Hii ndiyo Tanzania tunayoitaka

Dr Who,

Kufunga mkanda ni jambo zri sana kwa nchi yetu, unajua even at household level ukitaka kufanya kitu cha maendeleo unajibana au kwa hapa UK unaongeza kazi ya pili au ya tatu. Sasa tatizo linakuja pale ambapo wachache mikanda yao wanalegeza at he expense ya walio wengi through corruption, emblezzement and the like. Na hii imekuwa sehemu ya utamaduni wetu kwa sababu hakuna any deterence, ukiwa mwizi wa pesa ya umma mpaka jamii inakutuza.
 
Ndio hao Watanzania ambao jana walijazana neshno stedium (pengine ashauziwa mtu) kuungana na majambazi wa raslimali zetu kusherehekea birthday ya nchi hii isyojua inakoelekea.[/QUOTE]

Wengine wanatoka Gongolamboto na kutafuta njia za mkato kuelekea National Stadium
 
Watanzania Watu Wa Ajabu Sana

Jana Wamejazana Neshino Stediamu Wakati Wenzao Mwanza Na Shinganya Wanakufa Kwa Mafuriko , Hii Maana Yake Nini Na Wakazi Wa Mwanza Sijui Wamefikiria Nini Kuhusu Sherehe Hizi Kikwete Alikaa Pale Anafuraha Gharama Za Kuandaa Zile Sherehe Zingetosha Na Pengine Kubaki Kama Wangeenda Kuzitumia Katika Kuokoa Na Kujenga Maeneo Yaliyohabirka Mwanza Na Shingaya
 
GAZETI LA MWANANCHI, 11/12/2006

Mtikila aja na mpya

Na Muhibu Said

SIKU moja baada ya Watanzania kuadhimisha miaka 45 ya Uhuru, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ametangaza kuanzisha vyombo vya habari ili kuamsha hisia za utanganyika ili Watanzania bara waweza kuuthamini na kuupigania utaifa wao.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya DP, jijini Dar es Salaam jana.
Mtikila, vyombo hivyo ambavyo ni televisheni, redio na magazeti, vitaanzishwa kupitia Kanisa la Full Salvation, Taasisi ya Liberty International Foundation na chanma chake.


Mbali na kuanzisha vyombo hivyo, Mtikila ametangaza mpango wa kuzunguka nchi nzima na kuvitumia vyombo vya habari kuetekeleza lengo hilo.

Mtikila, alisema hakuna rekodi yoyote duniani inayoonyesha kuwa Desemba 9, mwaka 1961, ulipatikana uhuru wa Tanzania Bara kama inavyoelezwa na baadhi ya watu, badala yake, rekodi zote sahihi zinaonyesha kuwa kilichopatikana siku hizo ni Uhuru wa Tanganyika.

Alisema kufutwa kwa uhuru wa Watanganyika, kuliambatana na kuua hisia na uchungu juu ya utaifa wao, kiasi ambacho nchi yao inapoporwa huishia kuchekelea.
------------------------
KWENU WANABODI, WATOTO WETU WAELIMISHWE VIPI KUHUSU SIKU HII. NA JE HISTORIA SAHIHI INASEMAJE??

Kaiba Wambandwa
 
Wapinzani walilia masilahi ya majaji



na Mwandishi Wetu, Dodoma


KAMBI ya Upinzani bungeni, imetaka rais asipewe madaraka ya kuwa mtu wa kufanya maamuzi ya mwisho kuhusu masilahi ya majaji badala yake kazi hiyo ifanywe na chombo kingine.


Kauli hiyo ilitolewa jana na Mbunge wa Chakechake, Fatma Maghimbi, alipokuwa akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kuhusiana na muswada wa sheria ya marupurupu na mishahara ya majaji.


Badala yake, kambi hiyo ilipendekeza kazi ya kuamua kuhusu mishahara na marupurupu ya majaji, ifanywe na chombo kitakachohusisha majaji, wanasheria na walimu wa vitivo vya sheria kwa kuwa wao ndio wanaofahamu uzito wa kazi hiyo na stahili ya masilahi yake.


Aidha, kambi ya upinzani imeshauri serikali kutokata kodi kutoka posho na mishahara ya majaji kwa kuwa kundi hilo halina chombo cha kupeleka malalamiko yao kwa ajili ya kudai kuboreshwa kwa masilahi zao.


“Tunaishauri serikali wasikate kodi mishahara na posho za majaji, kwani hawana chombo cha kupeleka maombi ya kufanya hivyo…vilevile kufanya hivyo kutaongeza ushawishi wa majaji kupokea rushwa. Nashauri uwepo utaratibu wa kuboresha masilahi yao mara kwa mara,” alisema Maghimbi.


Kambi ya upinzani pia inashauri mhimili wa mahakama upewe uhuru kamili wa kupendekeza na kuboresha masilahi ya majaji katika kumiliki na kuendesha bajeti yake bila kuingiliwa na chombo kingine.


Aidha, Maghimbi alitaka bajeti baina ya mihimili ya dola, igawanywe kwa mujibu wa uwiano wa pato la taifa.


Pamoja na hayo kambi hiyo ilisema sehemu ya muswada huo inayohusu maziko haikuzingatia udini.


Maghimbi, alisema kwa kuwa majaji wa Kiislamu hawazikwi na jeneza kama ilivyoainishwa katika muswada huo, amependekeza kuwa zitolewe fedha kwa ajili ya hitma baada ya maziko ya majaji wa Kiislamu.


Akichangia wakati wa mjadala wa muswada huo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), alisema sheria hiyo imewasahau mahakimu wa ngazi zote.


Alisema kuwa pamoja na kuchelewa kuja kwa muswada huo, lakini upo ulazima wa kutazama tena masilahi ya mahakimu ambao ndio wenye hatari zaidi katika utendaji wao.


