Hii ndio kazi unayoifanya

Sipo

JF-Expert Member
Jul 25, 2008
2,139
91
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani (WHO) ya mwaka 2005. Kazi husababisha maumivu na vifo kwa kiwango kikubwa kuliko matumizi ya madwa ya kulevya au ulevi wa pombe vikijumlishwa kwa pamoja.

Nalo gazeti la The Guardian la Uingereza la mwezi May 2005 liliripoti kwamba kila mwaka zaidi ya watu milioni mbili duniani kote hufa kutokana na majeraha au magonjwa yanayosababishwa na kazi

Sababu kubwa zilizotolewa ni vumbi, kemikali, kelele, miale au mionzi mbalimbali ambayo husababisha kansa, magonjwa yakupooza na kiharusi. Pia kuna uchovu wa kupindukia.

Mwanasaikolojia Steven Berglas anasema woga, wasiwasi, mfadhaiko na sononi ni mambo ambayo humpata mtu kwasababu ya kunaswa na kazi yake kiasi kwamba hawezi tena kujinasua.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom