Hii ndiyo NMB

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
Kuweka pesa akaunti isiyo yako 1000.00, kuangalia salio 200, kuchukua pesa ATM 400, kuchukua pesa ndani 700, service charge per month 500

. Hii ni nini kama siyo wizi? kuna faida gani ya kuweka pesa benki? naona nirejee mbinu ile ya babu ya kutunza vichele vyangu kwenye kibuyu, pesa yenyewe naipata kwa shida, akaunti yenyewe ina pesa isiyofika hata 200000, niweke NMB so what? naibiwa tu!
 
Hyo ndo NMB zaidi ya usivyoijua na ukitumia NMB MOBILE ndo utashangaa zaidi wanakuibia live.
 
Ndo maana yule Mh. aliiita benki ya makabwela kumbe mambo yake makubwa ati,
 
majizi!lakini watumishi wa umma hawana choice cuz taasisi za serikali zina account na nmb,..ukijifanya mshahara upitie benki nyingine utapata mshahara baada ya wiki mbili tokea wa nmb wapate(mshahara wenyewe kichekesho)
 
Kibubu bank ndo mambo yote, faida zake ni kama,
haina foleni,
network haisumbui,
24 hrs,
huwez kusahau password,
haina makato/charges,
atm card haimezwi,
teller na customer ni wewe mwenyewe n.k.
 
Uzuri wa NMB ni kama wewe ni mtu wa kusafiri hasa vijijini ndiyo utaona unafuu wake vinginevyo waizi tena chunga sana kutumia simu wanaiba sana...
 
mh kumbe ndio walivyo yani ukiweka pesa wanakuchaji? Ukitoa ivyoivyo? Ss inafaida gani kwa walalahoi benki ya ukweli ni azania bank akuna upuzi wa makato
 
Kweli NMB wanaboa, hivi kwa nini wasitangaze kwanza kwa muda fulani ndo waanze kukata hayo makato yao ili tuangalie ustaarabu wetu! Maana last week nimeenda kutuma hela wakaniambia nilipe sh. 1000 nami sikuwa najua, yaani niliboreka sana nikauliza ina maana hata ATM nayo ukitoa hela unakatwa? teller akaniambia hapana, kumbe unakatwa? jamani kuweka hela bank ni usumbufu kwa kweli kufungua account kwenyewe taratibu zake yahitaji moyo!!!!!!!! ndio maana babu zenu walikuwa wanazichimbia chini na kwenye vibuyu kuliko style hii yaani ni hasara tupu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom