Hii picha imeniponza!

Majoja

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
612
186
Kama kawaida yangu huwa siachi kamera yangu kwa ajili ya matukio mabali mbali jijini Dar.

Nilipita Ocean Rd na nikaona watu wamepumzika na kupunga upepo.Mimi nikatoa kamera yangu na kuchukua hali ile mwanana.

Mara aktokea Afwande Arufonsi na kuniuliza

"haroo rete kibari chako"

"S..sina.. kibali afwendi kwani kupiga picha hapa inakuwaje" nikamjibu

"Wewe rinatoka wapi, na kama hujui kuwa hapa hakuna ruhusa twende kituoni" Arufonsi akawa mkali

"B... basi afwendi nihurumie nina mke na watoto wanao nitegemea" nikamjibu

"Araaa hutaki kwenda kituoni sioo, ohoo wewe hujui hapa ni njia ya ikuru" bado Arufonsi mkali.

Hapo nikaona nimpooze kidogo,

"Afwande mimi Mbongo pyuwa, na najua hujaweka chochote tumboni, chukua hii kapate ranchi basi"

Kwa mara ya kwanza nikaliona gego la afwande Arufonsi " Nenda sako, hapa mahari pa usarama"

Lets share JF

beach.jpg
 

Attachments

  • CIMG0014.JPG
    CIMG0014.JPG
    222.3 KB · Views: 1,210
Duh, pongezi zako mkuu, picha nzuri sana japo imekugharimu (hujaweka kiasi ulichotoa). Asante picha ni nzuri ila ze kamingi next tymu usitoe rushwa MUNGU hapendi
 
Picha nzuri ila huyo afande angekupeleka klituoni maana umepiga maeneo yake
 
jamaa alikuotea tu.mbona hapo watu wanakaa sana,wanaogelea,wanavuta bange,wanaokota chupa,wanatengeneza nyavu,wanapiga picha?ungempiga picha ukaiweka hapa.mia
 
ni kweli kabisa jamaa walinisumbua sana mwaka 1999 mpaka nilipotoa kitambulisho cha shule na kuwaambia mie sina mbuni kipande kwasababu bado ni kula kulala,ndipo wakaniachie niondoke zangu.Nalog off
 
Picha ni ya kawaida tu hakuna cha ajabu wala kinachozuilika kupigwa hapo !!
 
Ni kweli eneo hilo hairuhusiwi kupiga picha mi mwenyewe enzi za uchaguzi wa mwaka 2000 machafuko ya ccm na cuf nilienda kupozi na rafiki zangu eneo hilo la Ikulu tukawa tunapiga picha du tulikamatwa tukaingizwa ndani ya Ikulu jamaa wakidai sisi ni wafuasi wa cuf tunataka kuvamia Ikulu tulilushwa kichura chura mwishowe walipoona hatueleweki kwenye suala la Rushwa wakatuachia
 
Alikuona zooba mzee si unajua tena kule CCP wanafundisha na jinsi ya kumbana raia atoe chochote hata kama hajafanya kosa.......Bongo Dar is Salaaama hiyo.
 
Nilipita Ocean Rd na nikaona watu wamepumzika na kupunga upepo.
..................

"......... ohoo wewe hujui hapa ni njia ya ikuru" bado Arufonsi mkali.
Sasa hapo ikuru JK mbona simuoni kwenye picha?
Arufonsi inaelekea ni mradi wake
 
Ni kweli eneo hilo hairuhusiwi kupiga picha mi mwenyewe enzi za uchaguzi wa mwaka 2000 machafuko ya ccm na cuf nilienda kupozi na rafiki zangu eneo hilo la Ikulu tukawa tunapiga picha du tulikamatwa tukaingizwa ndani ya Ikulu jamaa wakidai sisi ni wafuasi wa cuf tunataka kuvamia Ikulu tulilushwa kichura chura mwishowe walipoona hatueleweki kwenye suala la Rushwa wakatuachia
Hilo sio eneo la ikulu ni ocean road near GYMKANA GROUNDS IT HAS NO PROHIBITION FROM TAKING PHOTOGRAPH
 
Usirudie kuripa rirushwa rire riArfonsi. Ukiriona tena risiku ringine riambie ww ni mdogo wa rire riafande Angerina ritaogopa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom