Hii Mifuko ya Hifadhi ya Jamii umefika wakati wa kumjali mteja

njiwamanga

Member
Oct 21, 2010
35
3
Hii mifuko na mingine ya namna hii inatumika kuwanufaisha mafisadi walioianzisha.mnaonaje iwekewe mfumo mzuri uso wa kinyonyaji kwenye katiba mpya?

NAWASILISHA
KANUNI zinazoongoza utumiaji wa Sheria ya Mamlaka ya Mifuko ya Jamii ya Mwaka 2008 zipo tayari na zimeanza kutumika tangu mwaka jana. Lengo la kuunda mamlaka ya mifuko ya jamii kwa mujibu wa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, ni kudhibiti matumizi ya fedha za mifuko hiyo.

Fedha hizo zinatokana na wafanyakazi wa mashirika na Serikali wakijiwekea akiba ya uzeeni. Mamlaka inahakikisha mifuko hiyo inaendeshwa kwa ufanisi kwa kuwanufaisha zaidi wanachama wake.

Sheria hiyo inaunda pia Mahakama ya Hifadhi ya Jamii ili kushughulikia migogoro yoyote ikijitokeza. Mahakama hiyo itakuwa chini ya Jaji wa Mahakama Kuu. Mahakama hii itakuwa ikipitia maamuzi yoyote yenye utata au mgogoro ya Mamlaka ya Mifuko ya Jamii. Itakuwa pia na uwezo wa kusikiliza rufaa za masuala ya hifadhi ya jamii kutoka katika mamlaka.

Mamlaka ya Hifadhi ya Mifuko ya Jamii imeundwa wakati kuna tuhuma kadhaa za ufisadi katika mifuko ya hifadhi ya jamii ya mashirika ya umma na hata serikali za mitaa kama vile NSSF, PPF na LAPF ambazo hata Mdhibibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, amethibitisha kuwepo ufisadi huo ambapo kuna fedha zimekuwa zikichotwa kutoka mifuko hiyo na kuwakopesha watu au makampuni binafsi.

Ndio maana sheria ya udhibiti wa fedha za mifuko hiyo zinazokatwa katika mishahara ya wanachama wake, imehakikisha mameneja au wakurugenzi hawatakuwa na maamuzi ya pekee yao ya uwekezaji kama ilivyozoeleka. Benki Kuu na Bodi ya Mamlaka ya Mifuko itatoa vigezo vya uwekezaji pale inapobidi kufanya hivyo.

Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Ludovick Utouh, imebainisha kwa mfano Mamlaka ya Mfuko wa Hifadhi ya Serikali za Mitaa (LAPF) iliikopesha GK Hotels & Resorts dola 535,000 katika mwaka wa fedha wa 2003|04, ambapo kufikia Juni 30, 2008 deni lilifikia kiasi cha dola 722, 000 wakati kampuni husika ilikuwa inadaiwa pia kodi ya kupanga katika jengo la LAPF dola milioni 1.127.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ameonesha matumizi ya fedha yasiyofaa kwa NSSF ambayo imekuwa ikitumia fedha za wanachama wa mfuko huo kuwalipa wafanyakazi wake bonasi eti kwa kazi nzuri wanayofanya wakati huo ni wajibu wao kwa mujibu wa ajira zao.

NSSF nayo imehusika katika kutoa mikopo na hata misaada ya fedha kwa watu na makampuni binafsi wakiwemo vigogo ndani ya Serikali bila utaratibu wowote kwa vile hakuna sheria iliyokuwa inazuia maamuzi hayo.

Sheria inasema Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mifuko hiyo itakuwa na Mwenyekiti atakayeteuliwa na Rais na wajumbe wafuatao: Msajili wa Hazina, Kamishna wa Kazi, Wawakilishi wawili wa Chama cha Waajiri, Wawakilishi wawili wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, mtaalam mmoja wa masuala ya hifadhi ya jamii na Mkurugenzi Mkuu ambaye hana kura.

