Hii nayo kali.. True story

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
4,963
15,239
Jamaa ametoka home anaenda zake mjini. Sasa kawaida amezoea kuweka simu yake mfukoni upade wa kulia. Mara akiwa kwenye daladala, akapanda abiria mmoja yuko rafu rafu kama kibaka vile na kwenda kukaa siti moja na jamaa. Jamaa kuona vile akahamua aihamishie simu yake mfuko wa kushoto, safari ikaendelea. Kufika mjini, yule kijana rafu akashuka, akavuka barabara, akasimamisha daladala nyingine akapanda. Huku nyuma yule jamaa aliebaki kwenye siti akapapasa mfukoni kutaka kutoa simu, hola! Simu haipo. Akapayuka 'Mungu wangu, nimeshaibiwa'! Naye akashuka, akavuka barabara, akingia kwene daladala lile lile liloingia yule kijana. Sasa akawa anafikiria alianzisheje? Apige kelele za mwizi au amkwide tu yule kijana aanze kumpa kichapo? Wakati anaendelea kujiuliza maswali, huku daladala likiendelea na safari, hasira tele, mara simu yake ikaanza kuita. Jamaa nusu azimie. Mfuko wa kushoto!
 
Kuna imani fulani hivi kwamba kitu ukikiweka ama kukishika upande wa kushoto wakati unakitafuta hauwezi kugundua haraka.

Kuna mzee aliweka shoka upande wa bega la kushoto akiwa shamba, alitafuta mpaka mkewe akamfata shamba akauliza kulkoni akasema natafuta shoka, kumbe ameliweka bega la kushoto
 
Mi nawaza ingekuaje simu isingeita? Yule dogo si wangemuua bure? Au ndio wamemaliza kumpiga yuko hoi mara simu inaita.. Jamaa angekua ktk hali gani?
 
Bahati yake hakulianzisha kwa kijana sababu mambo yangemgeukia mwenyewe!!!
 
hii ipo ni yaukwel kabisa na mara kibao inatokea tatzo mnazdsha mawazo na huku mnaugonjwa wa kusahau ila mnaakil za kukumbuka mmeibiwa
 
nakumbuka mdingi miaka hiyo kanunua samaki wabichi kasahau kwenye buti mpaka walipoanza kunuka ndio kastuka kama kuna kitu kinanuka humu,kwenda check fish ndio akakumbuka alaaa nilinunua wiki iliopita hawa samaki
siku ingine karudi safari ya mbali akasahau begi ndani ya basi kachukua zawadi tu alizonunua njiani
karudi hm mikono mitupu,siku hiyo mpaka alipata ajali alipokuwa akiwahi kufuata begi lenye viwalo vyake.
 
hahahahahah hii kiboko,walikuwa wangapi lakini :coffee:
 
hahahahahah hii kiboko,walikuwa wangapi lakini :coffee:

walikuwa kibao,yaani hivi ni visa viwili tu nilivyokumbuka,jamaa alikuwa ni msahaulifu aliyebobea,sometime naona kaniambukiza maana huwa nasahau ninii na kudhani nanihii.
 
walikuwa kibao,yaani hivi ni visa viwili tu nilivyokumbuka,jamaa alikuwa ni msahaulifu aliyebobea,sometime naona kaniambukiza maana huwa nasahau ninii na kudhani nanihii.

hahahahahaha kuwa makini usahaulifu mbaya,nilikuwa namaanisha mzee alikuwa anpiga yale mambo yetu au usahaulifu tu:coffee:
 
nakumbuka mdingi miaka hiyo kanunua samaki wabichi kasahau kwenye buti mpaka walipoanza kunuka ndio kastuka kama kuna kitu kinanuka humu,kwenda check fish ndio akakumbuka alaaa nilinunua wiki iliopita hawa samaki
siku ingine karudi safari ya mbali akasahau begi ndani ya basi kachukua zawadi tu alizonunua njiani
karudi hm mikono mitupu,siku hiyo mpaka alipata ajali alipokuwa akiwahi kufuata begi lenye viwalo vyake.
Hahahahaaah! Hii nayo imetulia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom