Hii ndiyo Tanzania tunayoitaka

Interested Observer said:
Kulikoni, soma tena ile habari: Kuna REginald Mengi na Benjamin Mengi au siyo?

Asante mzee, kumbe huyu ni Mengi mwingine! My apologies to the other Mengi to unknowingly link him on this. .. unajua tena yakitajwa mabiashara na jina la Mengi .. most of us know only one of them.

Shukran tena mzee IO.
 
DrWho,

Heshima yako mkuu, kichwa cha habari na habari yenyewe hazifanani kabisaa, huo ndio uandishi uchwara, kichwa kilipaswa kusema kuhusu malalamiko ya mbunge na sio kama kilivyosema, no! ni uandishi uachwara huoo tunaoukataa sana huku bongo!
 
Mwanakijiji,'
Ni mdogo wake Reginald. Ninavyosikia aliingia ubia na huyo Mwingereza lakini hakuna na nia ya kutimiza. Mzungu alipoleta fedha zake akamwanzishia vitimbi na kwa kuwa anafahamiana na wakubwa akasuka yule mzungu atiwe ndani.
 
that is what I thought... sasa sijui kama "This Day" wanaweza kumchunguza mdogo wake Bosi.... na kulivalia njuga kama wanavyomfanyia Manji....
 
Nimeona makala kwamba Uganda nao wanatumia 25% ya bajeti yao kwenye Elimu. Angalau hivyo ndivyo ilivyokuwa kwenye bajeti ya Uganda ya 2003/2004. Sijapata ya mwaka 2006/2007

Angalia http://www.efa.nairobi-unesco.org/efaX/index.php?option=com_content&task=view&id=20&Itemid=47

Sasa Kenya wanatenga 27% ya fedha zao kwa ajili ya elimu, Uganda wanatenga 25%, na sisi tunatenga chini ya 10%. Kama nilivyoainisha hapo nyuma, Malawi na Msumbiji vile vile wanatenga sehemu kubwa ya bajeti zao kwa ajili ya Elimu.

Tumezungukwa na watu wanaojua umuhimu wa Elimu, sio kwa maneno tu bali kwa matendo. Kwa nini sisi pekee ndio tunatoa lip service kwenye Elimu? Miaka ijayo tutaonekana kama taihira mbele ya majirani zetu.

Augustine Moshi
 
Augustine Moshi,

Kusema Uganda wanatumia 25% na Kenya 27% ya bajeti zao , bila ya kuwa na bajeti zao haitasaidia kitu . Tupatieni kwa figure za uhakika tujue bajeti ya uganda au kenya ni kiasi gani then tuzidi kwa hizo asilimia mlizotupa .
 
Mzee ES, nitawajaribu tena.. kwani wana mengi ya kujibu.. ila inaonekana wao hawataki kuulizwa maswali....
 
Ndugu Rufiji,

Hiyo asilimia inapima umuhimu uliowekwa kwenye Elimu. Hata hivyo, takwimu zinapatikana kwenye websites za nchi husika. Kwenye hizi mada nilishataja kwamba 27% ya bajeti ya Kenya ya 2006/2007 ni KSH.99 billion. Hizi ni kama TSH 1.485 trillion. Na ni fedha zao, hawakuweka hata senti moja ya wahisani kwenye bajeti yao.

Vile vile, kiasi cha bajeti ya Kenya kinachotengwa kwa ajili ya Elimu kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwenye bajeti ya 1999/2000, walitenga KSH. 48.3 billion kwa ajili ya Elimu. Kiasi hicho kiliongezeka kuwa KSH 49.9 billion kwenye 2000/2001 budget, KSH. 56.3 billion kwenye 2001/2002 budget, KSH. 66.4 billion kwenye 2002/2003 budget, KSH. 80.2 billion kwenye 2003/2004 budget, and so on, hadi kufikia hiyo KSH 99 billion ya 2006/2007 budget.