Alitoa mfano wa Mkoa wa Dodoma wenye mahakama 23 na kati ya hizo ni tano tu ndizo zenye mahakimu, hivyo serikali inakabiliwa na kazi kubwa ya kuongeza idadi ya mahakimu na kuboresha zaidi masilahi yao.


“Ipo haja ya kuwaongezea masilahi mahakimu… mfano, mishahara ya mahakimu wa mahakama za mwanzo ni kati ya sh 120,000 na 150,000, hakimu huyu anaishi kwenye nyumba ya kupanga, anajisafirisha kwenda kusikiliza kesi sehemu nyingi… lazima masilahi yao yaboreshwe,” alisema Kabwe.


Mbunge wa Kyela, Harrison Mwakyembe (CCM), alisema kuwa kazi kubwa inayofanywa na majaji haijapewa kipaumbele wala kuthaminiwa kwa kuzingatia kuwa kundi hilo ndilo lenye kutekeleza haki kwa jamii.


Alishangazwa na tofauti kubwa ya mishahara kati ya mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na jaji, kwa kusema kuwa huo ni uonevu kwa vile majaji hawana mahali pa kutolea kero zao.


Kabla ya kuwasilisha na kupitishwa kwa muswada huo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Mary Nagu, alisema kutokuwepo kwa utaratibu wa kisheria unaoelekeza masharti na haki za majaji wawapo kazini, safari ama wanapofariki, kuwa ni dosari kwa kuwa inakiuka mgawanyo wa madaraka kati ya Bunge, Serikali na Mahakama.


Alisema dosari hiyo ni sawa na kuingilia uhuru wa mahakama.


“Hadi sasa, Bunge halijawahi kutunga sheria wala serikali haijawahi kuleta bungeni muswada wa sheria kwa madhumuni hayo tangu tupate uhuru…kuandaa muswada huu kumetokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na wizara yangu katika nchi za Jumuiya ya Madola,” alisema Dk. Nagu.


Pia muswada huo umependekeza malipo ya uzeeni kwa majaji, Jaji Mkuu na mjane wa jaji mstaafu. Muswada huo utaanza kufanya kazi Machi mosi mwaka huu iwapo utasainiwa na Rais Jakaya Kikwete.


Baada ya maelezo hayo, wabunge waliridhia na kuupitisha muswada huo pamoja na marekebisho yake.
 
India's reluctant billionaire

By Steve Schifferes
Economics reporter, BBC News, Bangalore


AZIM PREMJI
Born: 24 July 1945
Job: Wipro boss since 1968
Net worth: $11bn
Education: BA, electrical engineering, Stanford
Family: wife (Yasmeen), two sons (Rishad and Tariq)

Wipro chairman Azim Premji wears his crown as India's richest man lightly.

He still drives a Toyota Corolla, flies economy class, and lives on campus at Wipro's headquarters in Bangalore.

But Mr Premji is one of India's most important hi-tech entrepreneurs.

He built his father's vegetable oil company into a $25bn global outsourcing giant which is challenging the likes of IBM and Accenture, and transforming the way many multinationals do business.

In an exclusive interview, Mr Premji said that with wealth came responsibilities - to his employees, to his clients, and above all to society.

With the attention I got on my wealth, I thought I would have become a source of resentment, but it is just the other way around - it just generates that much more ambition in many people
Azim Premji

"At the end of the day there is only x-amount you can consume, frankly, so that itself becomes a limitation," he told the BBC.

"I think that any wealth creates a sense of trusteeship ... it is characteristic of the new generation which has created wealth to have some amount of responsibility for it."

Admired, not envied

Mr Premji believes that his success in business, rather than causing envy, has inspired a new generation in India to become more entrepreneurial.


GLOBALISATION SERIES
A series on India's world class IT outsourcing industry
Friday: Your experiences
In two weeks: Detroit's decline

"With the attention I got on my wealth, I thought I would have become a source of resentment, but it is just the other way around - it just generates that much more ambition in many people," he says.

Many admire men like Mr Premji, or Nandan Nilekani, the boss of Infosys, who has become a millionaire from his share options.

Indians are proud that they are at last joining the ranks of the world's billionaires, with the number of Indians on the Forbes Rich List doubling from 13 to 27 last year.

Many of the new billionaires are also self-made men, like the head of Jet Airways, Naresh Goyal.

Many of India's biggest companies are still family firms, such as Wipro, Tata and Reliance.

And some, like steel magnate Lakshmi Mittal, have become global players and no longer live in India (Mr Premji is the richest Indian businessman who lives in India; Mr Mittal, who doesn't, is wealthier).

Building India's IT industry

Mr Premji played a key role in building up one of India's most successful industries.

India is the most important global location for outsourcing of business services, and Bangalore is the heart of the IT industry.

Mr Premji believes India had two advantages in IT outsourcing: a skilled workforce that was literate in maths; and widespread literacy in English, the global business language.


WIPRO
HQ: Bangalore
Employees: 61,000
Employees abroad: 11,000
Revenues: $2.2bn
Market value: $25bn
Source: Company
employees as of 31.12.06; revenues as of 31.3.06
market value as of 22.1.07

But the industry was only able to develop in the late 1990s when the government liberalised the telecoms sector and the cost of bandwidth dropped dramatically.

"I was basically trying to have a vision. One saw what was happening in manufacturing 25 years ago in terms of globalisation of manufacturing.

"The biggest bet the industry made is that, if can happen to manufacturing, it can happen to services - at least, the type of services that can be remotely delivered," he says.

But for the Indian IT industry to realise its potential, it needed to invest in people.

"I think the most important reason for our success is that very early in our quest into globalisation, we invested in people - and we have done that consistently and particularly in the service business.

"People are the key to success or extraordinary success."

Wipro's values included a refusal to pay bribes, which cost the firm work in the early days.

Western competition

Managing Wipro's explosive growth has been difficult.

For them, India is a back room - for us, India is the front room
Azim Premji

The company now hires 20,000 graduates each year, and faces competition from foreign multinationals also flooding into Bangalore.

As the demand for IT professionals has risen, Wipro has been forced to raise salaries twice in 2006.

However, Mr Premji believes that India is fully capable of increasing its output of college-educated engineers - already the largest in the world, with 400,000 graduates a year - to meet the growing demand.


PREMJI FOUNDATION
Spending: $4m a year
Schools helped: 18,000
Multimedia DVDs: 464 educational games in 18 languages
He says the industry is also training liberal arts college graduates to do the same work.

And he claims that Indian IT professionals prefer to work for Indian companies rather than foreign multinationals, because their career prospects are better.

"Today we hire more people from IBM and Accenture in India than we lose to them - because they've also realised that they are in India for a certain price advantage and they cannot afford to pay silly salaries because they dilute their price advantage.

"For them, India is a back room - for us, India is the front room," he says.

Reverse outsourcing

But Mr Premji believes that in the long run, the answer to the skills squeeze in India is for Wipro to do more work abroad.

Wipro already employs 11,000 professionals overseas and expects 20% of its business to be offshored from India in the medium term.


INDIA'S TOP BILLIONAIRES
Lakshmi Mittal (steel)*
Azim Premji (IT software)
Ambani brothers (oil, telecoms)
Kushal Pal Singh (construction)
Sunil Mittal (telecoms)
Source: Forbes
*not resident in India

He is planning further expansion in Europe, Japan and the Middle East.

"Indian service companies typically in software services will lead to globalise more - they'll need to localise more," he told the BBC.

"They'll need to localise more because of community reasons - community pressures will build up, visa pressures will build up and in a way, understandably so."

Mr Premji is well aware that in many Western countries, there is a growing backlash against the outsourcing industry, as many skilled professionals fear they will lose their jobs.

I would take China as serious competition for anything in the world
Azim Premji

But he says that globalisation has to be a two-way street.

"If you want emerging countries such as India - which is going to be one of your major markets - to open its borders to global competition and global access for products and services, the quid pro quo is that you have to play fair as a developed nation.

"The Western world loves liberalisation, provided it doesn't affect them. But that's the case with all countries all over the world - liberalisation is a great word if it doesn't affect you."

Many UK companies, however, complain that the UK is far more open to inward investment than India, which is still in the process of relaxing its tough controls on foreign ownership.

The China factor

Like businessmen all over the world, Mr Premji fears one country above all others - China.

Wipro already has set up operations in China, which has one of the world's largest software industries.

At the moment, most of that IT effort goes into manufacturing design, not outsourcing.

But Mr Premji believes that once China has trained enough people to speak English, it will be a real competitive threat to his business.

"I would take China as serious competition for anything in the world. I think Western nations are realising that too late," he said.

Mr Premji believes that the most important thing India can do to maintain its global competitiveness is to improve its education system, which he says is failing women.

He has set up the Premji Foundation to fund projects in 18,000 schools across India, which aim to encourage students to develop computer skills.

And his hope is that, as more girls stay on and finish school, the birth rate will drop to the same level as China.

Improved education and a lower birth rate, he argues, would give India a chance to find enough jobs for the tens of millions of young people coming to the labour market each year.
Gonga hapa chini kwa habari zaidi

http://news.bbc.co.uk/1/hi/business/6312195.stm


India's economy 'nears $1 trillion'

By Andrew Walker
Economics correspondent, BBC News

If we needed a reminder of India's growing global economic presence, we had it last week in the steel industry when India's Tata won a stock market auction for the European company Corus.

The result of putting the two together will be the fifth-biggest steel producer in the world.

And it is an Indian-born entrepreneur, Lakshmi Mittal, who is the driving force behind the biggest of all in the industry, Arcelor Mittal.

That story is merely a recent news event that highlights India's rise. It is a much wider phenomenon.

Gerard Walsh, Regional Director for Asia at the Economist Intelligence Unit in London, says India is already close to being a $1 trillion economy.

And if you measure it using purchasing-power parities - an alternative to exchange rates which accounts for different price levels between countries - India is already the third-largest economy in the world, behind only the US and China.

Growing impact

Most economists expect India's recent relatively rapid growth - an annual average of about 7% over the last four years - to continue.

That alone would ensure the country would make a growing mark. But it has been a relatively closed economy, with barriers to foreign trade and investment.

Those barriers have been eased, but many remain. The government appears inclined to continue the liberalisation process - and that would make India's international integration proceed even more quickly.

The World Bank has done a recent study, called Dancing with Giants, looking at the implications of the rise of India and China.

Alan Winters, one of the authors, says that for the most part, India's rise is good news for the rest of us.

India's economic growth generates more of the goods it produces and others buy - and that will tend to push prices down.

Competition

But there may be some adverse consequences. Demand for raw materials from growing Indian industry will create upward pressure on those prices.

That's also true for oil, although Mr Winters emphasises that India is a small part of what will determine the global energy prices.

In addition, the increased competition as India produces more goods and services might hurt other countries in South Asia, especially in the textiles and clothing business.

That is an industry where low costs are one of the keys to success.

The same is true of another sector where India is already a big presence on the world stage - medicines.

India's biggest is Ranbaxy, a name we will probably hear more of in the future.

The company's chief executive, Malvinder Mohan Singh, says that 80% of revenue comes from international markets and just 20% from India.

It divides half and half between developed- and developing-country markets.

More sophisticated

Ranbaxy is a company that makes so-called generic medicines, cheap copies of drugs developed by others. But Mr Singh says they have ambitions to develop their own patented therapies.

It would be a move into an area that requires more high-level expertise, and that is a characteristic of other areas of India business life - notably computer software.

The low-cost, high-volume manufacturing will continue - at Ranbaxy and in other Indian industries - but a more sophisticated side is emerging.

