TUKUTUKU
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 11,765
- 4,033
Kwa sababu ya kuuelewa umuhimu wa elimu, Uislamu umehimiza Waislamu kuitafuta na kujifunza elimu. Mfumo wa maisha ya Muislamu umetawaliwa na sheria maalum ambapo ili mtu aishi kama Muislamu wa kweli inambidi awe na elimu. Elimu huanza tangu utoto. Ni utaratibu uliopo tangu kutangaza kwa Uislamu kwa watoto wa Kiislamu kupelekwa katika madrasa kusoma elimu. Hapo zamani wazazi walikuwa wakichukua jukumu la kuwasomesha wenyewe watoto wao ambapo kwa siku hizi hutegemea zaidi madrasa. Kwa sababu hii miji yenye Waislamu wengi madrasa za watoto huonekana katika kila kona ya mji.
Vipi elimu dunia haina umuhimu katika maisha ya jumuiya ya kiislamu?