Hii ni sawa...?

Runner

Member
Feb 7, 2011
85
13
Mkeo umemuoa akiwa tayari ana mtoto,na ukakubali kumuhudumia mtoto kwa mahitaji yake yote,lakini inakuja kwamba bado anawasiliana mara kwa mara na mwanaume aliyezaa nae kwa namba nyingine tofauti,na ikitokea umesika anaongea anakwambia naongea na rafiki yangu,ukummbana sana anakwambia nilikuwa naongea na baba wa mtoto kuhusu mambo yahusuyo mtoto,je utafanyaje?Wana JF hebu nipeni maoni yenu
 
Hapo inabidi uwe serious kidogo..uongee nae aache kabisa hiyo tabia! Hawachelewi kukumbushia
 
si mkeo uyo
uyo ni mke wa jamaa aliyezaa nae
wanapendana nae sana
wewe amekubali kuoana nae kwa sababu ya maisha lakin mapenz bado yapo kwa uyo aliyezaa nae
mwambie astop la sivyo mtishie ...UNATUMIKA WEWE..KWAKO KIMAISHA LAKIN hakupend

km asingekuwa anakucht na uyo jamaa bas wakat anapiga asingekuw anajificha na angekwambia .like ehh nannii anapiga asjui anataka nini lakin ukiona anaenda ongelea nje bas ujue unazungukwa braza

ikiwezekana waambie ndg zake juu ya jambo ilo...SI AJABU ONE DAYA AKAKWAMBIA M SOR M GOIN BAK TO MY X...mmezaa kwan?
FUNGUA MACHO..UNALIWA..HAWAJAACHANA AO..wewe wanakufanya kibuz tu cha kuwalelea mtoto wao.

sor lakin
 
Mwambie mkeo marufuku kuwasiliana na huyo aliekutangulia,kama baba mtoto anataka kumuona mtoto awasiliane na wewe mpange ni lini anakuja kumuona au kumchukua kwa muda matembezi.Hilo la kuwasiliana kwa kificho kinaleta wasiwasi.
 
sasa utazuia mtu kuwasiliana na mzazi mwenzie?? As long as huyo jamaa yuko hai, na inategemea na mazingira yaliyofanya wasiishi pamoja... then wataendelea kuwasiliana... with or without your consent....
 
Tatizo sio mawasiliano bali ni mawasiliano ya siri!Sio vibaya kujuliana hali ya mtoto na mengine yanayomhusu ila anatakiwa amshirikishe mumewe!Yeye ndo mumewe na mtoto analea hivyo anastahili kujua nini kinaendelea kama kinamhusu mtoto!
 
Hapo kosa analofanya ni kujificha, na hapo ni mawili:-
  • Either anaficha sababu ana lake jambo ambalo sio zuri kwa uhusiano wenu
  • Au anaogopa ukijua kwamba anawasiliana na EX utapata mawazo potofu, tadhani anacheat na utaumia, hivyo hataki kukuumiza
So its up to you kujua kipi ni kipi na muonyeshe kwamba mawasiliano na EX wake sio vibaya kwa issue za mtoto ila wewe kama baba mlezi inabidi akuhusishe kwenye kila decision
 
Mkeo umemuoa akiwa tayari ana mtoto,na ukakubali kumuhudumia mtoto kwa mahitaji yake yote,lakini inakuja kwamba bado anawasiliana mara kwa mara na mwanaume aliyezaa nae kwa namba nyingine tofauti,na ikitokea umesika anaongea anakwambia naongea na rafiki yangu,ukummbana sana anakwambia nilikuwa naongea na baba wa mtoto kuhusu mambo yahusuyo mtoto,je utafanyaje?Wana JF hebu nipeni maoni yenu

Kwanini uoe mwanamke ambaye tayari ameshazalishwa, and funny enough aliyemzalisha yupo hai?
 
mnh,kama wewe unalea then lazima ushirikishwe kwenye hayo mawasiliano,
otherwise mpige mkwara mkeo kama hataki kukushirikisha then susa kumlea,mpelekee baba wa huyo mtoto naye aleee!!!
huku kwa nchi za watu nimeona mtoto anapelekwa ktk familia zote mbili analelewa!!!! hakuna kukwepa wajibu!:twitch:
 
Kwanini uoe mwanamke ambaye tayari ameshazalishwa, and funny enough aliyemzalisha yupo hai?