Nonetheless, there is much in India that remains pretty basic. Poverty is deep and widespread. It is a matter of controversy whether India's economic growth has helped or not.

Some, including Indu Prakash Singh of Actionaid in Delhi, say the rich and middle classes have benefited, but the poor have not.

He says there have been many cases of poor people being displaced from urban areas in the name of development to areas where they have no housing and no livelihood.

The World Bank's Mr Winters agrees that the wealthy and middle-class clearly have gained.

But he also says the data suggests that the distribution of income hasn't changed much, so the poor are benefiting from India's economic growth. He says there is no reason why they should not continue to do so.

Gonga hapa chini kwa habari zaidi

http://news.bbc.co.uk/1/hi/business/6334305.stm
 
Tanzania ni nchi ya kijamaa iliyochanganyikiwa baada ya kuonja utamu na urojo wa mfumo wa kipebari!
 
Tanzania haina wafalme! Mwinyi, Mkapa Wahojiwe
Na. M. M. Mwanakijiji

Nilipokuwa mtoto mdogo, nilikuwa na tabia ya kufanya mambo au kusema vitu fulani ilhali nikijua ya kuwa mambo au maneno hayo yanaweza kuniletea matatizo. Pamoja na kujua huku, sikusita kufanya mambo hayo kwa sababu nilijua pia ya kuwa kaka yangu mkubwa atakuja kunitetea na kunitoa kwenye visongombingo hivyo. Tabia hii ya kitoto, ilinifanya nisijali nimemuudhi nani, nimemtukana nani, au nimemtendea vibaya nani, kwani iwaye yeyote yule, mbele ya kaka yangu mkubwa nilijua ya kuwa hakuweza kufua dafu. Watu walikuwa na kila sababu ya kumhofia kaka yangu kwani alikuwa ni jitu la miraba minne, mtaani alijulikana sana kwa jina la utani la “njemba”. Nilipoingia matatani na watu wakatishia kuniadhibu au kunikwida shati wakihoji matendo yangu sikuchelewa kuwaambia “nitamwambia kaka”. Mara nyingi niliponea chupuchupu kupata kibano mara tu baada ya kutaja jina la “kaka” mkubwa kwani hakuna mtu ambaye angependa kakaangu amkung’ute na kumpiga roba ya nguvu.

Kama wengi mnaweza kukumbuka kitu kama hicho, mtakumbuka kuwa wale wakubwa waliokuwa wakitukingia vifua na kututetea waliogopwa mitaani, na kwa kweli kutokana na tabia hiyo ya kututetea walitudekeza sisi wadogo zao. Ni kwa sababu hiyo hatukuogopa matokeo ya vitendo na maneno yetu kwani “Kaka” mkubwa alikuwa tayari kutusimamia na kutukingia kifua. Ni kwa sababu hiyo basi hatukuchelewa kutamba na kujigamba kwamba mtaa mzima hata walalamike vipi hakuna wa kutubabaisha. Kwa kiburi huku tukibinua midomo yetu tuliwaacha waseme kwani hata wangesema vipi sisi tuliwahakikishia kuwa hatukutishika wala kubabaishwa.

Kashfa ya ununuzi wa rada inayoendelea hivi sasa inaanza kutuonesha ni kina nani katika Tanzania wanaofikiri ya kuwa wao ni watoto waliodekezwa wakadeka, kwa sababu wanajua wanaye kaka mkubwa kuwakingia kifua huko Ikulu. Hivi karibuni rais mstaafu Bw. Benjamin Mkapa akizungumza huko Kisarawe alitamba ya kuwa hababaishwi wala kukoseshwa usingizi na maneno ya Watanzania ambao wanataka azungumzie kuhusika kwake katika ununuzi wa rada ya shilingi zaidi ya Bilioni 40 chini ya utawala wake. Baadhi ya Watanzania wameendelea kuuliza ilikuwaje Tanzania inunue rada hiyo kwa gharama kubwa na namna hiyo na isiyokidhi mahitaji ya jumla ya ulinzi na usalama wa anga letu. Katika kuuliza maswali hayo baadhi ya Watanzania wametaka Rais Mkapa aeleze kinaganaga ni jinsi gani alishindwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wetu kusimamisha ununuzi huo na hivyo kuokoa fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika katika mambo mengine.

Wakati sauti za Watanzania zikianza kupaa angani na kusikika Rais Kikwete akiwa huko Sweden alijitokeza hadharani na kutaka watu wamuache Rais Mkapa apumzike na hivyo asiulizwe kuhusu suala hili la rada. Katika nchi ambapo maneno ya mfalme ni amri na matamanio ya mwana wa mfalme ni sheria basi maneno ya Rais Kikwete yangetosha kabisa kuwanyamazisha Watanzania na kuwafanya wale wote wanaotaka Mkapa azungumzie suala la rada wafunge midomo na kukaa kimya huku wakijikunyata kama waliomwagiwa maji ya barafu. Tunamshukuru Mungu nchi yetu ni ya Jamhuri na hatuna mfalme, malkia, mwana au binti wa kifalme! Sisi tote ni raia wa jamhuri hii na sheria zinatubana sote sawa wakiwamo marais wastaafu na wale wanaodhani kuwa kutokana na nafasi walizowahi kushika basi wana ‘kaupendeleo’ ka aina fulani mbele ya sheria.Katika Tanzania hii ukweli utasemwa kwa watawala bila kuogopa kama wanakasirika au wanachukizwa.