Bodi itateua pia mwanasheria mwenye uzoefu wa sio chini ya miaka miwili ili awe Mwanasheria wa Mamlaka na Katibu. Shughuli za Mamlaka kisheria ni pamoja na kuandikisha wasimamizi au mameneja wote wa mifuko, kutembelea na kukagua mara kwa mara utendaji kazi wa mifuko hiyo ikiwemo vitabu vya mahesabu.

Ukiisoma sheria hiyo kwa makini pamoja na vyombo vitakavyoundwa kusimamia utekelezaji wa majukumu yake, utaona ni sheria nzuri sana kama ambavyo tunazo sheria nyingi za namna hiyo. Hii imekuwa ni mtazamo tulionao kwamba sheria yaweza kuweka mambo sawa pale yanapokwama bila kukumbuka kwamba sheria hiyo hutumika endapo waliopewa mamlaka ya kuitumia watatekeleza.

Mfano ni ile Sheria ya Rushwa ya Mwaka 2007 ambayo ina vifungu vya sheria vya kudhibiti masuala mengi ya rushwa ikiwemo hata rushwa ya ngono ambayo uchunguzi na ushahidi wake huwa ni mgumu sana. Hata hivyo, sheria hiyo inayompa madaraka makubwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, inategemea na utashi wa wanaoitumia. Wanaweza kuamua isitumike ipasavyo kwa manufaa yao au ya mtu mwingine yeyote. Yaani sheria yaweza kutumika kifisadi.

Hata mashitaka yakipelekwa mahakamani ikiwemo ushahidi wa kutosha kutolewa, uamuzi wa kumtia hatiani mshitakiwa kwa ushahidi huo ni wa mahakama ambayo ndiyo yenye mamlaka pekee ya kutafsiri sheria. Inaweza kutafsiri sheria vinginevyo kwa manufaa ya mshitakiwa! Hivyo, ili sheria ifanye kazi nzuri, utashi wa maadili kwa wasimamiaji wa sheria hiyo unahitajika zaidi.

Ni maoni yangu kwamba ufisadi unatokana na mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu katika maeneo yote ya kikazi na hata taaluma. Nimewahi kueleza katika safu hii kwamba kila sekta nchini imekumbwa na mmomonyoko wa maadili. Haijalishi ni sekta gani kwani hata kwenye masuala ya dini kuna matatizo kiasi cha kushangaza kama tulivyoona ule upatu wa DECI unaoendelea kuliza watu wengi.

Kwanza, kuundwa kwa mamlaka ya kudhibiti mifuko ya hifadhi ya jamii ni kuongeza urasimu wa kusimamia masuala hayo ambapo wahusika wanaweza nao kuhongwa kwa kupewa mikopo na mifuko husika kama ambavyo imewahi kutokea ambapo Waziri Mkuu na hata Rais waliwahi kunufaika kinyemela na fedha za mifuko hiyo, ingawa baada ya kushtukiwa wakarejesha chap chap.

Pili, watakaoongoza mamlaka hiyo watakuwa wamepimwa vipi kimaadili kwani kama ambavyo imezoeleka ni dhahiri watakuwa ni Watanzania tunaowajua tena wengi wao ni wale waliowahi kuvurunda katika maeneo mengine ingawa wana sifa nzuri za kitaaluma. Nashauri watakaosimamia uendeshaji wa mamlaka hiyo wapewe semina elekezi za maadili na hata kupelekwa katika mafunzo zaidi nje ya nchi ili kuondokana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.

Maana sheria haiwezi kuleta mabadiliko yoyote ya udhibiti wa ufisadi unaofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii. Tunahitaji watendaji wenye maadili mema. Wasioweza kushawishiwa kupinda sheria kwa manufaa yao.
 
Mimi nasikitishwa na hizi hasasi za mifuko ya jamii kwa jinsi zinavyowanyonya wanachama wake na wao kujigawia mishahara minono na kuporomosha maghorofa marefu na kupangisha kwa bei ya juu,ukiangalia pesa za pango ktk maghorofa yote ya mifuko ya hifadhi wanafaidi wakubwa pamoja na wafanyabiashara wakubwa!ila yule anayetumia sehemu ya jasho lake hathaminiwi!

