Hii ndiyo elimu yetu

Jack Beur

JF-Expert Member
Feb 26, 2010
222
246
Kuna asilimia kubwa ya watanzania wenye kuandika maneno haya wakimaanisha yafuatayo
aendi-haendi
ana-hana
una-huna
uduma-huduma
aina-haina
raisi-rahisi
ukumu-hukumu
mana-maana

Je, hii ni "slang" ya kiswahili au ndo matunda ya elimu yetu.
 
Hii ni dalili ya kushuka kwa kiwango cha elimu. Waalimu wa Kiswahili wanapaswa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanatamka na kuandika lugha ipasavyo, lakini kutokana na hali ilivyo sasa naona hata waalimu nao hawajui kinachoendelea.
 
Mkuu, hakika haya makosa yamekuwa sasa ya kawaida kabisa. Wengi tu wana shida hiyo, hata hapa JF. Kuna shida huko shuleni.
 
Hili tatizo pia linasababishwa na lugha zetu za asili. Kuna jamaa zangu wa kanda ya ziwa hilo ni tatizo kubwa saana hata wakati wakizungumza.
 
Kweli,na hichi kitu kinanikera kweli.Ila mara nyingi unajikuta umeanza kama slang halafu unajikuta imekuwa tabia!nimesikitika sana kuona hata kwenye bang! magazine,na michuzi akiwa ndio chief editor. Mwishowe tutaharibu lugha yetu iwe kama kiswahili cha kenya!
 
Sidhani kama ni 'slang' hii ni kutofundishwa matumizi sahihi ya lugha.
Nakumbuka hata wakati nikisoma shule ya msingi mama yangu
alikuwa akinisahihisha matamshi. Tulikuwa tuna lazimishwa kusoma kile
kitabu kinachoitwa "soma kwa hatua" Ni bahati niliweza kusisitiziwa
msingi mzuri nyumbani. Lakini kuna ambao aidha hawakupata mwalimu
mzuri au msimamizi aliye fuatilia elimu yao nyumbani.
 
Una bahati mkuu wengine kwetu haikuwa hivyo,..Nina bonge la kithembe yaani omba mungu usinikute,.
Hata hivyo kithembe au kigugumizi,au wagonjwa wa stroke wanaoshindwa kuongea vizuri na hata mabubu matatizo yao husaihishwa na mtaalam aitwaye SPEECH THerapist na huyo bongo hatuna ,...na huchukuliwa kama tatizo la kawaida tu,..wanachojali walimu au mzazi ujue kusoma na kuandika mengine DUNIA itakufunza,...
 
Back
Top Bottom