Nadhani love haichagui mazingira, bali ni kwa kiasi gani mnapendana kiukweli/kiudhati,
''Kwa nini uolewe na mwanaume ambaye alishazaa/anamtoto' ??
 
Kwanini uoe mwanamke ambaye tayari ameshazalishwa, and funny enough aliyemzalisha yupo hai?

Kwani dhambi? mbona hii iko low sana.
Either mwanamke or mwanaume akizaa anastahili kuolewa.
Wenginen wamezaa kwa kudanganywa, wengine wamebakwa. ..

Kwa hiyo mwanamke akizaa tu hastahili kuolewa?
 
inabidi ukodi inteligensia ya Mwema, nina ushahidi wa ndugu yangu katika swala hilo, anapata taabu sana! na anaelekea kukata tamaaa kabisa. Mwambie ampeleke mtoto kwa baba yake.
 
dah! Pole sana kaka ila jaribu kuongea nae taratibu anaweza akaelewa
 
as long ulisha amua kumuoa akiwa na huyo mtoto,swala kama hilo ni kutegemea,huwez wazuia wasiwasilane,mana yawezekana yye ndo aloachwa-but bado anampenda huyo ex wake
 
ongea na mkeo na umshauri simu ya mawasiliano na kujuliana kwa mtoto itumike ya kwako.
lkn wanawake na sisi hata hatueleweki na hatusemagi ukweli some tymz, kama kweli anakupenda kwa dhati asingefanya mawasiliana na X wake tena kwa siri na no ya simu maalum!
 
Sio saw kabisa, kama kuna mawasiliano ya siri kuna lao jambo, just chunguza, kama vipi mtoto achukue na kumpiga maufuku mawasliano, ili kusiwe na kisingizio.
 
Pole sana,ni vizuri kufahamu kuwa wanazungumza nini na nani ana initiate mazungumzo.....ukimwambia kama ana lake atajificha tu na kuwa makini usijue,nakushauri kaa nae chini kwa upole,muulize kulikoni,kuna kitu hakipati kutoka kwako hadi awasiliane na huyo baba mtoto wake au bado ana feelings nae?then,usimuulze tena ila uwe unamfuatilia kwa siri,baada ya muda utaujua ukweli na hapo ndo itakapokulazimu kufanya uamuzi.......
 
Bro hapo kuna kitu kiko chini ya kapeti. Kwanini wafanye mawasiliano ya siri?? Halafu kama kutunza wewe ndio unagharamikia sasa wanaongea nini?? Kama mtoto hajambo hata dk haiiishi hapo kaa chonjo mkuu unazungukwa
 
Kwani dhambi? mbona hii iko low sana.
Either mwanamke or mwanaume akizaa anastahili kuolewa.
Wenginen wamezaa kwa kudanganywa, wengine wamebakwa. ..

Kwa hiyo mwanamke akizaa tu hastahili kuolewa?

Kwa hiyo alikuwa anaongea na huyo mdanganyaji au mbakaji kwa siri? mi naona huyo mama amefanya vibaya kuongea kwa siri alitakiwa kumshirikisha mumewe kwa kila kitu aongeacho na huyo mzazi mwenzake na kama amefanya hivyo inabidi umwambie akuweke wazi kama anaendelea nae kimapenzi mkishapatana mumuite au mpange mahala mkutane na mzazi mwenzake pamoja na watu wazima ili muongee na kuwekeana mipaka
 
si mkeo uyo
uyo ni mke wa jamaa aliyezaa nae
wanapendana nae sana
wewe amekubali kuoana nae kwa sababu ya maisha lakin mapenz bado yapo kwa uyo aliyezaa nae
mwambie astop la sivyo mtishie ...UNATUMIKA WEWE..KWAKO KIMAISHA LAKIN hakupend

km asingekuwa anakucht na uyo jamaa bas wakat anapiga asingekuw anajificha na angekwambia .like ehh nannii anapiga asjui anataka nini lakin ukiona anaenda ongelea nje bas ujue unazungukwa braza

ikiwezekana waambie ndg zake juu ya jambo ilo...SI AJABU ONE DAYA AKAKWAMBIA M SOR M GOIN BAK TO MY X...mmezaa kwan?
FUNGUA MACHO..UNALIWA..HAWAJAACHANA AO..wewe wanakufanya kibuz tu cha kuwalelea mtoto wao.

sor lakin

Punguza hasira.
 
Back
Top Bottom