Na hana thamani ktk mifuko hiyo! Zaidi ya kuambiwa mpaka afikishe umri fulani ndo alipwe vijisenti vyake!

Je huo siyo udhalilishaji?ktk nchi za wenzetu mifuko ya jamii inafanya kazi za huduma ya jamii kwa kuzipa kipaumbele sehemu zenye matatizo ya huduma za jamii kama mahosipitali,barabara,maji nk.Ila sasa mifuko hii imekuwa dhalimu hata kwa walala hoi!

Tujulisheni pesa za pango katika wajengo haya zinafanya nini? PPF HOUSE, PPF TOWER, LAPF, NSSF HOUSE ZOTE.

Na michango bado inaendelea kutolewa nakwasasa kodi za pango zinazidi michango ya wanachama! Lakini wanachama wanafaidikaje??
 
imefika sasa wakati wa sisi wanachama tuanze kunufaika na pesa zetu ujinga huu mijitu inakula tuuu haki zetu sie tunaishi kwa shiiiida
 
Basi hata wangeanzisha mifuko yakuwakomboa wanachama wao kwakuwakopesha huku wakikatwa katika mishahara yao kidogokidogo au kuwawekea kama saccos kwa liba ndogo sana kwakuwa yeye anakuwa tayari ni mwanachama!!Lakini wao nikujenga mighorofa hambayo wanachama hawana faida nayo!Hu ni unyonyaji wa hali yajuu kuliko hata ule wamkoloni!
 
wala hawakudhamini mchangiaji,wanajua kukusanya na kulipana pamoja na kukopeshana bila riba!
 
Nenda sasa kwenye ofisi zao particularly NSSF uone walivyo na nyodo.
 
Hiki ni kilio cha wengi. Naomba wataalam wanijuze malipo ya uzeeni mfuko wa PPF.
 
Heshima kwenu wanajamvi.

Mkuu Kakakiiza.Umenena haswa hakika kama kuna jambo linalokera wafanyakazi wengi wa kipato cha chini na kati ni mdudu mfuko wa hifadhi ya jamii.Fikiria unakatwa fedha 10% na mwajiri 10% kwa miaka mingi sana eg miaka 10,20 au 30 mwisho wa siku unapokwenda kudia mafao yako kiasi ulichochangia miaka 10 iliyopita eg 20,000/= per month hakilinganishwi na thamani ya fedha ya wakati huo.mfano mwaka 2000 us 1 ilikuwa sana na tsh 800.Pili uwekezaji unaofanywa na hii mifuko eg majengo makubwa,hisa kwenye makampuni mbali mbali hauna faida na mchangiaji kwa maana ya umiliki.

Wafanyakazi wa hii mifuko wamejipa mishahara mikubwa na marupurupu ya ajabu.Magari allowances na stahili kibao.Vyama vya wafanyakazi badala ya kukazania mishahara ipande waangalie uendeshaji wa hii mifuko wafanyakazi washirikishwe.Uandaliwe utaratibu mfanyakazi akichangia kiasi kikubwa apewe hisa.Mafao ya mfanyakazi anayestaafu yaboreshwe kumlipa mfanyakazi 30,000/= wakati gharama za maisha zimepanda maradufu ni udhalilishaji wa hali ya juu.
 
Mi nimeguswa sana na hii mada hasa hawa jamaa wa nssf kiukwel wanaboa kinoma hawako makini na kaz yao yan unakuta mtu anajiandisha uanachama alafu anafuatilia kadi zaidi ya mwaka na balaa ni pale unapoacha kaz miez 6 ishapita utahangaikia iyo pesa kama wanakupa bure kumbe umetafuta kwa jasho lako tena usiku na mchana wsivyokua na haya eti jitu linakwambia nipoze kidogo nikufanyie haraka mi naona kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko na mwanachama ahusishwe zaid ya ilivyo sasa.
 