Ukweli ni kuwa hakuna sababu ya msingi ya maneno ya Rais Kikwete ya kutaka Mkapa aachwe apumzike na asiulizwe kuhusu suala la rada kutiliwa maanani na kuzingatiwa. Maneno hayo hayana mantiki, yamekosa uzito, na ni ya kibabe; na hayana msingi wa utawala bora na wala wa kisheria. Ni maneno ya kaka mkubwa. Tunayakataa, tunayapinga, na tunayalaani kwani lengo lake ni kunyamazisha sauti za Watanzania (kwa kuwabandika jina la ‘wapinzani’), kuendelea kuficha ukweli kuhusu suala la rada, na kuwakingia kifua wale wote ambao kutokana na nafasi zao walihusika katika ununuzi wa rada hii na kuteletea aibu isiyo na mfano.

Kwa bahati nzuri, maneno ya Rais Kikwete kutaka Bw. Mkapa aachwe asihojiwe hayana nguvu za kisheria. Swali ambalo wengi tunalo ni Je Rais Kikwete anataka ukweli kuhusu suala la ununuzi wa rada ujulikane? Kwa jinsi alivyozungumza mwanzoni mwa mwezi wa Februari, mtu anaweza kuamini kuwa Rais Kikwete alisikia kwa mara ya kwanza kuhusu bei ya rada hii miezi michache iliyopita. Na kwa jinsi alivyozungumza mtu anaweza kuamini kuwa Rais Kikwete kweli anataka ukweli juu ya rada uwe wazi kwa watu wote kuuona. Hata hivyo vitendo vyake vinatufanya tuamini kabisa kuwa Rais Kikwete hana nia, mpango, sababu, lengo, na kusudi la kutafuta na kuufuata ukweli wa suala hili mahali popote ukweli huo utakapompeleka.

Inakuwaje serikali iliyoshinda viti vingi Bungeni, na kushinda Urais kwa zaidi ya asilimia 80 ishindwe kutafuta ukweli wa jambo hili? Inakuwaje basi serikali ambayo inajigamba kwa kudumisha umoja, amani na mshikamano kushindwa kuunda tume huru ya uchunguzi ili ukweli ujulikane ili watu wawe na umoja, amani, na mshikamano katika kupambana na ufisadi uliokubuhu? Mbona haingii akilini kuwaacha wazungu wachunguze suala hili wakati sisi tumejibweteka na kuendelea kukaa mkao wa “omba omba”. Rais Kikwete katika mkutano ule wa Februari alidai wazi kuwa yeye “hana ubia” na mtu yeyote katika kiti chake cha Urais. Sasa huu wa Rais Mkapa umetoka wapi. Kama kweli Rais Kikwete anataka ukweli ufahamike angefanya kile ambacho kiongozi mahiri, asiye na ushikaji, na mwenye kujali maslahi ya Taifa lake angefanya; nalo ni kuunda tume huru, yenye nguvu za kisheria (kuita mashahidi na uwezo wa kutoa kinga) ambayo itapewa mamlaka ya kuchunguza ni akina nani waliohusika kwenye ununuzi huu wa rada na endapo watu hao wamevunja sheria yoyote na kupendekeza hatua za kuchukuliwa dhidi yao.

Hata hivyo hili la kuunda tume yenye nguvu namna hiyo haliwezi kutokea Tanzania kwani Rais Kikwete hawezi kuthubutu hata kidogo kuhoji kwa uwazi ununuzi wa rada hii. Sababu kubwa ni kuwa yeye mwenyewe ni mhusika mkuu katika mchakato mzima wa suala hili. Rais Kikwete alikuwa kwenye baraza la mawaziri wa awamu mbili zilizomtangulia. Wakati suala hili la ununuzi wa rada mpya lilipodokezwa mwaka 1993 Rais Kikwete alikuwa ni Waziri wa Nishati, Maji na Madini chini ya utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi na mwishoni kama Waziri wa Fedha. Endapo mkataba wa ununuzi wa rada hii ulifanyika chini ya Utawala wa Rais Mkapa, basi Rais Kikwete wakati huo alikuwa ndiye Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na tunakumbuka vizuri jinsi alivyotetea ununuzi wa rada hii kwa majigambo na kebehi kwa wale wote waliohoji bei ya rada hiyo.

Kwa mujibu wa Mbunge wa Uingereza Bi. Claire Short kuwa aliambiwa na rais Mkapa kwamba Mkataba wa ununuzi wa rada hiyo uliingiwa kabla ya yeye (Mkapa) kuingia madarakani basi bila ya shaka mkataba huo uliingiwa chini ya utawala wa Rais Mwinyi. Ni kwa sababu hiyo basi, siyo Mkapa peke yake ambaye anapaswa kuzungumzia suala hili na kuhusika kwake katika ununuzi bali pia Rais Mstaafu wa awamu ya pili Bw. Ali Hassan Mwinyi naye ahojiwe. Rais Mwinyi awaambie Watanzania ilikuwaje Watanzania tukanunua rada hii yenye bei ghali kiasi hicho na kama yeye mwenyewe au jamaa yake walinufaika kwa namna yoyote katika mchakato wa ununuzi huo. Viongozi wote wawili wawe tayari kuweka hadharani kama wanaakaunti za kigeni huko Uswisi au kwingineko na zina kiasi gani na pesa hizo zilipatikana vipi.

Kwa upande wa Rais Kikwete yeye mwenyewe awe tayari kuwaambia wananchi kuhusu kuhusika kwake katika ununuzi wa rada hii. Yeye alijua nini na ni lini ya kuwa rada hii ilinunuliwa kwa gharama kubwa zaidi kuliko ilivyostahili, kuwa dalali alilipwa dola milioni 12, na pia kama yeye mwenyewe au familia yake wana akaunti nje ya nchi na zina fedha kiasi gani ambazo alizipata vipi. Pia atusaidie kujua nani, alijua nini, na lini kuhusu rada hii kwani tuna mashaka kuwa kuna watu ambao hawataki kuzungumza.