Matokeo ya kukazania Elimu hivi huko Kenya ni kwamba kuna wanafunzi wengi zaidi, wana waalimu, na shule zao zina madawati na vyoo. Hii aibu tuliyonayo ya shule ambazo hazina vyoo ni matokeo ya kuinyima Elimu fedha.

Augustine Moshi
 
Hapo wazee na mimi nawaunga mkono kwa kweli uwekezaji kwenye elimu ni mdogo mno. Hebu angalieni takwimu hizi hapa chini.

Density of tertiary students (per 10, 000 inhabitants)

Year TZ UG Zamb Nigeria
1980 22 45 128 229
1985 22 69 181 352
1990 26 107 212 ND
1991 28 126 ND ND
1992 29 124 ND ND
1993 33 135 ND 410
1994 36 150 238 ND
1995 43 160 ND ND
1996 48 179 ND ND
1997 57 ND ND ND


Source:http://www.scidev.net/dossiers/index.cfm?fuseaction=printarticle&dossier=13&policy=66&section=391
 
Bajeti yote ya Tanzania kwa mwaka wa fedha 2006/2007 ni TSH.4,850,588,000,000 (shilingi trilioni 4, bilioni 850, na milioni 588). Hizi ni fedha nyingi, kwani ni kasi cha sh. 138,588 kwa kila Mtanzania.

Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ni TSH. 239,650,710,000 (shilingi bilioni 239, milioni 650 na elfu 710)

Bajeti ya Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ni TSH. 167,610,218,000 (shilingi bilioni 167, milioni 610 na elfu 218)

Ukujumlisha bajeti za wizara hizo mbili za Elimu, unakuta bajeti yote ya Elimu Tanzania ni TSH. 407,260,928,000 (shilingi bilioni 407, milioni 260 na elfu 928). Hii ni 8.396% ya bajeti yote ya Tanzania. Ni sehemu ndogo sana ya bajeti yote, na hili lina matatizo makubwa.

Augustine Moshi
 
Mimi naona ni sawa tu akiitwa BM maana JK anafanya yale yote ya BM hakuna tofauti ama unasemaje ?
 
Asilimia 8 tu ya bajeti yote inaenda kwenye elimu? Hii ni kasi mpya kuelekea kwenye ujima. Sishangai wananchi wanapochangamkia kuchangia harusi badala ya harambee ya elimu. Serikali imeonyesha njia kuelekea kwenye ujinga.....
 
Mzeeshughuli Bwana said:
Mimi naona ni sawa tu akiitwa BM maana JK anafanya yale yote ya BM hakuna tofauti ama unasemaje ?

Naomba kukuunga mkono...
 
Wakati wa uraisi wa Mwalim, nchi ya Tanzania ilikuwa na mazuri na pia mabaya na Mwalim alichangia sana hali hiyo. Ili tuelewe tutokako, tulipo na tuendako ni vizuri tukautafakari wakati ule kwani ndio uliokuwa unapanda mbegu za baadaye.

Labda nianze hapa:

Tulipopata uhuru Mwalim akawa Waziri Mkuu na haukupita muda akauwacha uwaziri mkuu huo na kumkabidhi Mzee Kawawa wakati yeye anajitayarisha kugombania uraisi. Makabidhiano haya yalifanyikaje na yalifuata kanuni za demokrasia au yalifanyika katika njia za udikteta?
 
Unataka nini hapa, tafadhali fafanua vizuri swali lako.

Naona umekumbusihia jambo jingine la maana hapa. Wewe na wengine mnaosema Nyerere alikuwa na udini, kwa nini alimpa Kawawa uwaziri mkuu wakati siyo mkatoliki. Kama angejali sana dini, angempa madaraka hayo Oscar Kambona ambaye alikuwa na elimu nzuri kuliko kawawa. Kwanza kabisa Nyerere siyo kweli kwamba aliachia uwaziri mkuu kusudi ajiendae na urais, umepotosha; angeweza kubakia waziri mkuu hadi mwisho na baadaye kuwa rais kama ambavyo Obote na Mugabe walivyofanya.
 
