Mallaba
JF-Expert Member
- Jan 30, 2008
- 2,554
- 47
Penina Tiamaru
Florence Majani
NATAMANI hata kufa, hali niliyonayo inanipa mzigo mzito, wakati mwingine najiuliza kwa nini jambo hili limenikuta mimi? Roho inaniuma sana, nimekata tamaa kama siku moja nitaishi maisha yenye amani kama wengine (analia), huyo ni Penina Tiamaru (29), mkazi wa Mbezi Salasala, mtoto wa sita wa aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana, Mikocheni, marehemu Obeid Tiamaru.
Hawezi kuisahau Januari 2007, ndoto zake za kuwa mwalimu zilipoyeyuka baada ya kupata ajali ya mguu... Nilikuwa natoka nyumbani kwetu Mikocheni nakwenda kwa jirani yetu, nikawa navuka mfereji na kwa bahati mbaya nikateleza, mguu wa kushoto ukageuka, nikaukanda kwanza kisha nikaenda Hospitali ya Mwananyamala kupata matibabu.
Anafafanua kuwa baada ya kufika hospitalini hapo, madakatari walimkagua bila kusema chochote na badala yake wauguzi wakaanza kumchoma sindano za powersafe pamoja na dawa ya maumivu diclofenac.
Siku nne zikapita bila kupewa huduma nyingine ya ziada, nilikuwa na maumivu makali sana na mguu ukiwa umevimba kuliko kawaida tena umejaa malengelenge, ilinibidi niwaulize wauguzi kuhusu matibabu yangu wakaniambia kuwa mashine ya X-ray imeharibika, basi nikawa nasubiri ingawa nilikuwa katika mateso makali.
Anasema kwamba alikaa hospitalini hapo kwa zaidi ya wiki moja, ndipo siku moja jopo la madaktari lilipopita na kubaini kuwa hali ya mguu wa mwanamke huyo ilikuwa mbaya.
Baada ya madaktari kuniona vile, nikapewa rufaa niende Muhimbili, nikabebwa katika gari la wagonjwa nikapelekwa lakini cha ajabu, baada ya kunifikisha tu mapokezi muuguzi na dereva walionisindikiza waliondoka huku wakinitupia faili langu bila kutoa maelekezo yoyote. Madaktari wa Muhimbili walinipokea, nikaingizwa wodini na siku hiyo hiyo nilipelekwa katika chumba cha xray.
Anasimulia kwamba majibu ya Xray yalipotoka yalionyesha kuwa mfupa mkubwa unaoshikilia kikanyagio cha mguu umechomoka na siku hiyo hiyo saa tatu usiku iliamriwa aingizwe katika chumba cha upasuaji.
Baada ya operesheni nilifungwa vyuma vya kuunganisha mifupa pamoja na jiwe la kilo tano kwa ajili ya kuifanya damu itembee, nilikaa hospitalini hapo kwa zaidi ya miezi minne, anasema mwanamke huyo mwenye umbile kubwa linalozidi kumpa shida wakati wa kutembea.
Chanzo cha ulemavu
Penina anasema hata baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani, alishangaa kuona mguu wake hauendi mbele kama kawaida, akajaribu kuwaambia madaktari lakini walimtia moyo kuwa utanyooka tu na kuwa autembelee vivyo hivyo.
Muda mrefu ulipita lakini mguu wangu ukawa haunyooki ndipo nilipokwenda kujaribu matibabu katika hospitali binafsi iliyopo Kibaha ambako niliambiwa kuwa madaktari walionifanyia upasuaji walikosea na kwamba mfupa mkubwa haujaungana na unyayo na ndiyo maana mguu haunyooki kama ulivyokuwa mwanzo.
Anasema baada ya kufanyiwa upasuaji, madaktari wa Muhimbili walimwambia alale chali akiwa amenyoosha miguu na kuilaza ili mifupa iliyoachana iungane jambo ambalo akiwa Kibaha alielezwa kuwa hayo hayakuwa masharti kwa tatizo kama lake na ndiyo sababu ya mguu huo kwenda upande.
Kisa cha kidonda kudumu miaka minne
Baada ya kuumia, kabla hajaenda hospitali, alipewa huduma ya kwanza ambayo ilikuwa ni kukandwa na maji ya moto na hiyo ndiyo sababu ya mguu wake kuota malengelenge.
Mpaka naruhusiwa kurudi nyumbani malengelenge yalikuwa yameisha isipokuwa kifundo cha mguu (ankle) kilibaki kidonda ambacho mwanzoni kilikuwa kidogo lakini kikawa kinaongezeka ndipo nilipoamua kurudi Muhimbili.
Alipofika hospital madaktari walimkagua na kumwambia kuwa kidonda chake ni kikubwa hivyo watamfanyia upandikizaji wa ngozi ya mwili wake katika kidonda (skin grafting) ili kikauke haraka.
Nilikatwa nyama za paja, tazama (anafunua paja lake na kunionyesha makovu makubwa meusi) humu zilimeguliwa na baada ya hapo wakaziambatanisha katika kidonda, lakini cha ajabu kesho yake asubuhi nikapewa ruhusa nirudi nyumbani kabla hata sijajua hatma ya kidonda hicho.
Anaamini kuwa si haki hata kidogo kwa mgonjwa aliyefanyiwa upandikizi wa ngozi katika kidonda kuruhusiwa kurudi nyumbani katika kipindi kifupi na hiyo anadhani kuwa huenda ndiyo sababu ya kuoza akijiona.
Wakaniruhusu wakisema nirudi baada ya wiki moja, lakini kidonda kilikuwa kikitoa harufu na ukungu wa kijani ukionekana kwa juu. Hata hivyo, baada ya kipindi hicho nikaenda na nikaambiwa madaktari hawapo, sikuwa na jinsi nikarejea nyumbani.
Alikwenda tena hospitali kujaribu bahati yake lakini aliambiwa madaktari wametingwa kwani kuna wagonjwa wengi wanaofanyiwa upasuaji hivyo arudi baada ya wiki. Kuona hivyo, akafanya juhudi hadi akaonana na daktari mmoja na kumuonyesha mguu wake. Akamfanyia usafi.
Baada ya hapo nikawa napangiwa tarehe za kurudi nafanyiwa usafi lakini kidonda hakiponi na huu ni mwaka wa nne sasa niko katika hali hii. Kidonda kinazidi kuchimbika, maumivu na harufu kali vinanikosesha raha. Inzi ndiyo rafiki zangu.
Kwa mujibu wa maelezo ya Penina, hata kuoza kwa mguu huo kumesababishwa na madaktari kwani akiwa Kibaha aliambiwa kuwa alipewa masharti potofu baada ya kufanyiwa upandikizi huo wa ngozi na ndiyo maana kidonda hicho hakiponi kwani damu ilikuwa haitembei vizuri.
Hata hivyo, daktari mmoja anayefahamu historia ya ugonjwa wa Penina anasema kidonda chake na pamoja na ulemavu alioupata yawezekana umetokana na yeye mwenyewe kukosea masharti kwani kutokana na tatizo lake inaelekea alikuwa anauweka mguu chini hivyo damu ikawa haitembei.
Lakini Penina anasema ameambiwa atoe Sh300,000 ili arekebishwe mguu na kutibiwa kidonda upya lakini mpaka sasa ndugu zake wamemsusa hawampi msaada wowote hivyo amekata tamaa na anachosubiri ni kudra Mungu.
0657 118585