Rais Kikwete na chama chake walipita na kuomba kura za Watanzania ili watuongoze; asilimia 80 ya wapiga kura wote walimchagua Rais Kikwete. Kuna baadhi ya watu (akiwamo Rais Mkapa) wanaotaka tuamini kuwa asilimia 80 ya Watanzania ndio waliomchagua Kikwete. Hilo si kweli hata kidogo kama wengi mnavyojua Kwa mujibu wa takwimu za Tume ya uchaguzi kati kati ya wapiga kura milioni 11.3 waliopiga kura milioni 9.1 ndio waliomchagua Rais Kikwete ambayo ni sawa na asilimia 80 ya wapiga kura wote. Kwenye taifa la watu karibu milioni 35 idadi hiyo ya watu milioni tisa ni sawa na asilimia 26 tu ya Watanzania wote. Ni kwa sababu hiyo basi lazima Rais Kikwete atambue ya kuwa hawajibiki kwa CCM bali kwa Taifa la Watanzania wale waliopiga kura na wale wasiopiga kura, ni maslahi ya watu hao ndio yanapaswa kumuongoza badala ya mapenzi kwa chama chake, utii kwa viongozi waliopita na kuendeleza kulindana ambako kumekuwa kama alama ya utawala wa CCM.

Kama kweli Rais Kikwete hana ubia, na kama kweli CCM ni chama kinachojali wananchi basi aamue viongozi wote waliohusika katika suala zima la rada wakiwemo Rais Mwinyi, Rais Mkapa, Mwanasheria Mkuu Chenge na wenzao wote wahojiwe (akiwemo yeye mwenyewe) na chombo huru ambacho kitatafuta ukweli na kuhakikisha kuwa kama kuna watu walionufaika isivyo halali na ununuzi wa rada hii wanarudisha mafao hayo, na pale ambapo sheria za makosa ya jinai zimevunjwa basi watu hao wanafikishwa kunakostahili. Kama Rais Kikwete ataendelea kutaka Rais Mkapa asihojiwe basi tunamuomba atuambie majina ya wale wote ambao yeye hataki wahojiwe ili tujue ya kuwa “kaka mkubwa” kasema fulani asihojiwe ili tusijisumbue kuhoji. Kwa vile Rais wa Jamhuri ya Muungano ameamua kumlinda Bw. Mkapa, basi aamue kuwalinda wale wote waliohusika na ununuzi ili tusiumize vichwa vyetu. Vinginevyo, Rais Kikwete aharakishe kuunda tume huru (isiyo na wabunge) ya kuchunguza suala hili.

Hata hivyo kuombea hili lifanyike chini ya utawala wa CCM ni kuombea mvua inyeshe jangwani, na kujaribu kuvua mamba kwenye kikombe cha chai! Halitatokea! hadi pale Watanzania watakapokataa majigambo ya mtoto aliyedekezwa mwenye kumkimbilia kaka yake kila akiharibu. Hili litatokea pale tu ambapo Watanzania watakapoamua kumuondoa kaka huyo madarakani na kudai haki yao ya kuishi pasipo vitisho na mazingaombwe ya kaka huyo. Vinginevyo watawala wetu wataendelea kugawana na kugawiana, kumega na kumegeana, kuwinda na kuwindiana, wakilinda, kulindiana na kulindana, wakila bila kunawa, waking’ata na kupuliza, wakitafuna na kutafuniana; huku wakiendelea kutafuna kile kidogo tulivyovuna tangu uhuru. Hata hivyo naamini miujiza, itatokea Tanzania?
 
Mzee Mwanakijiji said:
Kama kweli Rais Kikwete hana ubia, na kama kweli CCM ni chama kinachojali wananchi basi aamue viongozi wote waliohusika katika suala zima la rada wakiwemo Rais Mwinyi, Rais Mkapa, Mwanasheria Mkuu Chenge na wenzao wote wahojiwe (akiwemo yeye mwenyewe) na chombo huru ambacho kitatafuta ukweli na kuhakikisha kuwa kama kuna watu walionufaika isivyo halali na ununuzi wa rada hii wanarudisha mafao hayo, na pale ambapo sheria za makosa ya jinai zimevunjwa basi watu hao wanafikishwa kunakostahili. Kama Rais Kikwete ataendelea kutaka Rais Mkapa asihojiwe basi tunamuomba atuambie majina ya wale wote ambao yeye hataki wahojiwe ili tujue ya kuwa "kaka mkubwa" kasema fulani asihojiwe ili tusijisumbue kuhoji. Kwa vile Rais wa Jamhuri ya Muungano ameamua kumlinda Bw. Mkapa, basi aamue kuwalinda wale wote waliohusika na ununuzi ili tusiumize vichwa vyetu. Vinginevyo, Rais Kikwete aharakishe kuunda tume huru (isiyo na wabunge) ya kuchunguza suala hili.

Paragraph hii inamkumbusha Prezidenti ahadi yake ya hivi karibuni; ni wajibu wake kuitimiza kwa kuhakikisha kuwa hatumii uraisi wake kuhifadhi watu wanaoonekana kuwa wabia wake.
 
MWANAKIJIJI GET 100%.
Ni kweli hatuna cha wafalme,

Kama anasema tumuache Mkapa, basi yeye mwenyewe anapaswa kujua kuwa iko siku hata yeye tutamuhoji tu!

NINAWAOMBEA HAO WAFALME VIVULI WAISHI MAISHA MAREFU ILI BAADAYE WAJE WAWE KAMA PINOCHET. WATANZANIA WATAWAFIKISHA MAHAKAMANI TENA WOTE NA WAJUKUU ZAO KWA KUTUPELEKEA KUWA NA MAISHA MABAYA.

HUKU WAO WAKIISHI MAISHA MAZURI KULIKO HATA MATAJIRI WA KIZUNGU, YAANI KAMA VILE WAKO MBINGUNI!
TIME IS TOO SHORT TO LIVE HERE IN THE WORLD, WHY OUR SO CALLED VIONGOZI LIKE TO AMASS WEALTHY AND BADLY EXPLOIT OTHERS LIKE THIS!!!
 
