Hii michango sasa imezidi

nassa

Member
May 8, 2012
22
2
Jaman kuna m2 leo kaniletea kadi nimchangie 15000 kwa ajili ya graduation ya darasa la 7 ya mwanae, ikifika harusi je itakuwaje?
 
Dah jirani yaani nimekuletea kadi ya mchango elfu 15 tu ushakuja kubandika tangazo JF je ningekuambia uchangie laki 1 ingekuwaje?
 
Jaman kuna m2 leo kaniletea kadi nimchangie 15000 kwa ajili ya graduation ya darasa la 7 ya mwanae, ikifika harusi je itakuwaje?

Harusi ya huyo mtoto au ya aliekuletea kadi au yako wewe?
Funguka.
 
sasa wataka tuambia walalamika hela ndogo au kubwa...??
 
Ni kweli michango hii imezidi sana, kipaimara mtu kadi, mtoto kamaliza chekechea kadi!!!!

Kadi ziwe za mambo ya msingi.
 
Harusi ya huyo mtoto au ya aliekuletea kadi au yako wewe?
Funguka.

Mimi niko tayari kutoa mchango kwa yafuatayo; 1. kuchangia elimu (sio sherehe ya elimu). 2. Nyumba ya Ibada. 3. Mgonjwa.
 
Hayo ndo mambo ya kibongo. Tukiambiwa tuchangie madawati tunaona haituhusu!
 
Jaman kuna m2 leo kaniletea kadi nimchangie 15000 kwa ajili ya graduation ya darasa la 7 ya mwanae, ikifika harusi je itakuwaje?
mie leo nimepewa kali ya mwaka. Kuna binamu yangu aliniambia last month kuwa bintiye anapata kipaimara. Nikamuambia poa. Leo ananiambia unajua wewe ndio Godmother wake? Kidogo nizimie. Manake hapo kuna blackmail ya kununua nguo ya mtoto (traditionally ndo inakuwaga kazi ya godmother), na bado kwenda manake anakaa mbali karibia na mbinguni! Nimechoka manake kiddo mwenyewe sijawahi kummeet, naskia alibatizwa hospitali ati nikaandikwa mie!
 
unalo hilo!
 
si kila mchango uchangie, mwambie mhusika huna hela..... Kipaimara, komunyo , graduation ni shughuli ndogo za mzazi pekee..... Kwani akipika pilau akaita watoto mtaani na soda mbili mbili haiwi sherehe?

Darasa la 7 anataka kufanya sherehe akimaliza chuo je?

Walaahi mie harusi tu nachagua ya kuchangia, kipaimara, graduu, ubatizo nk wala sitoi hata ndururu
 
mie leo nimepewa kali ya mwaka. Kuna binamu yangu aliniambia last month kuwa bintiye anapata kipaimara. Nikamuambia poa. Leo ananiambia unajua wewe ndio Godmother wake? Kidogo nizimie. Manake hapo kuna blackmail ya kununua nguo ya mtoto (traditionally ndo inakuwaga kazi ya godmother), na bado kwenda manake anakaa mbali karibia na mbinguni! Nimechoka manake kiddo mwenyewe sijawahi kummeet, naskia alibatizwa hospitali ati nikaandikwa mie!

utu uzima dawa.. usikwepe majukum
 
utu uzima dawa.. usikwepe majukum

nisikwepe majukumu yake? Kwani kuzaa tulishirikishana jamani? Kwanza nimekumbuka, mtoto akianza mafundisho i was supposed to be informed. Ntapata pa kukwepea, ngoja tu. Hawawezi kunifilisi hivi hivi!
 
Darasa la7=15000, akifaulu form two watamfanyia sherehe watataka 25000, mahafali ya kidato cha nne watakwambia uchangie 35000, kadiria mwenyewe kidato cha sita, chuo na harusi yake watakwambia utoe kiasi gani?
 
maisha magumu sana usawa huu, hapo unachangia mengi,hyo sherehe ni sababu tu
 
Me leo nimeletewa kadi eti nimchangie anataka kufanya sherehe kwa kupata chuokikuu cha dsm. Mchango 25,000. Kweli hii michango imezidi.
 
mie leo nimepewa kali ya mwaka. Kuna binamu yangu aliniambia last month kuwa bintiye anapata kipaimara. Nikamuambia poa. Leo ananiambia unajua wewe ndio Godmother wake? Kidogo nizimie. Manake hapo kuna blackmail ya kununua nguo ya mtoto (traditionally ndo inakuwaga kazi ya godmother), na bado kwenda manake anakaa mbali karibia na mbinguni! Nimechoka manake kiddo mwenyewe sijawahi kummeet, naskia alibatizwa hospitali ati nikaandikwamie!

ùsichukie sana,

Ila kuwa honest to them aboùt your financial situation

Waambie umeandaa zawadi ya kukabili changamoto husika anazoenda kuziface now that kabarikiwa ( mnunulie kitabu kitakatifu, nadhani waweza afford hicho)

Yaani michango imezidi mpaka namba nisizozijua sipokei, unakaribishwa kwenye kikao cha harusi cha mtu u met mwaka 47 primary, bado makazini,majirani,kanisani,ukweni kila kona ....

Inabidi tu mtu uprioritize (sp)
 
Back
Top Bottom