Hii ndo TZ ya leo

kafukugm

Member
Oct 10, 2009
11
6
Soma hii habari uone jinsi TZ ya leo ilivyokosa connection between the three pillars of a government that is, Parliament, Judiciary and Civil servant (bunge, mahakama na serikali kuu au utumishi wa umma)

This is real sad to see we are living in a less patriotic country like Tanzania, anyway, one day God will remember us an this generation will pass by. For Tz to lack strong institutions, it's now u find everybody putting blames on others, i can't believe even MPs are complaining, and now who is the govt? May b TZ is only Mr. President and his cabinet.

I see it's time now not to depend on these pple who have bn in power since we were very young n now we r grown up we see them playing d same game, them become rich n we suffer.

Tanzania only needs a strong president who will give strong orders to stop wht is goin on now. Tanzanians are good at recieving orders from top, i believe if Mr. President changes the whole country will change, let him give just a voice n corruption will stop. let him clean his own pple in power without mercy n let him feel sorry for TZ, it's shame we r outside d country n we can't speak proudly about our country.

We need CHANGE.

"Mbunge Ole Sendeka atishia kumharibia Rais Kikwete"

"Ataka serikali iwakamate kwanza nafisadu badala ya kuibua hoja ya 'posho mbili'


Daniel Mjema, Dodoma

SUALA la wabunge kuhojiwa na Takukuru, juzi lilichukua sura mpya baada ya Mbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka kugeuka msumari wa moto kwa serikali akitaka iwakamate kwanza wabunge mafisadi wanaohusika na kashfa za Kagoda na Deep Green Finance kabla ya kuwaandama wabunge.

Katika kashfa hizo, Kampuni ya Kagoda Agriculture inadaiwa kuchota kifisadi Sh40bilioni kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wakati Deep Green Finance inadaiwa kukwapua Sh9 bilioni kutoka kwenye akaunti hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa za kutoka ndani ya kikao cha faragha cha wabunge wa CCM kilichofanyika mjini Dodoma,inaelezwa kuwa Sendeka alihoji kama kweli agizo la kuwahoji wabunge lilitolewa na Ikulu.

Huku akishangiliwa na wabunge wengine, Sendeka aliibana serikali akitaka kujua iwapo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah ametumiwa na mafisadi au kweli katumwa na Rais Jakaya Kikwete kuwadhalilisha wabunge.

Sendeka alitoa kauli hiyo juzi usiku mjini Dodoma katika kikao cha faragha cha wabunge wa CCM kilichofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa chini ya Katibu wa Kamati ya Wabunge wa chama hicho, Ali Ameir na taarifa zake kulifikia gazeti hili.

“Kuna mambo mawili ambayo tunayaona katika suala hili; ama Dk Hoseah anatumiwa na mafisadi au ametumwa na rais kuwadhalilisha wabunge kwa sababu Takukuru siyo taasisi inayojitegemea bali iko chini ya rais,” chanzo chetu kilimkariri Sendeka akisema ndani ya kikao hicho.

Alisema hawaelewi na hawaamini kama rais ndiye ameagiza wabunge wadhalilishwe, lakini kama ndivyo awaeleze ili nao waende majimboni kwa wananchi kuwaeleza mabaya ya serikali wanayoyafahamu.

Huku akipigiwa makofi na wabunge karibu wote waliohudhuria kikao hicho, Ole Sendeka alisema baada ya kuwaeleza wananchi, wao ndio watapima ni nani wasafi kati ya wabunge, serikali na Takukuru.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zimedokeza kuwa Sendeka alitaka Rais Kikwete azungumze na Mkurugenzi wa Takukuru kabla mambo hayajaenda kombo.

Kikao hicho kilikuwa mahususi kwa kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM kutoa taarifa ya ujio wa kamati ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, lakini Ole Sendeka akakitumia kuibua suala la uchunguzi huo wa Takukuru.

“Tunafahamu Hoseah anajua humu ndani wapo wanaohusika na kashfa za Kagoda, Meremeta na Deep Green Finance awakamate kwanza, tuone kama kweli anakerwa kwa dhati na tatizo la rushwa,”alikaririwa Ole Sendeka.