Mzee MKKJ Hongera na nakubaliana nawe . wacha tuone sasa baada ya wito wako watasemaje .
 
Mkira,

Mzee sasa hao wajukuu wa hao maraisi wastafu wamekosa nini?? kama kuhojiwa ni hao Maraisi ndio wahojiwe, kwani kila mtu atabeba msaraba wake mwenyewe. Kosa la mtu mmoja lisiwe la watu wote
 
Mwanakijiji:

Hakikisha "Njamba" yuko karibu nawe saa zote, kwa maana unaelekea kuwanyima raha walaji. Jaribu kuwasiliana na Mh. Githongo, yule wa Anglo Leasing akupe mbinu kidogo.

Kinachosikitisha zaidi ya yote ni kukosa vyama vya upinzani vinavyoweza kuelezea na kushawishi kwa kina ili wananchi wa kawaida waweze kuyaelewa vizuri mambo kama haya! Sielewi wanashindwa vipi: mbona wewe unayaeleza vizuri tu? Ninayo hakika kuwa waTanzania sio wajinga wasiokuwa na uwezo wa kuelewa vizuri mambo kama haya.

Sitoi hukumu yoyote hapa; lakini serikali yenye 'uwazi' na inayofanya mambo kwa manufaa ya taifa letu kama hii iliyopo madarakani, inao wajibu wa kuyatolea ukweli mambo mhimu kama hili. Vinginevyo, imani za wananchi hutoweka.
 
Mzee MKKJ Hongera na nakubaliana nawe . wacha tuone sasa baada ya wito wako watasemaje .

Lunyungu, do you seriously expect any action on the part of the govt, simply because Mkjj wrote a stimulating 'piece' in JF?

Thank you for letting us know that you 'passed-by' here.
 
Kalamu wakati unangoja vyama viseme navyo vinangoja watu wa aina yako waingie ili wakasemee toka kwenye Vyama vipi kama unakata shauri na kujiunga na Upinzani ili uongeze nguvu ya kusema ? kwani Upinzani ni nani ? Si hata wewe unaweza kuingia na kutumia nafasi hiyo kutoa shule ?
 
Habari za asubuhi wandugu!
Napenda kuizungumzia hii mada ingawa nahisi lazima ilishawahi kujadiliwa humu coz ni moja ya vitu ambavyo vinatokea mara nyingi katika mazingira tunayoishi.
Walonifanya niandike hii Thread ni hawa jamaa wa EATV, katika kipindi chao cha EA STAT cha jana ingawa walikua wanazungumzia mada ya Freedom of press but kuna watu (I guess ni vijana tena ni Christians) waliandika E-mail kuhusu mada tofauti na hiyo amabayo ilikua ikizungumzwa, walisema kwamba waliandika barua kuomba kazi katika ubalozi falme za kiarabu hapa nchini but wakadai kwamba walifanikiwa kufika katika hatua za mwisho kabla ya kuajiriwa lakini balozi akawanyima ajira ati kwa kuwa ni wakristo!!!

Mi sina problem na maoni yao ya kuwa wamebaguliwa kupata ajira ubalozi wa UAE kwa ajili ya ukristo wao, kusema kweli hilo halinihusu kabisa coz kila mwajiri anakua na vigezo vyake (Vya siri na dhahiri) vya kumpata mtu ambaye atamuajiri, Kwanza mi sidhani kama kuna muislam anafanya kazi katika ubalozi wa Vatican hapa nchini! Tuyaache hayo.
Problem yangu ni kwa hawa jamaa wa EA STAT (Dany na Carol) kushadidia sana hiyo ishu ya kubaguliwa kwa wakristo kama walivyodai wao, mi nadhani walikosea sana kusema vile coz huwezi kulazimisha kitu kama hiko.

Na kama ni ubaguzi basi EATV ndio wanaongoza kwa ubaguzi wa kidini humu nchini. Natoa mfano mdogo sana, humu nchini tanzania i guess kuna dini nyingi sana but the most popular ni Uislam na Ukristo, na EATV ni channel ambayo inaangaliwa na watu wa dini zote, sasa kwa nini kila siku asubuhi wanaweka nyimbo za kikristo (Gospel) ilhali wakijua kwamba hii nchi ina dini nyingi? kuna nyimbo nzuri nyingi tu za kiislam but mbona hazionyeshwi EATV? sasa huu si ubaguzi wa kidini? Akina Dany naomba jibu.

Huo ni mtazamo wangu tu jamani naomba tujadiliane!!
 
Kwaza wewe mwenyewe ni mdini na huwezi kuona mambo kwa upana . Pili inakuwa shida ssi kuchangia maana wengine haya hatujayaona kwenye TV na kufuatilia ila tunasikiliza version yako ambayo tayari umesha chukua side .

Lakini Vatican Ubalozi wao hawawezi kumweleka Muislam mtumishi maana unajua ni Ubalozi wa vatican wakatoliki wale na UAE si udini ni Nchi sasa kama na wao wanakuwa kaa vatican sawa wana uamuzi. Ubaguzi upo sana na ukigusa waarabu dhidi ya Ukristo upo mwingi tunaanzia Sept 11 japokuwa waliua hata waislam , na mambo mengine ya Jihad ni vita dhidi ya Ukristo .

TV na nyimbo za dini , well nikusaidieje ? Sheria zinasemaje ? Huna ukazima wa kuangalia TV muda wa nyimbo za dini ukitaka .

Mambo mengine ni kutupotezea muda .Issues kama hizi zina mambo mengi endeleeni kulumbana huko huko na udini wenu haoa tuachieni siasa za bila udini .
 
