Hii ni nini na tiba yake ni nini?

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
303
154
Wana jukwaa!!
Mimi nina mtoto ana umri wa mwezi mmoja na nusu. wiki tatu zilizopita alitokewa na layer fulani hivi mdomoni as if amekunywa maziwa yaliyoganda. Nilimpeleka kwa wataalamu wakampa dawa flani inaitwa NYSTATIN. Nimempa dawa hiyo laini naona bado hali hiyo inaendelea. Wapo walioniambia nimpe asali lakini nayo haijasaidia. Ninachoshukuru ni kuwa ananyonya vema, amechangamka na zaidi ya yote MIMI NA MAMA YAKE WOTE NI SALAMA na MTOTO NI SALAMA(We are out of HIV infection). NITATATUA VIPI HILI?
 
Hongere kwa kuwa na familia salama na pole kwa matatizo. mi nadhani ungejaribu kumpeleka tena hospital kwa wataalam zaid wanaweza kumbadilishia dawa kwani sio dawa zote zinazoponya. Usikate tamaa atapona.
 
Mkuu ni bora ukaenda seriously kw a wataalamu wa magonjwa ya watoto wafanye kazi yao, wala usichelewe usije kumtia mwanao kilema bure!
 
Kweli ndugu mpeleke mtoto hospitali halafu mimi binafsi nikienda hospitali baada ya vipimo huwa napenda kujua naumwa kitu gani na nini kimesababisha. Sasa wewe dk. alivyokuandikia dawa hakukueleza tatizo la mtoto ni nini na chanzo chake ni nini? Nafikiri jitahidi urudi Hospitali kwa madk. bingwa wa watoto wamsaidie mtoto mapema iwezekanavyo usizembee tena mtoto ni mdogo sana asije akalemaa. Pole sana.
 
Huo utando ni fungal infection,mwanangu pia aliwahi tokewa na hiyo nystatin ilimponyesha. Mpe as directed itakwisha. Usimchanganyie dawa,be patient.

Pole sana coz i know how yo feeling.
 
pole sana mkuu, fuata ushauri wa wataalam haraka sana. Naamini kwa juhudi za madaktari mtoto atapona. Pole sana na hongera kwa kupata mtoto.
 
Back
Top Bottom