Hii ni kawaida ama nina shida gani mimi?

Chilli

JF-Expert Member
Jul 17, 2011
1,655
743
Nilisoma thread ya memba flani ambaye alipata ndoto kwamba kuna ndege itapata ajali na nikasoma nyingine kuhusu ndugu aliyekua anakabwa sana usiku. Thread hizo ndizo hasa zilizonisukuma na mimi nitoe hili ambalo nimekua linanisumbua maishani mwangu, japo sijawahi mwambia mtu.
Nikikosana ama kukorofishana na mtu halafu nikimchukia ama kumkasirikia huyo mtu basi huwa huyo mtu anapatwa na balaa flani au anaandamwa na mikosi.
Mtu wa kwanza kuligundua hili jambo hili alikua mama yangu mzazi, nikiwa mdogo sana nilisikia siku moja mama akimuhadithia shogake (jirani yetu) lakini sikutilia maanani ila nilivyokua mkubwa ndiyo nilielewa.
Baadhi ya matukio ninayoyakumbuka ni
1. Nikiwa shule ya msingi, kuna mwanamama alikua anauza mafenesi akanidhulumu hela yangu, nikakasirika sana na nikalia sana. Kuanzia hapo huyo mama alikua kila fenesi analoleta limeharibika hadi akaacha hiyo biashara.
2. Nikiwa advance, kuna jamaa tulipigana na nikamwambia utaona, baada ya wiki jamaa akakamatwa mtaani akawa suspended na hakurudi tena shule.
3. Nikiwa chuo kuna dada mmoja alikua girlfriend wangu na tukaachana, alinitukana sana na nikamchunia. Yule dada aliandamwa na sup hadi akaja kuniomba msamaha
4. Nikiwa chuo kuna jamaa mmoja tulikosana naye, baada ya wiki kama moja hivi alidisco.
5.kuna mwalimu alinipiga sana nikiwa shule ya msingi, nilimchukia na nikajisemea rohoni natamani afe, baada ya miezi kama mitatu yule mwalimu aliugua akafa.
6. Ni juzo tu kuna jamaa mmoja alinidhulumu hela flani, nimeshtuka kukutana na huyu bwana wiki iliyopita akiwa chizi.
Matukio kama haya ni mengi sana hadi inafika kipindi mtu akinikasirisha namuomba Mungu asije akapatwa na makubwa.
Nisaidieni wakuu, hii hali kweli ni ya kawaida, binafsi sidhani kama ni coincidence kwa haya yanayotokea!!.
 
Hapo kwenye nyekundu hapo hebu fafanua mtihani ulifanyika lini?ukasahihishwa lini na majibu kutoka ndani ya wiki mojahiyo hiyo mliyokorofishana?Mmhhhhhh:scared:
 
Ushauri wangu Muombe Mungu akuonyeshe jinsi ya kuzitumia hizo nguvu ulizonazo vizuri..Mungu atakuonyesha tuu kitu gani unatakiwa kufanya.
 
Hapo kwenye nyekundu hapo hebu fafanua mtihani ulifanyika lini?ukasahihishwa lini na majibu kutoka ndani ya wiki mojahiyo hiyo mliyokorofishana?Mmhhhhhh:scared:

Kipindi nakosana na huyu jamaa ilikua ndio tunaingia kwenye UE, jamaa alikamatwa na nondo.
Halafu ondoa wazo kwamba this is is a false story. Nitunge ili nini?
 
Mtu wa kwanza kuligundua hili jambo hili alikua mama yangu mzazi, nikiwa mdogo sana nilisikia siku moja mama akimuhadithia shogake (jirani yetu) lakini sikutilia maanani ila nilivyokua mkubwa ndiyo nilielewa.
................................................

Kabla sijaendelea mkuu naomba nijue: Maza-ako wapi anaishi?
 
pole na hongera kwa kujitambua. lililopo ni kutumia busara na kujiepusha na kuchukia/kuchukizana na watu. umejaribu kum-wish mtu kitu kizuri na kwa uwezo wako ukangundua kimemtokea? labda jaribu that side ili uone ni kwa jinsi gani utaweza kukitumia kipawa chapo +vely. vinginevyo mkuu utatisha. watu watakukimbia. umeahi kuiona movie ya the omen? kumbuka greatest talents come with greatest responsibilities.

naamini pia ukiamua now that unajua abilities zako, kukitumia kipawa chako maliciously kita-back fire dhidi yako we mwenyewe au watu wakuhusuo
 
Hakuna kitu chochote cha ajabu hapo huenda ni incidence tu ambazo huenda hao watu unaokorofishana nao zinawakuta na wewe kwa akili yako finyu unadhani wewe ndio chanzo. Haya mi nimekuponda humu nichukie tuone kitatokea nini?
 
Hata mimi mwanzoni kwa hizi akili unazodai ni finyu nilifikiria hivyo, lakini matukio yanazidi kuongezeka hadi naanza kupata hofu.
Halafu, mi siipendi hii hali na wala sioni fahari kuwa hivi ndio maana nikaisema na ndiyo maana siwezi kukasirishwa na maneno yako Sajenti.
Kiukweli hali hii inanishangaza.
 
Daah! Ukishangaa ya musa utaona ya firauni! By the way, knowing the problem is the apex of solving the problem'! Kwa vile umeshajigundua ni vizuri ukawa mwangalifu katika maamuzi yako! Haya mambo yapo na kiukweli huwezi kukwepa kukasirika ktk ulimwengu huu! Cha msingi unapokasirishwa usimnuie mtu huyo mabaya! Take it easy! Yaani usiendelee kumuwazia huyo mabaya kila unapokumbuka baya alilokufanyia! Na kwa vile wewe ni mkristu, Yesu alisema: waombeeni mema hao wanaowaudhi ninyi! Na tuwapende adui zetu...hakuna haja ya kuchukia hovyohovyo! Kila la kheri!
 
utakuwa mtumishi wa Lucifer inabidi uokoke kama we ni mkristo mpe Yesu maisha yako
sitashangaa baadae ukaja kuwa mganga wa kienyeji kama hutaokoka au kuwa shekhe
sali sana kijana.
unaposoma hapa angalia avatar yangu mwanga unaongaa utakuingia na ggafla utaanguka na ndio itakuwa mwisho
wa kuwa mtumishi wa Lucifer.
 
Hakuna kitu chochote cha ajabu hapo huenda ni incidence tu ambazo huenda hao watu unaokorofishana nao zinawakuta na wewe kwa akili yako finyu unadhani wewe ndio chanzo. Haya mi nimekuponda humu nichukie tuone kitatokea nini?

kazi unayo ndugu...usije kutuambia jamaa nam-pm kumuomba msamaha simpati..
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom