Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,796
Ni ile ndoa ya ajabu kuwahi kutokea ulimwenguni! Ndoa ya mke mmoja waume wawili....
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulileta maana kipindi cha waasisi wake ambao kwasasa wote ni marehemu Mwalimu JK Nyerere na Mzee Karume , muunganiko wa Tanganyika na Zanzibar ni matokeo ya vita baridi wakati huo
Mahitaji ya wakati yaliufanya muungano huu uanze kupoteza maana kuanzia mwaka 1985 mzee Mwinyi alipoingia madarakani....Ni kuanzia kipindi hicho yalianza kutokea mabadiliko kadhaa kwa upande wa Zanzibar kuelekea nchi kamili huku kitu kinachoitwa 'kero za muungano' kikiongezeka kila wakati
Ili nchi itambulike kuwa nchi inahitaji haya
.mipaka kamili
.katiba
.Bendera
.Sarafu
.Majeshi
.Bunge
.Rais
.wimbo wa taifa
.uongozi wa kisiasa au kijeshi nk
Mabadiliko ya taratibu yaliyofanyika kwa vipindi tofauti ndani ya miaka 30, vimekuja kuirudisha Zanzibar kama nchi kamili na si sehemu ya Mungu ni (siwalaumu)
Kilichopo kwasasa ni muunganiko wa kisiasa tuu kwamba chama kimoja cha siasa kinahudumu katika nchi mbili tofauti (hilo laweza kuwa ajabu mojawapo la dunia sawa na mke mmoja kuolewa na waume wawili)
Kumekuwa na utamaduni ndani ya ccm rais kuwa mwenyekiti wa chama pia...hili limefanyika kwa kipindi chote cha utawala wa ccm
Jana ilikuwa pia kukamilisha utaratibu huo wa kumkabidhi Magufuli uongozi wa chama...tunajua mengi yalifutikwa chini ya zulia ili mchakato uende salama japo kuna nyuso zilionyesha waziwazi kuwa hazikuridhika kabisa (ushahidi wa hotuba yake ulidhihiri hilo)
Magufuli ni mtendaji si mwanasiasa, Magufuli hana uvumilivu na hili kakari mwenyewe, mtu ambaye hana uvumilivu hana tafakuri hana diplomasia...siasa zinataka hivyo vitu...Muungano umedumu kwasababu ya uvumilivu tafakuri diplomasia na unafiki kwa upande mwingine
Je chini ya Magufuli muungano huu utadumu? Muda utaamua