Hii ni kali sasa kwa elimu ya tanzania.....

Mboko

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
1,095
293
Wadau nimesoma kwa news flani hivi ati mtihani wa darasa la saba hapo kesho ni kuchagua kweli au sikweli kwa maswali yote pia kwa kuchagua A B C D kwa masomo yote mpaka hisabati Lol!! kweli serikali hii imechoka kila siku inauwa tu Elimu ya Bongo aibu sana tu.Sasa kuna watoto wengine wanaweza kufaulu kwa kuchagua tu hata kitu hakielewi na mwisho wa siku mtu kafaulu kizali Duuh hii kali sana.Hapa hatutapata wasomi kabisa 100% ni zero walioasisi mfumo huu ni VILAZA wakutupwa hivi wao walifanya mitihani hivi jamani kwa nini waamue kufanya hivyo.Hebu wadau wapenda nchi hii tujaribu kufahamishana na kuelewanishana about this issue
 
hata kama mtihani huu utasimamiwa na Mungu mwenyewe, ikiwa ni kuchagua TRUE or FALSE, YES or NO A,B,C or D ni msiba tu.
 
wanavyo sema form one hajui kusoma wala kuandika ndo haya sasa
 
si tunataka kusahisha kwa kômpyuta ili twende na wakati!!? majibu yakiwa subjective kompyuta itashindwa kufanya kazi ya kusahisha, Kimsingi tumetunga mtihani kwa mtindo hùu ili kuirahisishia kazi kompyuta na sio kuwapima hao watoto, Afterall wataenda tu sekondari hata kama hawajui kusoma wala kuandika!
 
Kati ya vitu ambavyo viliniudhi ni nikavishangaa katika hii elimu ya tanzania ni pale niliposikia kuwa hata mtihani wa hisabati unafanywa kwa kuchagua herufi.. Yaani hapa ndo wanazidi kukiua hiki kizazi kwa sababu hakuna maana ya hesabu zaidi ya kubahatisha na hata wanafunzi hawa wakifikia elimu za juu(sekondari na kuendelea) ufaulu wao katika somo hili utakuwa mbovu kwa kutokuwa na msingi mzuri huku walikotoka.
 
ni tatizo sana kama masomo kama hisabati yatawekewa majibu ya kuchagua...
ila ni mbinu ya kuficha udhaifu katika mifumo ya elimu
 
Back
Top Bottom