Kichuguu,
Wewe ndugu unaonekana udini hasa ukatolic uko kwenye damu kwani udini umekuwa ndio kibwagizo chako. Hongera!

Hebu tueleze hizo sababu alizowachia uwaziri mkuu. Hata hivyo umemiss the point hapa, msisitizo sio kuuwacha uwaziri mkuu tu bali tatizo ni kuugawa kama njugu alivyotaka yeye na hatutilii maanan kuwa kampa nani. Hata hivyo angempaje Kambona. Ninakumbuka mkutano mmoja kabla ya uhuru ambapo Nyerere alirudiarudia maneno haya jukwaani "Oscar ninamwambia aseme, hataki". Sijuwi Oscar alikuwa anatakiwa aseme nini na nini alikuwa anakataa. Angempaje uwaziri mkuu mtu aliyekuja kumuita kibaraka (hata hivyo maana ya neno kibaraka siyo hiyo aliyolibatiza neno hilo Nyerere!) na aliyedai kuwa hakuwa raia wa Tanzania bali Mnyasa - sasa wewe ulitaka ampe uwaziri mkuu mtu ambaye alijuwa kuwa hakuwa Mtanzania.

Jokes nyingi sana humu!!!

Majadiliano yako hayaonyeshi kuwa hukuelewa nilichouliza. Labda nirudie nikupe muda wa kuyatafakari na kuchangia:

"Labda nianze hapa:

Tulipopata uhuru Mwalim akawa Waziri Mkuu na haukupita muda akauwacha uwaziri mkuu huo na kumkabidhi Mzee Kawawa wakati yeye anajitayarisha kugombania uraisi. Makabidhiano haya yalifanyikaje na yalifuata kanuni za demokrasia au yalifanyika katika njia za udikteta?"
 
Naona ujinga unaendelea katika hii bodi , Yaani kwa kuwa watu wanampinga kikwete katika mambo fulani basi watu wanataka kucounter attack kwa kumsema Nyerere ? Kwani nyerere aliacha urais lini ? na jee matatizo yetu yote tuliyonayo yameletwa na yeye ...kwa hiyo hata huu mkataba feki wa kampuni ya Richmond aliusaini yeye ?

Jamani tukue acheni kupoteza muda kudiscuss kuhusu mtu aliyeacha urais miaka ishirini iliyopita , tuangalie tunaelekea wapi ! tuache ushabiki wa simba na yanga.
 
Wanabodi,

Leo hii nitawapa picha halisi ya uongozi wa marehemu baba wa taifa Mwl. Julius kambarage Nyerere kwa mitazamo tofauti. Nyerere hakuwa mtume wala nabii isipokuwa kiongozi wa kwanza wa mama yetu Tanzania.

Nyerere siii kiongozi aliyemtoa bikra mama Tanzania kwa hiyo, matatizo ya Tanzania hayakuanza toka kwake bali yalianza kabla ya Uhuru na yatazidi kuendelea ikiwa sisi hatutakaa na kujitazama wapi tumekwama. Na sii vizuri kuunganisha zamani na leo ktk mkondo mmoja kwani leo hii tunakabiriwa na tatizo moja dogo lakini limekuzwa kutokana na uongozi mbaya -ACCOUNTABILITY!
Nyerere alikuwa na matatizo yake na moja wapo ilikuwa UBINAFSI. Lakini kwa msomi wa uongozi atakubaliana na mfumo wa Nyerere wakati ule kwani tulikuwa nchi changa inayohitaji Dikteta!..na dikteta yeyote lazima uwe mbinafsi ili kuhitimisha azma yako.
Was he?... jibu lake ni YES!
Wapo watakao kataa na kusema vinginevyo lakini mifano mingi sana ilijitokeza wakati ule ikiwa ni pamoja na kuwapunguza nguvu Ma-chief (Watemi) kwa kuwapeleka nchi za nje kama mabalozi. Ukiwa tishio kwake atakuweka nje ya uongozi na picha ya kitaifa. Hii ilimpa nafasi yeye kuweza kuingia mikoani kama rais na hakuna mtu juu yake ktk jitihada zake za kukata UKABILA.
Now, tunaweza kusema vyovyote vile kuwa ni dikteta, wivu n.k lakini Nyerere aliweza kufanikisha azimio lake la kuondoa UKABILA kwa njia ambazo mnaweza kutozikubali. Wasukuma, Wahaya, Wachagga na Wahehe hawakufurahia mfumo huo na kuona kama waliburutwa kwa kiasi fulani lakini wasingeburutwa kweli tungekuwa hapa tulipo?.
Hivyo hivyo katika dini kabla ya Uhuru waislaam walikuwa na nguvu sana ktk lindi la siasa TZ. Na isingekuwa rahisi kuondoa UDINI kama asingechukua baadhi ya hatua kama alivyochukua hatua za Ukabila ambazo leo hii tunafurahia matunda yake. Binafsi kinacho-matter kwetu Watanzania as a society ni results za mifumo yake. Hakuna amani inayokuja bure bila majeruhi.

