Elections 2010 Hii ndiyo ccm na viongozi tunayoitegemea ituongozei!!!!!!!!!

Jan 16, 2007
721
176
Bashe amuumbua Chiligati

• ASEMA CCM HAIKUMTUMA KUMVUA NYADHIFA ZAKE

na Kulwa Karedia




SIKU mbili baada ya serikali kumtangaza aliyekuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Hussein Bashe, kuwa ni raia halali wa Tanzania, ameibuka na kumtupia lawama nzito Katibu wa Itikadi na Uenezi, Kapteni John Chiligati, kwa kumdhalilisha na kulitangazia taifa habari za uongo kuwa yeye si raia.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, katika mahojiano maalumu mjini Dar es Salaam jana, Bashe alisema Chiligati hakuwa na mamlaka ya kisheria ya kumtangaza kuwa yeye si raia na kumvua nyadhifa anazoshikilia ndani ya CCM.

“Napenda kuwaambia Watanzania kuwa kitendo cha Waziri Chiligati kunitangaza hadharani hakikuwa cha kiungwana, hana mamlaka ya kusema mimi si raia… amenidhalilisha mimi na familia yangu.

“Tatizo langu kubwa ni moja, pale ambapo kiongozi mkubwa wa taifa, (Katibu wa Uenezi) ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, anaelewa sheria inasemaje, anaibuka na kuongea vitu vya ajabu ambavyo havijajadiliwa na vikao husika vya chama,” alisema Bashe.

Alisema Chiligati alipaswa kuishia kwa kusema CCM haijamteua Bashe kwa sababu kadhaa na kwamba zinafanyiwa uchunguzi.

Alibainisha kuwa Chiligati aliongea mambo mabaya yakiwemo ya kwake ya kuvuliwa nyadhifa za chama, kuishi nchini kwa mazoea na wazazi walihamia Tanzania katikati ya miaka ya 1960.

“Nakwambia kaka ni hatari kwa kiongozi kuzungumzia masuala ya mtu binafsi… napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa sina kinyongo chochote na haya yote.

“Maneno yaliyotolewa na Chiligati ni ya kwake binafsi kwa vile aliongea mambo ya ajabu ambayo yanadhalisha familia yangu, mambo haya yahakujadiliwa na vikao husika vya chama,” alisema Bashe.

Alisema ili chama kimfukuze na kumvua uanachama kuna vikao husika ambavyo hukaa na kupitia kwa kina malalamiko yote yaliyowasilishwa.

“Ninamshangaza Chiligati iweje yeye abwatuke? Anapaswa ajifunze kutovunja sheria za nchi, sisi ni chama tawala, viongozi wanatakiwa kuheshimu utawala wa sheria na kauli zao wanazotoa,” alisema Bashe.

Alisema pamoja na kauli hizo, Chiligati bado hakuwa na mamlaka yoyote ya kumfukuza nchini na kumrudisha Somalia ambako anadai kuwa ndiko alikozaliwa.

“Hebu fikiria mpaka hapa tulipofika CCM haijasema mimi siyo mwanachama, hakuna kikao kilichonivua uanachama, nachukua fursa hii kuwaomba wana CCM wote pamoja na wale wa Jimbo langu la Nzega waelewe kura 14,000 walizonipa nina imani nazo, naziheshimu, nathamini sana, wategemee ushiriki wangu katika shughuli zote za maendeleo kama ilivyokuwa hapo awali,” alisema.

Alisema kuwa ahadi zake zote azoziahidi atazitekeleza kama alivyoahidi wakati wa kampeni.

Alisema kauli ya Chiligati, ilitokana na majungu yaliyotengenezwa na viongozi wa CCM mkoani Tabora ambao anawatambua kwa majina na nyadhifa zao.

“Nilitengenezewa majungu na viongozi wa CCM Mkoa wa Tabora, nawajua kwa majina vizuri… nakuhakikishia kwamba majungu haya hayakutengenezwa na Kamati ya Maadili, Mkutano Mkuu au Halmashauri Kuu (NEC),
“NI wana CCM walioko Tabora, wengine ni viongozi wetu wakishirikiana na watu niliowashinda kwenye uchaguzi, walichukua majungu haya na kuyapeleka kwenye Kamati Kuu ili nisulubiwe,” alisema Bashe.

Alisema yeye binafsi alielewa vizuri uamuzi wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ambao aliupokea ili kunusuru chama kupoteza jimbo kwenda upinzani.

“Unajua CCM kumteua mtu au kutomteua ni utaratibu wa chama, hata kama ningekuwa raia inawezekana nisingeteuliwa na chama, wapo waliachwa kwa sababu ya tuhuma mbalimbali zikiwemo zinazochunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), sina kinyongo, nawaomba wana Nzega tukubali, ni uamuzi halali,” alisema.

Aliwaonya viongozi wa CCM Mkoa wa Tabora kuacha kufanya kazi kwa majungu kwani alisema kufanya hivyo kunaweza kuhatarisha ushindi wa viti vya ubunge na kuwataka watangaze Ilani ya chama kama inavyoelekeza.

“Nawaomba viongozi wa CCM Mkoa wa Tabora waache majungu na fitina, mkoa huu umekuwa na viongozi wakubwa, una historia ya kuleta uhuru wa taifa hili, lakini ni mkoa ulio nyuma kimaendeleo… lazima sasa tuamke na si muda wa kukalia majungu na fitina,” alisema Bashe.

Alisema kamwe CCM haiwezi kushinda Jimbo la Nzega kwa kuendeleza vitisho kwa viongozi wa matawi, mashina na kata eti kwa sababu walimuunga mkono wakati wa mchakato wa kura za maoni.

Alisema yuko tayari kama akiombwa na chama chake kwenda kusaidia harakati za kampeni zinazoendelea kukinadi kwa wananchi ili kiubuke na ushindi.
 
Back
Top Bottom