Hii ndiyo Mizigo TISA ambayo JK alijibebesha

Wakuu zangu, JK ni reflection yetu sisi wenyewe...Uzalendo hauletwi na kiongozi bali wananchi wenyewe kuwa na uchungu wa mali yao wenyewe..

1. Grand Corruption - Hii imeanza toka wakati wa Mwinyi viongozi kujilimbikiza mali na hakika kwa kila msomi akipewa madaraka alifikiria kuiba na kujineemesha. - Grand Corruption imenza na RUKSA baada ya kuondoa Azimio la Arusha. JK hawezi kurudisha azimio hilo ambalo Watanzania wengi hawapendi hata kusikia wala kujihusisha na mfumo unaowakwaza viongozi kujitajirisha. tuwe wakweli ktk hili kwani sidhani kama ni JK aisyependa isipokuwa Watanzania wenyewe wanapenda kuona miiko ile imeondoka.
Leo hii Mtanzania yeyote aliyeajiriwa na serikali ktk vyombo vyake iwe TRA, BoT, Bandari, Ardhi, NHC,Banks ni wezi kwa kwenda mbele. Na Mzalendo yeyote akisimama atatafutiwa mganga alishwe sumu ya mamba..There is little JK can do if WE don't play our part.

2. Hoja ya Wapemba na Unguja - Hili sii swala gumu kwa sababu cheche zake huanzishwa na viongozi walioko madarakani. Toka wakati wa Salmin Amoor kumekuwa na mgawanyiko baina ya Pemba na Unguja kisiasa zaidi ya Ukweli..Chama cha CUF kikituhumiwa kuwa ni chama cha Wapemba na CCM chama cha Waunguja (Wangazija). Leo hii yapo mabadiliko makubwa sana ambayo yametokana na Uzalendo wa Wazanzibar wenyewe...Wazanzibar leo kwa pamoja wameweka pembeni tofauti zao kutokana na issues zinazohusu Muungano na nafasi ya Zanzibar ktk Muungano wetu.

3. Mgogoro wa Muungano - Hili ni swala gumu zaidi na hakika Wazanzibar wamejipanga vizuri kulilia haki na nafasi yao ktk Muungano.Tatizo liko bara ambako watu tumegawanyika kwa sababu hatuitambui Zanzibar kama ni nchi au Taifa pamoja na kuundwa kwa Muungano. Ni makosa aliyorithi JK toka mfumo uliokuwepo wa kiutawala. Serikali ya Muungano imejengwa na kuongoza Bara zaidi ya Muungano, wakati Visiwani wanajiongoza ili kuweka tofauti baina ya nchi hizi mbili zisizokuwa tofauti kwa kauli za viongozi.

Hakuna njia rahisi ya kuondoa mgogoro huu bila kuitambua Zanzibar kama ni nchi tuloungana nayo kwani hata ndoa iliyofungwa baina ya mume na mke haiwezi kuunganishwa hadi nafsi zao.. Tulichojaribu kujenga Tanzania ni fikra za kwamba nafsi mbili zinaweza kuwa moja.. Hakuna kitu kama hicho labda ktk Uungu wa Kikristu...

4. Ujenzi wa Shule za Secondary na JKT - Bila shaka ujenzi wa shule za Secondari bado unaendelea isipokuwa makosa makubwa yamefanyika ktk misingi ya ujenzi wa elimu yenyewe nchini. Tanzania kama nchi maskini duniani inatakiwa kuchukua Elimu ni HAKI ya kila mwananchi hivyo investment kubwa ya kwanza ni kuwapatia wananchi elimu inayowawesha kuwa waajiri wa taifa la kesho. Tulipokubali kushindwa kwa Ujamaa, tulishindwa kufahamu Ujamaa umeshindwa kwa sababu zipi.. nini yalikuwa malengo ya Ujamaa na yalishindwa vipi kufikiwa..

Hivyo kama adui zetu walikuwa Umaskini, Ujinga na Maradhi na Ujamaa ukashindwa kuvithibiti, ilitakiwa tutafute mbinu nyingine mpya ya kupambana na madhara hayo badala ya kubadilisha policies ili mradi tunaiga nchi Tajiri ambazo zimejenga policies zake ktk kugawana Utajiri.

Hadi kesho, mimi siamini kama private schools na private Hospitals ni solution ya elimu na Afya ktk nchi maskini isipokuwa mfumo huu ndio chanzo kikubwa cha UFISADI na wizi maofisini.. kwani kila mwananchi atajitahidi kuvuna fedha zaidi ili kusomesha na kumtibu familia yake kutokana na pato dogo ambalo halikidhi mahitaji ya kila mwananchi kukabiriana na adha hizi..

Mfumo uliopo umeyafanya maadui wetu yaani Umaskini, Ujinga na Maradhi kuwa ni Privilege badala ya HAKI ya kila maskini (wananchi)...JK hawezi kuwa na solution ikiwa kila Mtanzania anaamini kuwa The way to go, is Privatise even our our rights wakiiga nchi za Ulaya.

5. sikuona kitu....

6. Udini - Swala la Udini ni letu sisi wenyewe wananchi baada ya kukubali private schools kuingia nchini. Shule hizi zina kila right ya kufundisha masomo wanayotaka na kuchagua wanafunzi kutokana na qualifications zinazotakiwa.
Nimeona Mwalimu Kichuguu akigusia shule za kiislaam, lakini alichoshindwa kuelewa ni kwamba hata waislaam wanaona hivyo hivyo pamoja na kwamba wanalazimika kusoma shule za Kikristu. Shule zote zaKikristu zinawataka wanafunzi wake wabadilishe dini, nimeona hadi NGos zikitumia dini kutoa elimu au misaada..Hata huku Ulaya zipo shule za Kikatoliki ambazo hazipokei Muislaam na tunakubali kwa sababu hata wao hii ni misaada wanayopokea ikija na masharti.