Kwa hiyo tafsiri zinaweza kuwepo mia kidogo na zenye kila sura lakini muhimu ni matokeo ya mbinde hizo. Leo hii tupo hapa tunajadili maswala haya kama vile hadithi tu maanake kati yetu hakuna mtu aliyepitia athari za Ukabila wala Udini ila tunazisikia tu ktk bomba ama Luninga kwa sababu Nyerere alizifuta kabisa. Hivyo basi alifanikisha mambo makubwa na mazuri sana kwa majeruhi kidogo. Hivi kati yenu kuna mtu kesha fikiria ikiwa Nyerere hakufanya hayo leo hii tungekuwa wapi ktk Ukabila ama Udini!.Hivi kweli Mwinyi, Mkapa na hata huyu JK wangeweza kweli kuwa marais leo hii?..Labda nambieni kuwa hilo lilikuwa kosa kubwa na ndio maana kuturithisha marais bomu, lakini sidhani kabisa kama kungekuwa na marais toka ktk makabila madogo acha mbali makabila madogo kupata elimu.
Je, mmewahi kujiuliza mama zenu waliolewa wakiwa na umri gani?... mnajua kabla ya Uhuru wanawake wengi waliolewa wakiwa na umri wa miaka 14 hadi 18. Hapa hawakuhesabika kabisa ktk elimu. yaani mwanamke akifika 20 huyo kisha chelewa na hatapata mume lakini baada ya Nyerere kushika madaraka tumeona mabadiliko, leo hii tuko radhi kutukana watu wanaotembea na watoto wa chini ya miaka 18 hali wote sisi mama zetu waliolewa wakiwa na umri mdogo. Haya ni matunda sokoni tena tumepewa bureee hatufahamu mkulima alichukua jitihada gani kuyalima.
Kwa hiyo jamani, alifanya hiki ama hakufanya haina sababu kabisa ikiwa lengo ni ubora wa maisha kwa kizazi kijacho. Wenzetu hawaendelei kwa sababu ya rais wao wa kwanza na hakuna historia yoyote ama analysis yoyote ya uchumi inayosema maendeleo hutokana na rais wa kwanza... ACCOUNTABILITY ni tamaduni ngeni kwetu.. wakati wa Nyerere tulisema huo ni Udikteta na tulitukana sanaaa, hali wenzetu nchi za magharibi Accountability is built into their daily lives.
Waendesha magari wanaheshimu taa za barabarani kama vile ni ibada kwao bila traffic polisi kuwepo. Bongo tamaduni ndogo kama hiyo ama kupanda bus kwa mstari bila kupitia madirishani jambo ambalo haliwezekani kabisa. Lazima awepo askari kuhakikisha sheria zinafuatwa laa sivyo kila mtu na mzigo wake. haya ndiyo maisha tuliyokuwa nayo leo na sii Nyerere wala baba yake ila sisi wenyewe shurti twende kwa fimbo. Hatuwezi kumsema Nyerere kama ndiye katufundisha kudandia na kuruka taa nyekundu.
 
Back
Top Bottom