Hii ndiyo CV ya Dk. Hadji Hussein Mponda

So, mi sishangai kuwa Dr. M-ponda mawe kuwa mbumbumbu ndo bongo yetu hiyo
Pale Elimu ndo upuuzi mtupu,sijui ilikuaje.. bora hata angekewa Sofia Chui wasomi wetu wangepata mipasho ya taarabu, jamani msifanye mchezo na elimu jamani watoto wetu wanataabika
 
tumevamiwa tena jamani, angalieni kaja lini hapa




Hivyo April 2010 ndio umevamiwaa!! Eti nikweli kuwa umwanachama wa BAVICHAA, nawe ukiwa mmoja wa wale walioletwa hapa na kuambiwa kuwa huu ni mtandao wenu? Basi fahamu, tutabanana humuhumu!
 
huyu jamaa ameingia kwenye health sector juzi tu, wizara ya afya ni ngumu sana kuiongoza kama hauna background ya medicine. Public health huwa wanaenda kusoma vilaza unachukua miezi 6 tu una master yako mkononi.
 
CV inaonyesha si Daktari wa Binadamu kwa kuwa hajawahi kusomea udaktari wa binadamu (Doctor of medicine) bali daktari wa afya ya Jamii (Public Health), Kwa hiyo huyu jamaa hawezi kutatua matatizo ya madaktari.
 
Kwa Tanzania uwaziri na vyeo vingine vya kuteuliwa (ikiwamo ubungo wa viti maalumu eg.Vi- Kama taa) ni kulipa fadhila hali imekuwa dhahiri awamu hii ya 4
1. ngelejaaa ni fadhila kawekwa na Rosti-tamu(kumbuka alikuwa kule VO DA ambako ROSTI TAMU ana hisa kibao
2. kawa-mbwa ni binamu kabisaa wa K. J
3. Hawa Vurugu yeye ni ndugu wa Mama namba 1
4. Sophia Chui ilikuwa chakula ya K. J na mzee kitwana Kondoo allikula
5.Luku-vipi ni shosti wa siku nyingi wa KJ toka (UVCCM)
6.Si-6, Makufuli, Mwa-ndoo-syaa(wamewekwa kupotezea tu)

Mkuu ubarikiwe sana leo nimecheka majina yako haya .Ama kweli JF ina vichwa chako mwisho
 
Wampe Hiyo Wizara Faustine Ndugulile... Muone atakavyoibadilisha hiyo Wizara... Siipendi CCM

Lakini Dr. Faustine will make a change and not this Dr. Mponda from Mzumbe
 
Naomba tuongee ukweli hapa sasa hapa JF. Tatizo la matatizo ya hii nchi ni mfumo. Kinachotokea ni kwamba viongozi wanataka kuishi kwa mfumo wa kurithi kutoka kwenye historia ya enzi ya CCM chama kimoja. Viongozi wengi hasa walio mawaziri wanatoka kwenye historia ya labda baba likuaga waziri, au alishakuaga mbunge miaka kadhaa iliyopita, au alishashika nyadhifa serikalini chini ya uongozi wa CCM. Sasa tukimchukulia mfano huyu Haji Mponda, kwangu mimi ni mtu ninaye mfahamu na ni mtendaji mzuri sana sana. Hajawi hata siku moja kushika nyadhifa yeyote serikalini au kisisasa kabla ya uchaguzi wa 2010 na kwa maana hiyo hayuko polluted kwautawala wa kihistoria. Sasa, ni lazima tutambue kwamba ni vigumu sana kwa mtu anayetoka nje ya mduara wa watu waliozoea kuishi ndani ya utawala wa kihistoria, na wanaotaka kulonda maslahi yao na ya vizazi vyao, kuleta mabadiliko. Anachokosa Dr. Haji Mponda ni support ya watu walio lelewa nje ya mfumo wa kihistoria ili kuleta mabadiliko. Ikiwa kama watu wengi ambao hawakuweko katika serikali zilizopita, na sio product ya viongozi waliopita, wataingizwa kuiongoza serikali, kwa kweli mabadiliko tutayaona. Kwa hali ilivyo kwa sasa ni vigumu sana kwa damu mpya kuleta mabadiliko. Kwa kuongezea tu, ni kwamba wizara ya afya haihitaji daktari wa binadamu kuwa waziri wala katibu mkuu. Nafasi hizi ni za kisera zaidi, hivyo zinahitaji economists, au politicians wanaoelewa uundaji na utekelezaji wa sera za afya. Na kwa kumalizia tu, Dr. Haji Mponda amesoma London School of Hygiene and Tropical Medicine ambacho ni chuo bora kwa Public Health na Health policy. Najiamini kusema kwamba sina wasi wasi na utendaji wa Dr. Haji Mponda, ila tu kuna umuhimu wa kubadilisha mfumo wa uongozi na kuondoka kwenye mfumo wa uongozi wa mazoea na kuingiza damu mpya kwa wingi.
 
