Hii ndo mistari ya bongo fleva iliyoandikwa na mwanafunzi wakati akifanya mitihani ya kidato cha 4

haya ndio matunda ya taifa ambalo maadili hayapo ama yapo njiani kutoweka kabisa. taifa ambalo vijana wake wana maadali wanajua pia umuhimu wa kuwajibika na uzalendo heshima na athari ya kutokuwanayo.kama kijana anaandika matusi katika mtihani ina maana hajitambui, hatambui pia thamani yake katika jamii aliyomo na hajali lolote.lakini hajui wajibu wake kama mwana jamii kuwa afanyapo hivi ni kuchafua jina lake shule yake na familia yake.

tujitahidi sana kuwafunza maadili mema vijana wetu kwani athari zake si katika familia tu hata kwa taifa zima.
mfano mzuri ni shule za seminari ambazo vijana wanafundishwa maadili na heshima hata wakiwa hawapo shuleni utawapenda jinsi wanavyobehave. lipo jambo la kufanyika kwa vijana bado.
 
So scary! Nitashukuru nikifa kabla kizazi hiki hakijaingia maofisini na mataani na kutoa maamuzi ya kitaifa, hakika patatisha kuliko haya magamba ya sasa.
 
This is just sad; it is not even funny. Nilimsikiliza huyo nama nikajua tuna tatizo kuvwa zaidi.

Madawati hamna, maabara hamna, Walimu hamna, vitabu hamna, stationary hamna, wakaguzi hamna ! Sasa ? ................. Bora kushusha mistari kama Ngwear !
 
Ndugu Zangu Watanzania;

Si jambo geni hili, labda huenda mwaka huu limeongezeka ndio maana wameamua kuliweka wazi, au kutokana na matusi yamewashitua.

:photo::photo: Ninayoipata hapa ni kwamba tatizo hili limetokana na Kuvuja kwa Mitihani,

Hao Baraza wakichunguza vizuri watakuta kuwa hiyo mitihani yenye majibu ya utumbo ni lazima ilikuwa imevuja. Sasa MWanafunzi alipata paper na akalitafutia majibu kabla ya kufika chumba cha mtihani. Akiwa anajiaminisha MIA KWA MIA kufanya vizuri, anafika ndani ya chumba kufunua karatasi anakuta SIYO PAPER ALIYOIONA KABLA!!!!!!! :lol::lol::lol:

Ndipo hapo mtu anakosa jibu na anachanganyikiwa na kufikia kufanya mambo kama hayo.

Katika hili pande zote ni za kulaumiwa (1) Wanafunzi (2) wazazi (3) Walimu (4) Baraza la Mitihani

Wazazi tunachangia kiasi kikubwa kwani tunashiriki katika kuwapa pesa ili wanunue mitihani. Ili tu mtoto afaulu na kujiona ni sifa mtaani. kumbe tunamjengea msingi mbovu na matokeo yake ni haya.

Wanafunzi wanachangia kwa uvivu wa kutojibidisha kimasomo kwa kutegemea kununua mitihani.

Waalimu wanashiriki kiasi kikubwa, kwani kuna baadhi ya shule Walimu wanawatafutia mitihani ili watotot wafaulu wengi na shule ipate sifa kwa kupata alama za juu kitaifa, kumbe tunawaharibu watoto badala ya kuwajenga.

Baraza la Mitihani kuna wafanyakazi ambao siyo waaminifu, kwani wao kwa tamaa ya pesa wanatoa mitihani na kuiuuza.

Hivyo hili tatizo tusimlaumu mtoto peke yake kwani kuna Chain ndefu iliyoshiriki katika hili. Mtoto amefika na kukuta mtihani siyo aliotegemea, Je, tunafikiri atajibu kitu gani na ikiwa alitegemea shwali la kwanza ni Multiple Choice kumbe kufika pale anakuta hakuna Multiple Choice kuna ESSAY tupu mwanzo mwisho.

Kwa nini asiandike matusi yaani kumtukana aliyebadilisha mtihani!!!!!!!

Sote tujirekebishe katika nafasi zetu tulivyoshiriki kumfanya mtoto aandike utumbo huu.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
MAJITA wake wapo level za juu yani DAVOZ, N/YORK, W/DC, ANKRA......nk yanini asumbue kichwa majita wapo na wengine wapo KIKOSI CHA MIZINGA yan full majita
 
Mhh...This is shame to our education ministries. Halafu tunajivunia kuongeza udahili wakati hakuna kufundisha!!
 
wachukuliwe hatua za kisheria na vyombo husika! maana wazazi wao hawajawatuma wakafanye UPUUZI KAMA HUU! Mungu ibariki TZ, Mungu wabariki VIJANA WETU!
 
Mi naona ingekuwa vizuri majina yao yangewekwa hadharani...
 
ilifaa atajwe kabisa kwa jina na shule anayotokea, ili iwe ni fundisho kwa watoto wasio penda kusoma
 
Kata at work


Mkuu, tukubali tukatae, shule za kata ni janga la Taifa. Nimecheki shule za kata kutoka kwenye wilaya yangu, waliofaulu kwa kiwango cha juu wameanzia division three. Wengi wamefeli! Cha ajabu, shule nyingine katika wilaya hiyo hiyo ( za dini na zile za serikali proper) zimefanya vizuri. Nawasikitikia sana hawa vijana wanaopangiwa shule za kata. Wanapotezewa muda!!
 
Elimu itaboreka wote kwa pamoja tutatafakari na kujipanga upya. Wazazi wanachangia sana kudidimia kwa elimu ya watoto wao. Mtoto anafanyiwa 'birthday', anapewa zawadi ya kinanda cha kupuliza, baiskeli au mdoli wa cellular phone badala ya kitabu au daftari ni mwanzo mbaya kwa safari ya kielimu ya mtoto huyo. Kinanda kinamwelekeza kwenye u-bongo flavor, baiskeli inmwelekeza kwenye uzururaji, mdoli unamwelekeza kwenye umbeya badala ya kuzingatia masomo
 
Back
Top Bottom