANZANIA isubiri ivamiwe ndio ikanunue silaha?
Ongea mengine,hapo siungi mkono hoja!!!

Sidhani kama alimaanisha hilo
Ulinzi ni muhimu na ni wa maana kwa kila taifa
Ila maana yake aliyosema hapa ungeunganisha ujumbe wote ungepata maana
Kuwaonyesha wananchi wako madege ya kivita na vifaa vya kisasa au kila siku kununua vifaa vya kijeshi na kuongeza vipya kuwaonyesha wananchi wako sio alama ya maendeleo wakati wao adui yako mkubwa ni umaskini wao na njaa zao
 
mkuu,hapo natofautiana na wewe unless useme hizo zana zisizo na maana ni zipi!!!
Pamoja na umaskini,suala la kuwa na zana za kisasa za ulinzi ni jambo muhimu mno hivyo kupinga hili ni wendawazimu!!!

kuwa mwepesi wa kuelewa silaha zinazoonyeshwa kila mwaka ni zile zilizotumika 1978 zimepigwa rangi,angalia silaha kenye walizoingia nazo somalia na fuatilia tulizo nazo ndipo utamwelewa huyu jamaa.
Au kwa maana nyingine kama tuliweza kuhifadhi mabomu ya mwaka 47 mpaka yakamaliza ndugu zetu kwa nini ujifanye humwelewi huyu
 
"Huwarubuni wananchi wao wasio na uelewa kwa kuwafanyia sherehe kubwakubwa zisizo na maana yoyote. Wakirusha ndege moja ya kivita angani, wanawaambia wananchi wainue macho yao juu wayaone maendeleo yao. Maisha bora yanaonyeshwa kwa mizinga na vifaru vya kisasa. Mtu huna adui hata mmoja, lakini kila uendeko una panga mkononi. Ukiitwa chizi unakasirika sasa uitweje?
SOURCE: PASCALLY MAYEGA TANZANIA DAIMA JUMATANO 25/01/2012

Sio kila mwanadamu amejaliwa Uelewa wa kwamba anarubuniwa... kwamba anatumiwa na kwamba yeye ni kafara. Hapo kuna wawili; A kuna wale ambao wanarubuni wananchi wao wasio na uelewa na kuwafanyia sherehe kubwa kwa malengo ya kuwatoa kafara - B Na kuna wale ambao waelewa wazi kua wanachi wenzao wanarubuniwa na karibu watatolewa kafara. Lakini hawatingishiki/hangaiki wala thubutu kufanya lolote kuwaonya hao wanachi kua hala hala hio sherehe ni pazia la mabaya yalopangwa na kwamba ndege ya kivita imeendaliwa.

Kati ya hao A & B nani mbaya zaidi? Ni stahili kuwaashutumu wasoelewa kua ni wajinga? Kama nia ya Kundi A ni kujiboreshea maisha na Ubinafi; Je hao kundi B wamepona katika ubinafsi? Huu mchezo mchafu huu..... Enways.... Tuache kama yalivo.
 
AshaDii kuacha kama yalivyo ni dalili ya kukata tamaa
Yaani pamoja na kuteseka kwako bado unaamua kukaa kimya na kuona ni sawa tuu hata wakiendelea kukunyonya na kukupaka mafuta kwa mgongo wa chupa unasema hewala bwana
Hiyo ni mbaya sana
Bora kutafuta alternative ya kuondoa hali hiyo na kumaliza matatizo ya wengi ambao wanaonekana kunyanyasika na mfumo uliopo
Mfumo ambao unawafanya waaminishwe kwamba uwingi na ubora wa ndege za kivita au ndege kuonekana angani na kuwa na magari mengi barabarani ni dalili ya maendeleo wakati mwananchi huyo hana uhakika wa mlo wake wa jioni ni jambo la ajabu sana
Tutafute njia ya kuuondoa mfumo huo wa kigandamizaji bila kuathiri maisha ya hao wanaogandamizwa au kuwapa elimu kuwa hayo wanayoambiwa ni maendeleo sio maendeleo bali ni aina nyingine ya matumizi
Huwezi ukawa na gari na ukaliita kwamba ni mali wakati kila siku value yake inapungua na thamani yake inazidi kushuka kwa kadri unavyotumia
Tutafute namna ya kubadilisha huo na hii mifumo ya kigandamizaji na kiufisadi bila kuathiri maisha ya hawa wanaoonewa na wao angalau wafaidike na raslimali za taifa angalau na ile cake ya taifa waionje
 
Kwa vile wamelala usingizi wa pono kwa miongo mingi waache wachezewe pengine siku moja watafunguka na kufanya kweli kama wenzao huko Misri na Libya!!
 
Back
Top Bottom