mwenye hii education background hapa chini anaitwa jakaya mrisho kikwete.
1958-1961msoga primary school
1962-1965lugoba midle school
1966-1969kibaha secondary school
1970-1971tanga secondary school
1972-1975udsm (ba economics)
1976-1977military training at tanzania military academy at monduli
1983-1984military leadership training


baba collins anadai kwamba jamaa mwenye education background ya hapo juu, amesoma darasa moja na jamaa mwenye education background hapa chini. Mwenye education background ya hapa chini anaitwa hadji mponda!!!
1967-1970manda chini primary school
1971-1973nawenge primary school
1974-1977minaki secondary school ( o-level)
1978-1980tosamaganga secondary school (a-level)
1984-1987mzumbe (advanced diploma)
2003-2004london-masterz
2007-2010london-phd.


nimeamini kwamba jf is never boring!!!

umepindisha......mtoa hoja kasema kuna mtu amemkuta kule ngorongoro na sio huyu mponda........hebu soma vizuri post yake
 
Picha+no+1.JPG
 
Naomba tuongee ukweli hapa sasa hapa JF. Tatizo la matatizo ya hii nchi ni mfumo. Kinachotokea ni kwamba viongozi wanataka kuishi kwa mfumo wa kurithi kutoka kwenye historia ya enzi ya CCM chama kimoja. Viongozi wengi hasa walio mawaziri wanatoka kwenye historia ya labda baba likuaga waziri, au alishakuaga mbunge miaka kadhaa iliyopita, au alishashika nyadhifa serikalini chini ya uongozi wa CCM. Sasa tukimchukulia mfano huyu Haji Mponda, kwangu mimi ni mtu ninaye mfahamu na ni mtendaji mzuri sana sana.

Yote uliyoyasema ni sahihi, kama kuna CV iliyokaa vizuri basi ni ya Dr Hussein Haji Mponda. Ameandaliwa kiuongozi kwa Stashahada ya juu kutoka hapo Mzumbe ambacho ndicho kinachotambulika kitaifa na nje ya nchi ktk fani ya uongozi. Kwenye fani ya afya ya jamiii ana shahada ya Uzalmili na Shahada ya Uzamivu kutoka Hapo London School of Tropical Hygeine, moja kati ya vyuo bora kabisa ktk fani ya public health. Sasa wnao doubt CV hii watuambie walitaka ionyeshe amesoma wapi? Kwa uzoefu amekuwa lead reseacher kwenye eneo la malaria kama mfanyakazi wa Ifakara Healtj Institute. Kwa taarifa ya wasiojua Ifakara Health Institute ilnatambulika kimataifa kama Taasisi ya utafiti wa malaria ikishirikiana na Swiss Tropical Institute & Research Centre.

Kiutendaji ktk wizara yeye si mtendaji bali ni msimamizi wa sera. Inawezekana tatizo ni la mfumo na halitokani na Dr Haji Mponda as an individual. Tunapo discuss kwa kwa kuponda kila tuna poteza malengo.
 
