Hii ni bodi ya mikopo au ya makopo?

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
695
12
Nashindwa kuelewa nchi inaelekea wapi, jana tbc1 waliwaonyesha wanavyuo wakiwa bodi ya mikopo wakifuatilia hela za ada,matumizi na za field.hivi mpaka wanavyuo waende bodi wenyewe au mawasiliano kati ya bodi na vyuo hayapo? Nilidhani mambo haya yataisha muda ule tulipokuwa tunapewa 100% baada ya sasa kubadilika kwa mfumo wa utoaji mikopo kwa mafungu lakini ndo badooo,je bodi au serikali mmeshindwa kukopesha wanafunzi hata kwa hizo percent ndogo mlizoweka? Je mkapa alitoa wapi hela za kuwakopesha wanavyuo asilimia mia?.

AU NDIO HIZO SAFARI ZA NJE ZA JK AU MATUMIZI MAKUBWA YA SIRIKALI HII KAMA SEMINA, MASAFARI YA MAWAZIRI MIKOANI NA KUNUNULIA MAVX V8 YA SERIKALI ZIMEKAUSHA HAZINA?

Napata kichefuchefu na nchi hii.mimi nakatwa hela kurudisha mkopo niliochukua bodi wakati nasoma naamini na wengine wanakatwa vilevile, je hizo hela zinaenda wapiiii?


Nashauri: bodi isivunjwe ila mabadiliko makubwa ya uongozi yafanyike na serikali wawe serious na kuhakikisha hela zinakuwepo pale bodi ili wanavyuo wasipoteze muda badala ya kusoma kuja dar toka ar au mby kufuatilia hela.

Wananchi: wakati wa mabadiliko ni sasa, hawa viongozi wetu hawana uchungu na wataalamu wa kizazi kijacho, angalia sasa wanavyuo wanafikia hatua ya kufanya ukahaba ili waishi, hii inatisha sana.

MKEREKETWA. :mad2:
 
Ikiwa unashauri isivunjwe unacholalamika ni nini?

Kuivunja bodi sio suluhisho, hii bodi bado ni msaada kwa wanavyuo wengi ambao ni watoto wa walala hoi, maboresho ya uongozi na kuwepo hela za kutosha pale bodi ndio suluhisho tu.Kutoa milalamiko yetu ni jambo zuri ili kuelezea serikali ni jinsi gani hii bodi inaadhili wanavyuo kwa utendaji wake mbovu aidha kutokana na uongozi mbovu wa bodi au kutowekewa hela na hazina.
 
Back
Top Bottom