Hii nimeipenda - Ving'ang'anizi wa madaraka hii inawafaa sana

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Gbagbo huyoo na aibu yake
LAURENT.jpg
 
Aibu ya Gbagbo ni aibu ya Africa na pia inaonyesha double standard ya Mataifa ya Ulaya na hata AU yetu. Viongozi wengi sana katika Africa wangekuwa wamekutwa na aibu ya kuvuliwa nguo kama Gbagbo kama kweli hao Watawala (Mabeberu tu)wetu wa zamani wangekuwa wameamua kama walivyoamua kwa Ivory Coast. Nakumbuka ktk uchaguzi Allasane Outtara alitangzwa mshindi na tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC ya Ivory Coast) na kwa kuwa Gbagbo alikuwa na dola akaiamuru Mahakama imtangaze yeye!! Alifikiri itakuwa kama Kenya ama Zimbabwe lakini yamemkuta. Ilikuwa Mugabe na Kibaki nao wavuliwe nguo awali kama Gbagbo. Wao pia walilazimisha tume ziwatangaze na watu kuuwa. Africa kunaweza kuwa na uchaguzi huru ila hakuna vyombo huru vya kutangaza matokeo. Kilio ni kikubwa katika hii demokrasia yetu ya kuungaunga!!
 
Hapa kwetu Tanzania wamegundua staili mpya ya kuwepo madarakani. Yusuf Makamba ameondoka, kaingia January Makamba. Moses Nnauye kafa, kaingia Nape NNauye, Ali Hassan Mwinyi atakuwa CC ya CCM na mwanaye Hussein Mwinyi. Mama Fatma Karume nilimsikia juzi akisema familia yake haitaacha siasa.
 
Aibu kweli... Halafu alitamka hadharani kuwa hapendi kufa, anapenda maisha, hayuko tayari kufa kwa sasa. Sijui mshkaji alijiamini nini? Tatizo la viongozi wa Afrika wengi ni vilaza, wanategemea ushauri wa viongozi waongo wanaotoa ushauri unaolinda maslahi binafsi. Huenda walikuwa wanamdanganya kuwa jeshi lake lina uwezo mkubwa kupambana na kushinda ndio maana kakomaa, lakini mwisho wake ndio hivyo tena aibu.
 
Back
Top Bottom