Wabunge: Mawaziri kikwazo cha kupambana na rushwa
+Mzindakaya atishia kuanza kulipua 'mabomu'
+Wataka mikataba mikubwa ipelekwe bungeni

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

MAWAZIRI wawili akiwemo wa TAMISEMI wamelalamikiwa na wabunge kwa kukalia kwa muda mrefu tuhuma za rushwa walizopelekewa. Mbali ya madai hayo, wabunge wametishia kuanza kulipua 'mabomu' kutokana na kutokupata majibu ya taarifa walizoziwasilisha kwa mawaziri hao.

Wabunge walitoa madai hayo jana wakati wakichangia mjadala wa muswada wa vita dhidi ya rushwa uliowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Philip Marmo. Akichangia mjadala huo, Dk. Zainab Gama (Kibaha Mjini-CCM) alisema halmashauri ya Kibaha ilipatiwa sh. milioni 300 ambazo baadaye zilipelekwa katika benki ya CRDB ambayo haiko Kibaha.

Alisema kwamba alipojaribu kuhoji katika baraza la madiwani na kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya hakupata majibu, hivyo aliamua kumuuliza waziri wa TAMISEMI.

"Nilipoona huko sipati jibu la kuridhisha niliamua kumuuliza waziri wa TAMISEMI ambaye aliahidi kufuatilia, lakini hadi sasa muda mrefu umepita hakuna jibu lolote," alisema Dk. Zainab. Alisema suala la rushwa lisifanyiwe mzaha na kuwa wahusika wafungwe jela kwa kuwa hatua hiyo itawadhalilisha.

Mbunge huyo pia alipendekeza mikataba mikubwa iwasilishwe bungeni na kuchunguzwa na kuondokana na tabia ya sasa ya kuifanya siri. Dk. Zainab alisema pia Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) asipewe mamlaka ya mwisho ya kuamua kuhusu kesi zinazohusisha masuala ya rushwa. Alipendekeza kuwepo na kipengele cha sheria kinachotoa nafasi kwa maofisa wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB) kuendelea na mashitaka iwapo DPP atashindwa kutoa uamuzi wa kusikilizwa au kutosikilizwa kwa kesi za watuhumiwa wa rushwa ili waendelee na kesi.

Mbunge huyo alimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa jambo lililofanya baadhi ya maofisa kumshangaa walipomkuta akiwa waziri wa mambo ya nje, nyumbani kwake akitumia mkaa kupikia. Kwa upande wake, Dk. Chrisant Mzindakaya (Kwera-CCM) alisema anasikitishwa na baadhi ya watendaji wa serikali wakiwemo mawaziri kukalia taarifa za rushwa bila kuzifanyia kazi.

Dk. Mzindakaya alisema kutokana na tabia hiyo, wabunge hawatasita kuanza kulipua 'mabomu' kutokana na tabia yao hiyo. Alisema alitoa taarifa ya vitendo vya rushwa kwa waziri mmoja (hakumtaja jina) kuhusiana na vitendo vya rushwa, lakini waziri huyo amekalia taarifa hiyo kwa zaidi ya miezi minne sasa bila kuchukua hatua.

"Haya mambo tuwe nayo makini. Niliwahi kumpa waziri taarifa kuhusu rushwa, lakini hakunijibu lolote na hata kunishukuru kwa kumpa taarifa, hajafanya hivyo...sasa ni miezi minne imepita. Sisi wengine ni watundu tunapata taarifa, tukianza kurusha makombora mawaziri msitulaumu," alisema Dk. Mzindakaya.

Mbunge huyo alisema baadhi ya wabunge wanashindwa kukemea vitendo vya rushwa kutokana na kuwa na matarajio ya kuteuliwa kuwa mawaziri. "Kuna mambo mengi yanatendeka, lakini hatuwezi kuyasema humu," alisema.

Alipendekeza mawaziri wasitokane na wabunge kwa kuwa hali hiyo inawafanya kuoneana aibu na kutoa mfano wa waziri mmoja kumlalamikia mbunge kuwa anamsakama kutokana na kuhoji mambo mbalimbali.
Mzindakaya pia aliponda utaratibu wa kuwakamata wahusika wa rushwa ndogo kama za sh. 10,000 hadi sh. 30,000 na kuwa rushwa ipo kwenye mikataba ambayo wanatakiwa kuanza kupambana nayo.

Kwa upande wake, Dk. Harrison Mwakyembe alieleza kushangazwa na serikali kushindwa kutoa taarifa kwa wabunge na badala yake kuzitoa kwenye vyombo vya habari hasa magazeti na kuhoji hali hiyo ni kwa faida ya nani.
Alisema hali hiyo inashangaza kwa kuwa kamati za bunge mara nyingi zimekuwa zikiomba taarifa mbalimbali za serikali lakini inakuwa vigumu kuzipata huku taarifa hizo zikipenyezwa kwenye vyombo vya habari.

Dk. Mwakyembe alisema mbali na hilo, inashangaza kuona mikataba mikubwa ya nchi haipelekwi bunge kujadiliwa na kuwa wabunge wanaonekana hawana nguvu. "Hii ni nchi yetu wote, lazima tuseme kama mambo hayaendi sawa," alisema Dk. Mwakyembe na kuwa suala la rushwa liangaliwe kwa dhati kwa kuwa ni vita ngumu.

Aggrey Mwanri (Siha-CCM) alipendekeza wala rushwa wanapobainika wafilisiwe na aliapa kuwa ndani ya CCM kiongozi atakayebainika kujihusisha na rushwa jina lake halitapitishwa kwenye kuwania nafasi za uongozi.

Mwanri alisema bila kupambana kwa dhati na vitendo vya rushwa katika siasa inaweza kutokea bungeni wakaingia watu ambao hawakustahili na wale wanaofaa wakaachwa nje. "Suala la mapambano ya rushwa lipo ndani ya ilani ya CCM," alisisitiza Mwanri.
 
Back
Top Bottom