Wadau kama kuna mtu mwenye cv ya waziri wa afya tafadhari atuwekee ili tuweze kujua, kwa kuwa kuna tetesi kuwa Mh. rais amedanganywa juu ya elimu ya huyu mh mponda
Nimefanya naye Kazi. Alianza na Adv. Diploma huko Mzumbe. Nafikiri alifanya Kazi Mbeya kabla ya kuja Ifakara ambako aliajiriwa kama Social Marketing Research Officer kwenye masuala ya matumizi ya neti za kuzuia mbu wa malaria. Alifanya kazi kwa juduhi kubwa na akafanikiwa kupata scholaship ya kwenda kufanya Masters chuo kikuu cha London (School of Hygiene and Tropical Medicine). Hiki chuo kinaheshimika sana kwenye masuala ya Afya na hasa magonjwa ya kitropiki. Nafikiri alimaliza Masters yake miaka ya 2004/5. Akabahatika kupata mradi wa watu wa UNICEF kwenye masuala hayo hayo ya kusambaza neti. Akatumia zile data kufanya PhD yake kwenye chuo hicho hicho za London na aliimaliza miezi michache kabla ya Kampeni za uchaguzi nchini Tanzania. Hivyo tunaweza kusema kwamba kwenye afya ameingia kama mtafiti na siyo daktari wa binadamu. Ni mchapa kazi mazuri ila kama mwanasiasa siwezi kusema maana sikuwahi hata kusikia opinion zake kuhusu masuala ya siasa!
ni dhahiri jamaa ameungaunga,..lakini bongo lolote lawezekana!!
hivi huyu kumbe hana hata MD degree !! na watetezi msituletee habari za LSHTM hapa!
Wadau kama kuna mtu mwenye cv ya waziri wa afya tafadhari atuwekee ili tuweze kujua, kwa kuwa kuna tetesi kuwa Mh. rais amedanganywa juu ya elimu ya huyu mh mponda
nimepata kukutana na mtu wa type ya jk ambaye pia ni conservator wa ngorongoro,inasemekana walisoma darasa moja hawa jamaa.
swali langu ni je,mbona jamaa wengi sana waliosoma na jk wana tabia zinazoendana? au ilikuwa ni ka generation kalipita ka watu wa aina hiyo?