hii ni kawaida jamani??

Nilham,

Kwa nini usiwe na raha siku ya birthday? Mie mwenzio tangia nilipofikisha miaka arobaini, nimeamua kila Ijumaa nifanye sherehe ya birthday. Kila mwaka ninakuwa na birthday parties angalau 52! Ukumbuke Nilham, furaha inakuongezea umri wako wa kuishi (other things remaining equal).

Ni vema kwamba unampenda mama yako, lakini nakushauri ukitaka furaha ya kweli wapende watu wote. Mie kwa mfano, nilimpenda sana mama yangu, lakini akafariki nikiwa na umri mdogo wa miaka 17. Hata hivyo namshukuru Mungu kwamba nimeweza kuishi na sasa nimeishi miaka mingi na walimwengu, ndugu na rafiki, zaidi ya niliyoishi na mama.

Birthday yako ni lini? Mungu akubariki.
 
wellcome N! pole sana kwa hayo: lakini hujatuweka wazi kuwa kilio chako huwa ni cha FURAHA au HUZUNI? unaweza ukawa mnyonge labda kwa ajili ya stress za kuandaa sherehe yako, lakini pia ukalia kwa sababu umefanikiwa kutimiza hasma yako, au ukawa mnyonge na kujikuta kulia kwa sababu hukutimiza kiwango cha maandalizi uliyotarajia-pengine ukiwa unajaribu kufikia kiwango cha rafiki/member wa familia! hebu weka bayana hali halisi!
pili: unasema mama ndiye mara nyingi anakuliwaza: je una wazazi wote wawili, mpenzi??:kama siyo, pengine unapoona waalikwa wako wameambatana na wapendwa wao wa karibu unajisikiaje???
 
Nilham unaweza kuwa unampenda sana mama yako ila unajihisi upweke cause unamiss kitu, labda mapenzi kutoka kwa umpendae wa rohoni yaan soulmate hii pi inawezekana.na hali inaweza kuwa hivyo hata kwa muhusika kutokujua ila ndio hivyo. embu angalia na hili pia.ni maoni tu
 
Huo ni ugonjwa.....ukatae ukubali mimi nakwambia.. tatizo hilo wanalo wengi na hasa katika furaha yaani furaha inakumiliki baada ya wewe kuimiliki furaha ''you must cry'' mfano kuna miss au mlimbwende mmoja aliulizwa na mwandishi wa habari kwanini yeye hakulia baada ya kutangazwa mshindi kama wengine wanavyolia baada ya kutangazwa washindi.......alijibu ''kwakuwa furaha yangu haikunimiliki''.

ok; ndiyo mlimbwende pekee ambae inasemekana alikuwa na akili kuliko walimbwende wote waliowahi kutokea licha ya uzuri wake.

Tunatembea lakini ni wagonjwa na hatujijui.....dunia ya tatu ndivyo ilivyo.
 
ahsante kwa ushauri,,,ntaufatilia inshallah lakini mi kawaida yangu sichagui.... nampenda kila mtu na watu nao nashkuru alhamdulillah wanipenda pia si mama tuu...:wink2:
Nilham,

Kwa nini usiwe na raha siku ya birthday? Mie mwenzio tangia nilipofikisha miaka arobaini, nimeamua kila Ijumaa nifanye sherehe ya birthday. Kila mwaka ninakuwa na birthday parties angalau 52! Ukumbuke Nilham, furaha inakuongezea umri wako wa kuishi (other things remaining equal).

Ni vema kwamba unampenda mama yako, lakini nakushauri ukitaka furaha ya kweli wapende watu wote. Mie kwa mfano, nilimpenda sana mama yangu, lakini akafariki nikiwa na umri mdogo wa miaka 17. Hata hivyo namshukuru Mungu kwamba nimeweza kuishi na sasa nimeishi miaka mingi na walimwengu, ndugu na rafiki, zaidi ya niliyoishi na mama.

Birthday yako ni lini? Mungu akubariki.
 
tanx dinnah..
Nilham unaweza kuwa unampenda sana mama yako ila unajihisi upweke cause unamiss kitu, labda mapenzi kutoka kwa umpendae wa rohoni yaan soulmate hii pi inawezekana.na hali inaweza kuwa hivyo hata kwa muhusika kutokujua ila ndio hivyo. embu angalia na hili pia.ni maoni tu
 
shukran my dear msema kweli siku zoote huwa karibu na allah mi huwa nafunga siku moja tuu kabla ya ile siku kama ni kesho nafunga leo au baada maana ndio nadhiri nilioweka baada yakuwa na faham... inshallah na kwa ulivyonisihi ntatekeleza allah isalimk jamiya ya raab...?
Jitahidi ifikapo siku yako kuzaliwa basi 'funga sunna', na ikibidi jitahidi siku 3 kabla ya birthday yako 'funga na zingatia ibada' kwa karibu saana. Hii ni ishara za shukrani njema kwa muumba wako.
LANGU: Katika hali za kiuchamungu...machozi huwa ni sehemu ya imaan ya mwaminio, zingatia.
 
hehehehehe mie siwazi hivyo lakini....maana binaadam lazma uweke neno kifo kichwani mwako,,, na kila siku ni lazma ukumbuke kuwa kuna siku itafika utakutana na death...na ukiwa huwazi hili jambo basi inasemekana kuwa mwepesi wa kufanya dhambi na maass,, inshallah allah atuepushie maas na maovu,,,(ameen)..
Katika tamaduni za western China sherehe ya kuzaliwa uwa ni sawa sawa na msiba - Wao wanaamini kuwa unakaribia kufa (right?)...