Mbunge huyo machachari alisema endapo suala ni malipo ya posho kwa wabunge, iundwe tume huru ya pamoja kuchunguza na uchunguzi huo ufanyike kwa mihimili yote mitatu ya dola kwa maana ya Bunge, Mahakama na Serikali.

Chanzo hicho cha habari kimedokeza kuwa Ole Sendeka alisema endapo uchunguzi huo utabaini wabunge wamekula fedha haramu, wako tayari kuzirejesha lakini, akasema nao watatumia nguvu ya umma kupasua mabomu ya serikali.

Alidai kuwa hata yeye Hoseah na taasisi yake (Takukuru) ilipokuwa inataka Bunge lipitishe muswada wa marekebisho ya Sheria ya Rushwa, aliandaa semina kwa wabunge na kuwalipa posho kama ilivyo kwa taasisi nyingine.

Ole Sendeka alimtaka Dk Hoseah kama ana hoja ya msingi katika uchunguzi wake asubiri kwanza Bunge limalizane na suala la Richmond wiki ijayo, ndio waendelee na uchunguzi wao.

“Baada ya uchunguzi wao watupigie mahesabu kama kuna fedha haramu tumekula, tupo tayari kuzirejesha lakini uchunguzi huo uendelee pia kwa mihimili mingine ya dola ambayo ni serikali na mahakama," alikaririwa Sendeka.

Katika kikao hicho Ole Sendeka alihoji ni mkuu wa mkoa gani au waziri anayesafiri kwenda wilayani au mikoani ambaye hata kama amelipwa posho stahiki, husafiri na chakula chake bila kukirimiwa na halmashauri anakokwenda.

Habari kutoka katika kikao hicho, zimezidi kueleza kuwa Ole Sendeka aliitaka serikali kuwasiliana na Spika wa Bunge au katibu wake ili kupata ufafanuzi wa posho hizo vinginevyo iwaite wabunge wote na kuwahoji.

Wakati mvutano huo ukiendelea, zipo taarifa kuwa Takukuru imekuwa ikijiandaa kuwakamata baadhi ya wabunge siku moja au siku ya mjadala wa Richmond ikiwa ni mbinu ya kudhoofisha mjadala huo.

Habari zilizowakariri baadhi ya wabunge zinadai kuwa mpango huo umeandaliwa mahususi na wapo wabunge kwa majina ambao wanaandaliwa mpango wa kuwakamata, ila wanasubiri kwa hamu hilo litokee.

Wiki hii, Mbunge wa Kyela, Mwakyembe alinukuliwa na vyombo vya habari akisema hatua hiyo ya Takukuru kutaka kuwahoji wabunge sasa, ina lengo la kuwafunga midomo wasijadili kashfa ya Richmond.

Alhamisi wiki hii, Spika wa Bunge,Samuel Sitta alisema wabunge wataendelea kupokea posho kwa kuwa ni halali na serikali ilileta bajeti zake bungeni na zikapitishwa na kuitaka Takukuru ishughulikie mambo ya msingi.

Msuguano huo kati ya Serikali na Bunge umekuja wakati wiki hii Bunge linatarajiwa kujadili ripoti ya serikali ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge yanayoitaka serikali kutekeleza maazimio yote bila kusitasita.

Miongoni mwa maazimio hayo ya Bunge ni kuwajibishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Hoseah kwa namna alivyoficha ukweli kuhusu Richmond hadi kamati ya Bunge ilipogundua uozo mkubwa.

Kashfa ya Richmond ndiyo iliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu akifuatiwa na mawaziri wengine wawili, Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi ambao waliitumikia Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti wakati wa mchakato wa zabuni iliyoipa ushindi kampuni hiyo.

Pamoja na kujiuzulu huko maazimio ya Bunge yalitaka pia kuwajibishwa kwa aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali, Johnson Mwanyika na katibu mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi ambao wamestaafu kwa mujibu wa sheria.
Wabunge wanataka suala la utekelezaji wa maazimio hayo ya Bunge limalizike katika Bunge hili la 17, lakini hadi jana kulikuwa na usiri mkubwa wa lini ripoti hiyo ya serikali ya wa maazimio hayo itawasilishwa bungeni."

Source: http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15689
 
Back
Top Bottom