Hii Mitandao ya Jamii ina mambo!

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Miezi 2 iliyopita rafiki yangu mmoja alinipa taarifa juu ya mahusiano na mdada mmoja aliyempata kwa njia ya Mtandao mmojawapo wa kijamii, uitwao face book. Kwa maelezo yake, amekuwa akiwasiliana na huyu dada pasipo kuonana naye kwa takriban mwaka na nusu sasa. Uhusiano wao ulikuwa mzuri mno kiasi hata cha kufikia kupeana emails, majina yao halisi na picha ambazo kimsingi zilionyesha uhalisia wa mawasiliano yao!

Kilichokuwa kikimsibu huyu jamaa ni kuwa dada huyo alikuwa akikataa kata kata kuonana na huyo kaka, ingawa maelezo ya kuchat ya kila siku through emails and yahoo messenger na SMS (alitoa namba ambayo ilikuwa blocked kwenye voice call) yalionyesha dada kumpenda kaka kupita maelezo.

Kaka amekuwa akijitahidi kutuma vocha na vijisenti kupitia MPesa kwa ajili ya matumizi kwa takriban mwaka sasa akiamini kuwa ipo siku dada huyo angemkubali maana kuna kipindi rafiki yake mwingine aliwahi kuoa kupitia face book.
Juzi kapokea sms kutoka kwa huyo dada, kuwa yeye ni mwanaume na siyo dada na aliamua kumlia pesa kwa kipindi chote hicho na anamshauri atafute mke badala ya kuendekeza online dating!

Swali: Hivi kweli kuna midume inayojifanya midada kwenye mtandao ya kijamii? Na kwanini wanafikia kufanya haya mambo? Na ni kweli dada huyo ni mwanaume au kamchoka tu huyo kaka na kumtumia msg hiyo kwa lengo la kumkatisha tamaa?

Wenu,
HP
 
anything can happen, hii ndo dunia yetu.
Si hata hapa kuna mtu kaliwa laki mbili na dume?
 
Kuna kijana mmoja harusi yake ilifanyika mwezi wa nane, anasema naye pia wife wake alimpata thru face book, Sikulijua hilo, loh!
 
Unajua through internet lazima uwe mwerevu sana,usiamini mtu,any thing may happen kwa sababu hakuna physical interact,
 
Mbona huyo ndg yako ni zuzu hivo ? Yeye alikubalije kuuziwa mbuzi kwenye gunia ?
 
alipigwa na mistari iloshiba
yenye vina na mizani
beti za kutosha

weee laki mbili kitu gani
pesa makaratasi
hasara roho
acha mtoto akatumie
kumbe dume jenzie

Mbona huyo ndg yako ni zuzu hivo ? Yeye alikubalije kuuziwa mbuzi kwenye gunia ?
 
Yaani wewe unadhani member wote wenye username zinazoishia na neno lady na wenye Avatar za kike hapa JF ni wanawake? kuwa makini na internet, itumie Internet kwa ajili ya kujielimisha na kuongeza maarifa na kujiburidisha, Yaani mademu wote hawa kitaa mtu unashindwa kupata mchuchu?
Ok mwambie rafiki yako aingie kwenye link hii atapata demu anaemtaka lakini hii ni kampuni na huduma hii inalipiwa. DATING SERVICE, COUNSELING SERVICE, OUT OF BUSINESS!
 
Mpe pole huyo kaka mwambie hayo mapenzi ya FB ni sawa na kuoga vumba, unweza kuekewa picha ya mwanake au ya mwanaume ukasema umepata kumbe umepatwa,chamsingi awachane na huyo mtu kama nimwanamme kweli na alikua anajifanya yeye mwanamke basi walisha mpitia wanaume wa mjini ndio mana anakua na ujinga kama huo,mwanamme alotimia hafanyi hayo hata siku moja...
 
Yaani wewe unadhani member wote wenye username zinazoishia na neno lady na wenye Avatar za kike hapa JF ni wanawake? kuwa makini na internet, itumie Internet kwa ajili ya kujielimisha na kuongeza maarifa na kujiburidisha, Yaani mademu wote hawa kitaa mtu unashindwa kupata mchuchu?
Ok mwambie rafiki yako aingie kwenye link hii atapata demu anaemtaka lakini hii ni kampuni na huduma hii inalipiwa. DATING SERVICE, COUNSELING SERVICE, OUT OF BUSINESS!

[FONT=Verdana,Arial,Helvetica,sans-serif]DATING SERVICE, COUNSELING SERVICE, OUT OF BUSINESS![/FONT]
spacer.gif

This site The Web
[FONT=Verdana,Arial,Helvetica,sans-serif] Due to the Sad Death of LAURELEE, we are forced to close our business.

If you are interested in purchasing this WEBSITE, please make any legitimate offer in writing to
us at Laurelee@roadrunner.com
[/FONT]
[FONT=Verdana,Arial,Helvetica,sans-serif] www.FRIENDFINDERS.COM is no longer in business.

The WEBSITE IS UP FOR SALE.
[/FONT]
[FONT=Verdana,Arial,Helvetica,sans-serif][/FONT]​
Laurelee1BW-1.jpg.w300h346.jpg
spacer.gif
spacer.gif

[FONT=Verdana,Arial,Helvetica,sans-serif]

EMAIL US NOW IF YOU ARE INTERESTED IN PURCHASING THIS WEBSITE!

[/FONT]
[FONT=Verdana,Arial,Helvetica,sans-serif]

[/FONT]

spacer.gif

spacer.gif
[FONT=Verdana,Arial,Helvetica,sans-serif]THIS WEBSITE IS FOR SALE-- Email us at LAURELEE@roadrunner.com and make offer[/FONT]
Powered by Register.com
spacer.gif
 
Mjini shule!
Mwambie aendelee tu kumtumia hizo hela labda anaweza kumpata siku moja amkameruni!
 
Mbona huyo ndg yako ni zuzu hivo ? Yeye alikubalije kuuziwa mbuzi kwenye gunia ?
JF watu utumia third part kuzungumzia yaliyowapata, ni wachache wanaoconface kwamba wanachoripoti hapa kinawahusu wao, wewe angalia thread zote utagungua neno rafiki yangu ndio linawakilisha nafsi zao wenyewe.
 
Yaani wewe unadhani member wote wenye username zinazoishia na neno lady na wenye Avatar za kike hapa JF ni wanawake? kuwa makini na internet, itumie Internet kwa ajili ya kujielimisha na kuongeza maarifa na kujiburidisha, Yaani mademu wote hawa kitaa mtu unashindwa kupata mchuchu?
Ok mwambie rafiki yako aingie kwenye link hii atapata demu anaemtaka lakini hii ni kampuni na huduma hii inalipiwa. DATING SERVICE, COUNSELING SERVICE, OUT OF BUSINESS!

ina maana,unalipa kupata date!.khaa,mbona wasichan wengi tu..tusidanganywe na picha za kueditiwa,tuta date na majin
 
Back
Top Bottom