Birthday inakuwa siku ya kukufariji ku-accept death!
 
sina tatizo wallah katika maisha yangu namshkuru allah alhamdulillah..... na sababu inayonipelekea kuwa na simanzi kwa siku ile huwa nawaza kumuomba mama radhi napanga kama maneno mama nisameh kwa kila nilichokifanya kikakuudhi,,, huenda nikawa namtizama yeye tuu nikimshkuru kwa dhati lakini huwa sitamki neno lolote na yeye akiniona natoka machozi kwa siku ile huwa anisogelea sana karibu na kunifurahisha na mazungumzo mengine.... subhanallah mpaka wakati mwengine huwa najiuliza hivi huwa anafaham vipi kitu gani chanisumbua kwa siku ile maana utakuta hata na sababu haniulizi ya kulia ila atanambia maneno yanayoendana na nnavyowaza mie... na wakati mwengine huwa nalia kwa furaha tuu,,,, kama nilivyoambiwa hapo juu kwamba inakuwa inanitawala sijui?? hehehehehhehe...but inshallah everrything gona be allright... tanx...:wink2:
Tatizo kubwa ni hilo (in red). Bila kujua sababu ya jambo, ni vigumu kupata ufumbuzi wake.

Kwa kweli, si kuwa sababu huijui sababu, bali usichokijua ni njia tu za kuifukua hiyo sababu. Moja ya njia hizo ni "kujitambua (self awareness)". Hili linahitaji maelezo marefu lkn ngoja nikushauri hivi: Kaa peke yako ktk sehemu ambayo kwako ni tulivu sana; ambayo hutapata bughudha yoyote -- vizuri ikiwa ni chumba kitupu au kisicho na samani (furniture) nyingi. Weka stool au kiti ktk kona mojawapo mbali nawe. Kisha mweke NILHAM ktk stool/kiti hicho. Sasa anza kumchunguza NILHAM kwa undani, historia yake tangu utotoni, maisha yake mtaani, shuleni, n.k., mambo anayoyapenda na asiyoyapenda; kwa kifupi, everything about her. Kubwa zaidi, chunguza udhaifu wake (huna la kuficha kwa sababu upo wewe, kivuli chako -- NILHAM in qn -- na Mwenyezi Mungu; wote hao hawawezi kutoa siri zako). Mtafiti pia NILHAM ili uweze kujua utatuzi wa kila tatizo na kikwazo. Ukiwa mkweli kwa NILHAM utajua mengi mno kumhusu yeye, na hivyo utajua pia njia za kutatua matatizo yake na kufukua uwezo na vipaji vyake.
 
Pole sana, hiyo ni hali inayowatokea watu wengi huenda ni ugonjwa!
 
Pole NR, kuna sehemu umesema kuna wakati unatamani umuombe mama msamaha kwa yote uliomkosea. Sio vibaya ukifanya hivo lakini sio lazima hiyo siku ya birthday. May be kuna uponyaji unaweza ukaupata kupitia hilo. Manake sisi watoto wa kike bwana kuna wakati unaweza ukakupitia ukajikuta unamdharau mama tu bila sababu ya msingi......lakini unapopata akili za kiutu uzima unajikuta unajutia.

Halafu naomba usimbebe sana mama moyoni, sina maana usimpende hapana, mpende mama, masaidie, mjali lakini kumbuka pia huyo sio mali yako ni mali ya Mungu pia. Kwa sababu ukimbeba sana moyoni siku mwenye naye akimchukua (MUNGU) utaumia zaidi na utakuwa na majeraha ya moyo yasiopona mapema.

Be blessed NH!!!
 
Dah!
Pole nilham.
Mi pia nina tatizo kama lako ila sio kwenye birthday.
 
tanx my dear,,,, inshallah i will do dat,,,, si kwamba nilikuwa nilkimdharau mimi tangu utoto ninavyoambiwa na kaka zangu nilikuwa siwekwi mbali na mama na katika kumbukumbu zangu hakuna siku niliyowahi kumdharau kwa lolote sijui nilipokuwa sina faham nzur,,,, lakini hii hal sijui wallah sijui yasababishwa na nini ispokuwa jambo kubwa inakuwa ni kama kumshukuru ndio kama nilivyosema mwanzo...na wengine wanambia ni kwa ajili ni mimi tuu ndio mtoto wa kike katika familly ndio sababu,,, inshallah ntajitahid kujipukurusha...
Pole NR, kuna sehemu umesema kuna wakati unatamani umuombe mama msamaha kwa yote uliomkosea. Sio vibaya ukifanya hivo lakini sio lazima hiyo siku ya birthday. May be kuna uponyaji unaweza ukaupata kupitia hilo. Manake sisi watoto wa kike bwana kuna wakati unaweza ukakupitia ukajikuta unamdharau mama tu bila sababu ya msingi......lakini unapopata akili za kiutu uzima unajikuta unajutia.

Halafu naomba usimbebe sana mama moyoni, sina maana usimpende hapana, mpende mama, masaidie, mjali lakini kumbuka pia huyo sio mali yako ni mali ya Mungu pia. Kwa sababu ukimbeba sana moyoni siku mwenye naye akimchukua (MUNGU) utaumia zaidi na utakuwa na majeraha ya moyo yasiopona mapema.

Be blessed NH!!!
 
Kila birthday mvua zinaogezeka na una approach to the end, unadhani kwanini wazee wengi hawapendi kufanya birthday? Their birthday means approaching to the end. utasikia ah hizo ni sherehe za watoto.. :A S 13: dont cry enjoy your day.. ni ,mawazo tu
 
Back
Top Bottom