Kwa Tanzania uwaziri na vyeo vingine vya kuteuliwa (ikiwamo ubungo wa viti maalumu eg.Vi- Kama taa) ni kulipa fadhila hali imekuwa dhahiri awamu hii ya 4
1. ngelejaaa ni fadhila kawekwa na Rosti-tamu(kumbuka alikuwa kule VO DA ambako ROSTI TAMU ana hisa kibao
2. kawa-mbwa ni binamu kabisaa wa K. J
3. Hawa Vurugu yeye ni ndugu wa Mama namba 1
4. Sophia Chui ilikuwa chakula ya K. J na mzee kitwana Kondoo allikula
5.Luku-vipi ni shosti wa siku nyingi wa KJ toka (UVCCM)
6.Si-6, Makufuli, Mwa-ndoo-syaa(wamewekwa kupotezea tu)

Penye Red
umenimaliza kwa kicheko
teh teh te
 
Hata hivyo anajua mambo ya ufya kwa ujumla, mbona wizara yake inayumba sana hasa hili swala la madaktari? Kwanini asijiuzulu?
 
Dr Hadji Hussein Mponda profile.


First Name: Dr. Hadji
Middle Name: Hussein
... Last Name: Mponda
Member Type: Constituency Member
Constituent: Ulanga Magharibi
Political Party: CCM
Office Location: P.O. Box 9083, Dar Es Salaam
Office Phone: +255 783 003 635
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail: hmponda@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 27 September 1958


EDUCATIONS
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
Manda Chini Primary School Primary Education 1967 1970 PRIMARY
Nawenge Primary School Primary Education 1971 1973 PRIMARY
Minaki Secondary School O-Level Education 1974 1977 SECONDARY
Tosamaganga Secondary School A - Level Education 1978 1980 HIGH SCHOOL
Mzumbe University Business Management 1984 1987 ADV DIPLOMA
London Univeristy Public Health 2003 2004 MASTERS DEGREE
Mzumbe University Material Management - GRADUATE
London Univeristy Public Health 2007 2010 PHD


Nimekuwa najiuliza sana kuhusu huyu waziri wa afya na jinsi anavyohandle issues za wizara yake hasa mgomo wa madaktari nikaishia kupata CV yake hii.

Nadhani kuna haja wizara kuwa zinaongozwa na watu wenye taaluma husika pengine inaweza kusaidia kuondoa mitafaruku isiyo ya lazima na adha zinazowakumba wananchi......

I think he is the righ person (see red) for that Ministry. The problem is that when come the issue of money, that is beyond his power to decide....Doctors are claiming for more pay, the money which is either released by treaury nor budgeted and approved by the Parliament

 
Nimepata kukutana na mtu wa type ya JK ambaye pia ni conservator wa Ngorongoro,inasemekana walisoma darasa moja hawa jamaa.

Swali langu ni je,mbona jamaa wengi sana waliosoma na Jk wana tabia zinazoendana? Au ilikuwa ni ka generation kalipita ka watu wa aina hiyo?

Huyo conservator unamaanisha chief conservator au?

Bernard Murunya au?
 
JK amedanganywa elimu ya Mponda

Joji Poji kama JK kadanganywa tupe ushahidi kwa vile kuna watu humu kwenye JF wamesoma naye. Kuliko ku generalise tu nakushauri utoe evidence kama hajasoma vyuo hivyo.
 
Dr Hadji Hussein Mponda profile.

London Univeristy Public Health 2007 2010 PHD
......

Hongera sana Mh.Mponda;
Ila suala la madaktari mkomalie Mh.Pinda mlisawazishe maana jina lako ndo linaharibika sio la Mh.Pinda.
images


Kumbuka ule usemi......
 
Ok! ni kazi kweli Tz, We nenda hata upande wa Sector ya Elimu tu utawakuta Akina Mlugo ni kazi kwelikweli. Sijui kama ndo Tz tunayoitaka hii. Hata bosi wao ni Kazi ileile.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom