Hii ndoto inatisha- nisaidieni

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Usiku wa kuamkia leo kwa kweli nimeota vibaya sana.

Nilijikuta nadondoka kwenye mnazi mkubwa uliolala kwenye bonde kubwa. wakati niko katikati angani nikiwa napiga mayowe nikaona kinakuja kitu chenye ncha kali, wakati kinakaribia kunigusa hafla nikajikuta nimeaota mbawa na kuruka juu zaidi na kufanikiwa kukikwepa hicho kitu mfano wa mshale unaokimbia kwa kasi katika hali ya kujizungusha zungusha. Hali iliyonitisha zaidi niliona naelea angani tu na wala sifiki chini mpaka nilipojilazimisha kupiga zile mbawa kwa mkandamizo kuja chini nikashtuka niko chini yakitanda na tayari nilishamwaga maji yaliyokuwemo kwenye jagi. Nimeduwaa kwa muda kwa kweli.

Hii ndoto imenitisha sana. Naomba mawazo yenu.
 
Ndoto yako inaashiria baada ya kufa utaumbwa upya na kurudishwa duniani kwa umbile la ndege.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom