Hii ni kali: Mwanamke ajioa mwenyewe

WILSON MWIJAGE

JF-Expert Member
May 30, 2011
276
76
Wana JF,

Heri ya mwaka mpya 2012.

Wakristo wanaamini katika ndoa ya mke mmoja mme mmoja. Waislam wanaamini katika ndoa ya wake wengi yaani mme mmoja wake wengi (wasiozidi wanne), hizi zote ni ndoa za mme na mke au mme na wake. Baada ya umagharibi kushamili tunasikia ndoa za jinsia moja zinapigiwa chapuo (mwanamme kwa mwanamme AU mwanamke kwa mwanamke)

Sasa hapa kuna kisa cha kufungua mwaka 2012, Mwanamke aitwae Wei-yih Chen (30) ameamua kujioa mwenyewe baada ya kuona misukosuko ya kimapenzi katika jamii. Alialika watu takribani 30 hivi baada ya kulipa fedha ya fungate ya harusi yake na kumwita mchungaji ili amfungishe ndoa baada ya mumweleza kwamba ana umri mkubwa, kazi mzuri lakini hajapata mwamme.

Ndoa hiyo iliyotumia dola za kimarekani 1,500 (sawa na shilingi za kitanzania 2,307,000 'dola kwa leo') ilifana sana hasabaada ya watu wengi duniani kumpongeza, kwa kuwa ni uamuzi ambao unahusu maisha yake. Hii ni ndoa ya aina yake ambayo haijawahi kuwapo duniani.

Nawasilisha:yawn:

Chanzo: Tanzania Daima; Jumapili Januari 8, 2012 uk:18
 
kweli hujafa hujaumbika!! Hivi ndo vituko vya kuwa na hela nyingi kupita matumizi.
 
Magonjwa ya akili yapo ya aina nyingi sana ambayo humpelekea mgonjwa husika kufikia maamuzi fulani ambayo kwa kawaida hua si yakawaida katika jamii.
Lakini kingine pia ni hizi teknolojia za siku haswa viungo bandia vya kike na kiume, hizi ndo zimeharibu kabisa maadili kabisa,
hapo kafunga ndoa pekeake lakini nadhani ukienda rum kwake utaweza kuta utitiri wa misanamu ya viungo vya kiume.
USHAURI;-
Ni vema apatiwe mtaalamu wa matatizo ya kisaikolojia na matatizo yake yataisha.
 
Yale maswali ya mchungaji ya upande wa pili yalijibiwa na nani!!!!
 
Ukistaajabu ya musa utaona ya firauni, na ndoa alifungishwa na kiongozi wa dini au?
 
Wana JF,

Heri ya mwaka mpya 2012.

Wakristo wanaamini katika ndoa ya mke mmoja mme mmoja. Waislam wanaamini katika ndoa ya wake wengi yaani mme mmoja wake wengi (wasiozidi wanne), hizi zote ni ndoa za mme na mke au mme na wake. Baada ya umagharibi kushamili tunasikia ndoa za jinsia moja zinapigiwa chapuo (mwanamme kwa mwanamme AU mwanamke kwa mwanamke)

Sasa hapa kuna kisa cha kufungua mwaka 2012, Mwanamke aitwae Wei-yih Chen (30) ameamua kujioa mwenyewe baada ya kuona misukosuko ya kimapenzi katika jamii. Alialika watu takribani 30 hivi baada ya kulipa fedha ya fungate ya harusi yake na kumwita mchungaji ili amfungishe ndoa baada ya mumweleza kwamba ana umri mkubwa, kazi mzuri lakini hajapata mwamme.

Ndoa hiyo iliyotumia dola za kimarekani 1,500 (sawa na shilingi za kitanzania 2,307,000 'dola kwa leo') ilifana sana hasabaada ya watu wengi duniani kumpongeza, kwa kuwa ni uamuzi ambao unahusu maisha yake. Hii ni ndoa ya aina yake ambayo haijawahi kuwapo duniani.

Nawasilisha:yawn:

Chanzo: Tanzania Daima; Jumapili Januari 8, 2012 uk:18

kwahapa home tz itatambuwa ni ndoa ya aina gani?kimila,dini au!
 
Wooow!! kwahiyo hatakuwa na worries zakuwa-cheated bali ataji-cheat mwenyewe....asipoji-satisfy ataji-stress mwenyewe hana wakumlaumu..kitanda cha futi 3 kwa 6 kitamtosha (atabana matumizi)...saaafi sana!! Ila sio mfano wa kuigwa...
 
sasa hii inahusu nini jukwa hili?

Kwanini waandishi wa awali waliichapisha mwenye mitandao mingine na kwenye gazeti? Kwanini mwengine kwenye JF wanaichangia?Kwa maana nyingine sikuelewa msingi wa swali lako uko wapi

Mwisho wa kujibu hoja hii:juggle:
 
Sidhani kana hiyo ni ndoa hasa, maana kama ni ndoa, basi vijana wengi ambao wako single (pengine hata hao wenye ndoa) watakuwa wamejioa wenyewe, kama kujioa mwenyewe ni suala linalowezekana!

Huyu mama nadhani alikuwa anatafuta umaarufu ili attract attention za watu kwa lengo la kujipatia umaarufu ....
Ni viumbe wachache sana ambao huishi bila kuwa na mahusiano ya jinsia tofauti ambao hutumia binary fission (which is a form of asexual reproduction) kujiongeza, lakini kwa binadamu mhhh, haiwezekani.:poa
 
Ukistaajabu ya musa utaona ya firauni, na ndoa alifungishwa na kiongozi wa dini au?

Kwa mujibu wa mwandishi hakuweza kueleza ni kiongozi gani wa dini alifungisha hiyo ndoa zaidi ya kuandika ".......... inadaiwa alimuita mchungaji wa dini ya kwao, akafungisha ndoa ..........."
 
Ofcoz binadamu tukisema mf.
Lile ni Darasa.
It'means inakua walimu & wanafunzi wamehusishwa.
Lile ni Shamba.
Maana yake kuna ardhi na Mazao.
Na tusemapo ile ni Ndoa basi lazima Mwanamke & Mwanaume wahusike.
Tofauti na hivyo hapo Ndoa haipo, ni mahoka flani tu.
 
Hizo ni dalili za wanawake wameisha kuwa wengi na wanaume wachache, itabidi tu watake wasitake wakubali kuwa 2nd wife, 3rd wife and 4th wife.

Mungu taratibu ananza kuonyesha dalili.

Na baod kabla ya jua kutokeza magharibi na kuzamia mashariki wanawake 70 watataka kuolewa na mwanaume mmoja.

Tuomba uzima mana siku zimekaribia.
 
Back
Top Bottom