Mimi sielewi hivi mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, mbunge na madiwani wanafanya nini au ni nini kimeshindikana hadi watoto wakae chini wakati sijaona Landcruiser za wakubwa hawa zimekosa mafuta??
source: Majira
Hakika hii picha ukiiangalia mara 2 unaweza kutoa machozi, ni kweli taifa linaloweza kununua gari moja kwa TZS 110,000,000 linalomtoa waziri, katibu au Mkurugenzi masaki kwenda posta na kurudi linashindwa kutoa TZS 500,000,000 kununua madawati ya nchi nzima
hizi ndo ajabu ukienda baa,hotel hukosi kiti lakini watoto wanasoma eti wnakaa chini, ndo watawala wetu hao halafu wapo kifua mbele,dah inatisha
Pole sana Bill lkn hii ndiyo Tanzania na Chama Chao cha kupindu aka CCM nambali one...maisha bora kwa kila mdanganyika....kuna watu wana hasira na CCM lakini watapozwa na Kanga, T-shirt, Kofia, Pilau (msosi) then watasahau shida zao zote na maisha yanaendelea... sijui tuwaelimishaje wadanganyika maana mpaka kero, maana ukiangalia maswala ya EPA, magari wanao tembelea viongozi wetu,richmond,melemeta,majengo pacha ya BOT, mgao wa umeme nk halafu uangalie halisi ya wadanganyika kweli machozi yatakutoka... kama kweli watanzania tunakereka basi tuwaonyeshe Tarehe 25/10/2009..Hakika hii picha ukiiangalia mara 2 unaweza kutoa machozi, ni kweli taifa linaloweza kununua gari moja kwa TZS 110,000,000 linalomtoa waziri, katibu au Mkurugenzi masaki kwenda posta na kurudi linashindwa kutoa TZS 500,000,000 kununua madawati ya nchi nzima
kwanza hata mfumo wa watoto wetu kukalia madawati umepitwa na wakati kwa nini tusitumie viti vya plastic tu?? Najua watasema oh...mara siyo imara lakini hivyo imara kama tunashindwa kwa nini tusitumie ambavyo tunakalia baa??
Prof. Maghembe mwenyewe anajua tuliwahi kukaa naye pale kwenye baa ya kambarage morogoro na tulikalia viti vya plastic, je anashindwa nini kuvitumia kusaidia watoto wetu mashuleni??
Zipo hata meza za plastic ambazo bei yake ni nafuu, hili pia najua wabongo watasema ah.... mbona zinavunjika haraka lakini swali ni je, hizo imara tunaziweza?? na kama tunaziweza kwa nini CCM na serikali yao wanazishindwa??
Prof. Maghembe, tunataka mabadiliko????
Binafsi sioni sababu ya kutumia meza na viti vya plastic, iwe bar, shuleni au nyumbani. Mtu huishi kutokana na mazingira yaliyomzunguka. Tumezungukwa na ardhi kubwa na misitu ya kupandwa ya mbao laini (soft wood) kama Cyprus, bines, mikaratusi nk.
Wenzetu kule Uarabuni, Asia na hata Ulaya hawana soft wood za kutosha ndo maana wanatumia plastic. Hawa jamaa wangekuwa wanaishi Africa hata viti vya mabasi vingekuwa vya mbao.
Tatizo letu tunapenda kutumia vitu wanavyotumia wenzetumpaka tumefanywa soko la kila kitu. We don't need plastic chairs/tables. Lets be innovative.