Hii "Presidential Delivery Bureau" Huenda ikasaidia kwa kadiri!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Hiki kitengo cha "Presidential Delivery Breau" Kilichoanzishwa hivi karibuni huenda kikasaidia sana katika kuharakisha maendeleo katika nchi yetu.

Kitengo hicho pamoja na mambo mengine kitahusika na kuwajibika katika kufatilia, kuraribu na kuhamasisha miradi yote inayoenzishwa nchini ili kuhakikisha inatekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati.Hii ni kutokana na ukweli kwamba Rais mwenyewe hawezi kujua miradi yote nchini, na kujua yote imefikia wapi na kwa wakati bila kuwa na chombo kama hiki hasa katika kipindi hiki ambacho kuna mawaziri wazembe.

Naamini wazo la kuanzisha kitengo hicho litaweza kupunguza madhara yanayotokana na mawaziri wazembe kwa kiasi fulani , ikiwa kitengo hicho kitasimamiwa na watu makini.
 
Mtatengeneza hadi agencies za kukusanya ushuru wa vyoo vya stand za mabasi
 
Hicho kitengo ni mtu katengenezewa tu ulaji wake hapo hakuna kipya!
Lakini niliona walitangaza ajira na wadau waliomba!Halafu inasemekana kitengo kama hicho kimefanya vizuri katika nchi nyingine. Wewe unasema je?
 
Back
Top Bottom