Shule za Kikristu zinazofundisha Biblia haziwezi kumpokea Muislaam kuingia hapo kuchukua masomo ya Bible hata kama wanafundisha masomomengineyo, vile vile shule ya Kikristu haiwezi kumchukua mwalimu Muislaam kufundisha ikiwa wapo walimu Wakristu wenye uwezo sawa na huyo mwalimu. Hii ni human nature, we chose to differ na ndipo tunapojenga matabaka. Private schools ni biashara ama misaada ambayo huja na masharti, JK hawezi kuingilia private business ambazo zimelenga kufundisha dini kwa walengwa unless shule hizi zinapata subsidy.

7. Miiko na Maadili ya Viongozi - Baada ya anguko la Azimio la Arusha, hakuna kiongozi hata mmoja anakubaliana na dhana hii ya kuweka miiko kwa viongozi wa serikali hasa ktk kuwa na kofia mbili au kujitajirisha. Hakuna kiongozi yeyote anayeweza kuelewa logic ya kuweka miiko wakati kila Mtanzania anaruhusiwa kuchuma. Swala la conflict of interest halina Uzito kwao woote na JK hawezi kuzua sababu za kuchukua hatua hii ambayo haipokelewi na kamati zote za chama pamoja na viongozi wenzake.

Hata hivyo JK alishasema viongozi wote wanaotaka kufanya biashara wapishe Uongozi, lakini hakuna sheria iliyotungwa bungeni kurudisha miiko na maadili hivyo hadi sasa hivi tunasheria tu ya kukabiriana na Ufisadi unapotokea lakini hatuna miiko wala maadili yake Kitaifa..Kifupi hatuna kinga ila tumeweka dawa zisizoweza kuponyesha ili mradi tunalo kabati lamadawa..

8. Ukosefu wa Maji na utunzaji Mazingira - Hili ni tatizo liinalotokana na Kizazi, maadam tumeshindwa kuondokana na adui wetu watatu -Umaskini, Ujinga na Maradhi hadi nafsi zetu zimekuwa immune ni vigumu sana kwa kiongozi kufikiria umuhimu wa mazingira zaidi ya FEDHA.. Maskini yeyote, mjinga yeyote na mgonjwa yeyote huwa hawezi kuona mbali ya urefu wa matatizo yake na FEDHA ndio huwa dua yake kila siku kujaaliwa Utajiri ili aondokane na adha hizi. Anachokifanya JK ni fikra zile zile za Kimaskini kwamba fedha ndio pekee itakuwa msingi wa kuondokana na madhara haya.

9. Pengo kati ya Matajiri na Maskini - Huwezi kuondoa pengo baina ya maskini na Matajiri pasipo kukubali itikadi inayowezesha uuwiano huu kutokea...itikadi ya CCM haikubaliani na malengo haya kiutendaji..Na kibaya zaidi ni kwamba maadam tulishindwa kuondokana na maadui zetu, ambao ndio mzizi wa fitna zote za pengo hili basi tumekwisha...
Tumaini lilobakia ni kuita wawekezaji ambao hawana fikra za Umaskini wa wananchi isipokuwa wanafikiria tu wataweza vipi kuchuma toka nchini mwetu. Njia pekee ambayo ingetuwezesha kimsingi kupunguza pengo baina ya maskini na matajiri ni kwanza kurudi nyuma na kuthibiti maadui zetu, kisha sisi wenyewe kukubali Ukiukaji wa HAKI za BINADAMU katika AJIRA, kuondokanana fikra za Ubwana na uvivu wa kutegemea misaada toka kwandugu na jamaa waliotajirika wakatuacha nyuma.

Tunapomlalamikia JK kwa kutoongeza mishahara ya kima cha chini nasi pia wananchi tuache kuwa na vijakazi majumbani mwetu tukiwalipa Tsh.30,000 kwa mwezi hali wake zetu wakishinda saloon kusafisha kucha na kupaka poda za urembo. Kuweka walimaji wa jembe la mkoo kwa mishahara duchu hali sisi wenyewe tukishinda mijini kufanya biashara za Ulanguzi na Udalali..Be a farmer ukitaka kuwa mkulima.

Ni wakati sisi Watanzania wenyewe tunatakiwa kujenga working force ambayo ndiyo itatuwezesha kuondokana na pengo hili..Na hatutaweza pasipo kurudi nyuma na kuzungumzia maadui zetu. Ikiwa kila mtu ataweza fanya kazi kwa masaa manane ya uzalishaji kwa kila siku, tukaondoa mila chafu za ubwana na umalkia tulorithi baada ya utumwa.. Tukajituma sisi wenyewe kuliendeleza taifa letu, hili pengo litaondoka laa sivyo hakuna kiongozi hata mmoja anayeweza kuondoa pengo hili kwa fikra na mtaji tulonao.

Asilimia zaidi ya 70 kama sio zaidi ya Watanzania wanafanya kazi ngumu kwa malipo madogo sana na wale wenye kipato kikubwa ni mabwana wanaoendesha utumwa wa karne mpya. Tunapolalamikia wazungu na neo colonisation tufikirie pia kwamba sisi Waafrika tunaendesha utumwa Uliopigwa marufuku majumbani mwetu kila siku kama ni maisha ya kawaida. JK can do very little to change the situation! we're in deep shit!
 
Back
Top Bottom