Jiwe Linaloishi
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 3,736
- 2,137
bado cjaona cha kunishangazab hapo
Makengeza mko wengi.... siku ukiumwa wakakupeleka huko ndio utaona vya kukushangaza...
bado cjaona cha kunishangazab hapo
tupitishe sheria rais, makamu wa rais na waziri mkuu peke yake ndio watatibiwa njee kwa garama ya serikali iwapo watakuwa na tatizo kubwa wengine tubanane huko muhimbili ama sivyo ujigaramie mwenyewe kwenda apolo tuone kama muhimbili haitawezeshwa.Mnafikiri ni sababu gani zitakazowafanya viongozi wetu waikumbuke Muhimbili wakati wao wanatibiwa India?
Kumbe gloves zipo?Mkuu hayo ya kawaida huku mikoani ndo usiseme, hakuna karatasi mgonjwa anaandikiwa kwenye karatasi la gloves na inawekwa kwenye file... Maisha yanaendelea!
Kinachoifanya Tanzania iendelee kuwa na umasikini na kukosa ufanisi ni tabia ya kukosa maadili kwa watanzania. Kwa mfano kiongozi badala ya kufuata maadili ya kutumikia wananchi anachukua pesa kwa manufaa yake binafsi. Mfano mwingine wa kukosa maadili ni pale daktari au mtumishi wa afya anapopiga picha nyaraka binafsi za wagonjwa zenye majina yao na namba za mafaili yao na kuziweka kwenye vyombo vya habari. anakiuka patient confidentiality!
Tukitambua kuwa maadili yanaanza kwa kila mmoja wetu tutafika, iwapo tutaendelea kulilia wengine wawe na maadili ilhali sisi hatuna maadili tutakuwa tunajidanganya tu.
mkuu doctor-patient confidentiality ni kuhusu ugonjwa ila suala la nani kalazwa hospitali sivyo, kutaja usiri ya UGONJWA ni kukiuka maadili kweli lakini not just names.
Absolutely, nakubaliana na hoja yako. Ulimbukeni wa kujua kupost vitu kwenye mtandao utawaponza wabongo.Si sahihi kusema tarehe ya mtu ya kuzaliwa, kusema kuwa siku fulani afya yake ilikuwa na mgogoro, kusema kuwa Dr. Fulani alimtibia. Taarifa hizo ni mali ya mgonjwa na kuziweka kwenye vyombo vya habari ni ukiukwaji wa maadili. Hawa mnaoweka majina yao hapa ni watu wa Kama kuna chuo kinafundisha kuwa kukiuka maadili ni kutaja ugonjwa tu basi wanafundisha uongo.
Chukua mfano mtu ana ugonjwa wake ambao ameamua kuufanya siri na tarehe husika aliaga nyumbani anaenda kumtembelea rafiki ili aende hospitali, halafu the following week file lake linawekwa kwenye media, huoni kuwa kitendo hicho kitamkwaza mgonjwa na kusababisha kuogopa kuhudhuria hospitali next time? Tabia hii inawafanya wagonjwa wakose uhuru wa kueleza matatizo yao hospitalini.
Mkuu Measkron, yaani hata continuation sheets hazipo, imagine NGT(Nasogastric tube) na gloves(clean gloves and not sterile) ndio zinatumika kufungia karatasi za wagonjwa??? zikipotea nani alaumiwe? vifaa navyo vikipotea-kama feeding tubes(NGT) zinatumika??Sijui tunaelekea wapi, kama hii ndio Hospitali ya TAIFA!!!!