BIG X
JF-Expert Member
- Nov 4, 2011
- 777
- 212
Niliingia duka moja kununua sandroz, bahati mbaya nilikuwa nimevaa viatu. katika harakati za kutaka kujaribisha nikavua viatu, nikazijaribisha zile sandroz nikiwa na soksi, nikawambia hizi ngozi yake ni ngumu sana itabidi mtu awe anazivaa na soksi. Pale dukani wakacheka sana wakasema utavaaje sandroz na soksi, wakasema "watu watakushangaa sana watajua unatoka Tanzania mana ndio wanaovaaga hivyo" mi niliposikia nilishangaa sana, sikuelewa kwanini walisema vile, Nilipowaambia mi natoka hukohuko wakasema basi kama ni hivyo hamna shida unaweza ukazivaa na soksi.
Sasa hii ilinipa mtihani kutaka kujua ilikuajekuaje mpaka ijulikane kwamba watanzania ndio wanaovaaga hivyo!!! lakini nilikuwa na muda mfupi sikuweza kufanikiwa.
Kama kuna mtu amekutana/anaelewa hili vizuri amwage hapa.