Mimi naona vyama vya wafanyakazi havipo kwa masilai ya wanachama wao ndiyo maana migomo ya mkipanga kitu ikitokea na viongozi wa vyama vya wafanyakazi wakaitwa ikulu, utasikia tuwape serikali muda ili madai yetu yafanyiwe kazi baada ya miezi 3! kama hawajatekeleza tuingie tena katika maandamano!!.....

Lakini kama wangekuwa na uchungu na wanachama wao wangekuwa wakwanza kuwatetea maana hii mifuko ya jamii kwa sasa ipo kibiashara zaidi,na kwa kutumia pesa yetu wanachama!! Kwa sasa inahitajika kila mchango wa mwanachama uwe na riba kwani hizohizo pesa zetu ndizo zinaporomosha majengo na kulipa mishahara minono kwa wafanyakazi wao!

Mfano NSSF tazama Tanzania nzima ina majengo mangapi iliyo yapangisha!!Je mwanachama anafaidika vipi??

Tunadanganywa na Mafao ya uzazi,vifo,nk kwa nini tusifike mahali tuseme hapana??Au itungwe sheria mtu ukichangia miaka 10 ujengewe nyumba kwa mkopo kwa kukatwa asilimia 40 ya mchango wako na asilimia 60 apewe pale utakapo acha kazi!Lasivyo tunanyonywa sana na mifuko hii ya jamii.!!
 
Mimi ni mwanachama wa moja ya mifuko ya pensheni lakini ninavyoona wanachama wanaostaafu waanapata mafao kidogo sana.

Walipa michango ile tu iliyochangwa na mwanachama, kwanini hawalipi na riba.Mifuko ya pensheni kama PPF, NSSF na PSPF wanatoa mafao ya elimu,matibabu na mazishi.

Je hii inatosheleza kwa mwanachama anayechangia miaka 10,15,20 hadi 30? Ukilinganisha na faida wanayotengeneza?

WanaJF na wanachama wa mifuko hii mnasemaje kuhusu hili.
 
Mafao ni kidogo ila kuna tabia ya waajiri kutopeleka kiasi kinachostahili kwenye hiyo mifuko.
Niliulizia NSSF wanasema wanatoa riba.
 
Kama kweli wanatoa riba waliweke wazi suala hilo,pia waanze utaratibu wa kuwakopesha wanachama wao kama Benki ili waweze kujiendeleza.
 
Wananyonya sanaaaa,hii mifuko ya kijamii haitutendei haki kabisa,assume mtu alichanga mchango wake kipindi hiko assume 1995 akachanga 20,000/= akija kustahafu assume 2015 ile 20,000/= ya 1995 awaivaluate katika rate ya 2015 huu ni wizi mtupu......Mwaka 95 20,000/= ulikuwa unaweza kutumia mwezi mzima lakini sasa haifiki hata siku 3 waangalie na hili.....
 
Kwanini kusiwe na mfuko mmoja tu wa pensheni, jamani watu tunaumia ile mbaya.
 
Wahusika wa mifuko hii mlio JF mnayaona maoni haya.

Kama mwanachama angekuwa anaweka fedha zake Benki bila kutoa kwa miaka 10,15 hadi 20 anapostaafu sianapata fedha ya kuridhisha?

Serikali ichukue hatua kwa hili maana fedha za wanachama wa mifuko hii haiwasaidii wanachama,wanatumia kuendeshea miradi mbalimbali yenye faida lakini wanachama hawawekewi faida. Ingefanywa kama kwa wanahisa wa CRDB,TCC na TBL.

Wanachama wapewe faida kwa mtindo wa kugawiwa devidents kutokana na faida inayozalishwa na mifuko hii.
 
Bobsambeke III

Usichokijua bora ujikalie tu kimya!
Formula zote za kukokotoa mafao zina time of value na interest components!
 
Last edited by a moderator:

Back
Top Bottom