Hii nayo vipi-wasaidie majibu

Jul 14, 2009
86
19
Jamaa mmoja alimiliki miche ya sabuni za kufulia mingi sana. Akafikiria afanye nini kutumia miche hiyo akagundua kiasi cha sabuni aliyonayo ingetosha uwekezaji wa sehemu ya kutoa huduma ya ufuaji nguo na vitu vya aina hiyo ila yeye hakuwa na mitambo ya ufuaji na pengine mtaji wa awali na kasi cha kuwaliwapa wafanyakazi. Mara akatokea jamaa mwingine, kupitia kwa baadhi ya watoto wa jamaa mwenye sabuni tena aliowasomesha kwa gharama kubwa, akasema yeye ataleta mitambo na chochote kile cha kuanzishia biashara ile ila makubaliano ni kwamba angemlipa jamaa mwenye sabuni pale atakapoanza kupata faida ya uwekezaji. Ebwana ukatumika mche wa sabuni wa kwanza mpaka karibu na wa mwisho jamaa akisema atengenezi faida japo anaendeleza ufuaji akimpoza jamaa mwenye sabuni kwa vijisenti kidogo tu tena baada ya malalamiko sana kutoka kwa familia nzima.

Wengine wakajiuliza;

  1. Je ni kweli muwekezaji hapati faida na anaendelea na biashara?
  2. Haikuwezekana kwa mwenye sabuni kufanya sabuni alizonazo kuwa ni sehemu ya uwekezaji na hivyo mapato ya uwekezaji kugawanywa kwa uhuwiano kati ya aliyeleta vifaa na mwenye sabuni?
  3. Hawa watoto waliokubali kufanya makubaliano hayo hawakujua kitatokea nini au ni makusudi tu kuna maslahi binafsi
  4. Na je kuna kosa limefanyika? Kama lipo kifanyike nini sasa?
 
This is very simple!

Just consider the situation in Tanzania today. Tuna madini, misitu, mbuga za wanyama, milima etc etc...lakini ndo hivyo, hatuwezi kuvitumia kugenerate faida za kutuondoa kutoka kwenye umasikini!

Wanakuja wageni wazungu, wanaojidai wanajua kuzigema mali hizi. Wanatumikisha Watanzania na kuwaondoa kwenye makazi yao halali na kuwachomea majumba, huku wakipata back-up ya serikali, na wananchi hao wanaitwa wahamiaji haramu toka nchi ya Kenya!

Je hapa kuna kosa lililofanyika?

Jibu ni ndiyo! Kuna watu wachache wenye kiu na uroho wa Maslahi binafsi, wakitumia dhamana ya vyeo vyao kunenepesha makalio yao!

Poor we!

Mungu ibariki Tanzania
 
Sasa mkuu PakaJ,
Kwa makosa kama haya ambayo kimsingi yamegundulika kifanyike nini kwenye chochote kilichofanyika kimakosa? Au ndiyo mimi au wewe uendelee kulalamika tu mpaka mwisho wa ulimwengu (kama kweli upo)?
 
Back
Top Bottom