Hii kitu imeishia wapi!?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
[h=1]Zitto wants Swiss bank accounts investigated probed[/h]Wednesday, 27 June 2012 Nadia Ramirez

The government has been asked to conduct thorough investigation to determine who owns the huge sums of money deposited in Swiss accounts.

Money amounting to more than Sh300 billion believed to be from the gas industry in the country is owned by some few Tanzanians.The call was made by Kigoma North MP, Mr Zitto Kabwe, who said the money is owned by about six Tanzanians. “We seriously want to know the names of the culprits,” he said.

He cited a case of India where the government named the culprits and confiscated the money proved to be dirty and used it to fund development projects in the country.

“Mr Prime Minister, we want the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) to immediately launch an investigation on the accounts, name the culprits and take legal action against them,” noted Mr Kabwe.
Recently, the Swiss National Bank (SNB) released a story which shows that a total of Sh303.7 billion have been stashed away by some Tanzanians in Swiss banks.
On his side, the anti-corruption chief Mr Edward Hosea said Tanzania needs to establish from Switzerland who owns the money and if it is illegally acquired and would consult the Bank of Tanzania (BoT) on the immediate steps to be taken.

“After we have established where the money originated from, we will follow due procedure and make sure the money is returned home,” Dr Edward Hoseah said. “We shall use available laws that guide all nations.”
 
Zito alisema kama serikali haitawataja hadi kufikia kikao cha bunge lijalo, yeye atawataja. Bunge linakaa hivi karibuni. Subiri!
 
Ngoja tusubiri mkuu ili tuone kile kitakachojiri kuhusiana na sakata hili.

Zito alisema kama serikali haitawataja hadi kufikia kikao cha bunge lijalo, yeye atawataja. Bunge linakaa hivi karibuni. Subiri!
 
Daniel Mjema, Rombo na Exuper Kachenje, Dar
Mwananchi

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amemlipua Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk Edward Hoseah, akidai kuwa bosi huyo ameandikia barua Uswisi, akieleza kwamba Tanzania haina masilahi na mabilioni ya fedha yaliyofichwa katika benki za nchini hiyo.

Zitto amedai pia kwamba, atawasilisha hoja binafsi katika kikao cha Bunge kinachoanza keshokutwa Jumanne, akiiomba Benki ya Dunia (WB), kutumia kikosi chake kinachojulikana kama Asset Recovery Unit (ARU), ili kuwabaini Watanzania walioficha fedha hizo na namna gani zitarejeshwa nchini.

Hata hivyo, alipotafutwa na Mwananchi Jumapili jana jioni, huku akionyesha kushangazwa na madai hayo ya Zitto Dk Hoseah amekanusha akisema kuwa tuhuma hizo hazina ukweli wowote.

"Nashangaa, kwanza nipo hospitali naumwa, wala sijawahi kuandika barua anayodai Zitto,"alisema Dk Hoseah.
Mkurugenzi huyo wa Takukuru alisisitiza: "Anavyosema Kabwe, labda muulizeni Huo ni uongo, mimi sijawahi kuandika barua hiyo na sifanyi biashara hiyo. Tambua kuwa hilo siyo kweli, sisi tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria. Kama kweli mwambieni huyo Zitto aonyeshe hiyo barua."

Hata hivyo alivyotakiwa kueleza kuhusu afya yake na mahali alipolazwa, Dk Hoseah alisita na kusema:
"Wewe jua hivyo tu kwamba ninaumwa, nimepumzika. Siyo India, nipo nyumbani."

Zitto Kabwe alitoa tuhuma hizo dhidi ya Dk Hoseah jana eneo la Kibaoni, Kata ya Nanjara Reha, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro katika mkutano wa hadhara, ambapo alimtaka Dk Hoseah ajitokeze hadharani na kuwaeleza Watanzania sababu za kuandika barua hiyo.

"Juzi tumeambiwa, Dk Hoseah ameandika barua kwenda Uswisi kuwaambia ya kwamba, Tanzania hatuna interest (masilahi) na hizo fedha zilizofichwa huko nje kwa sababu ni fedha binafsi…; Huyu ndiye mkurugenzi wa kupambana na rushwa nchini," alisema Zitto.

Aliongeza: "Tunamtaka Dk Hoseah atuonyeshe barua aliyoiandika kwenye mamlaka za kule Uswisi na atuambie ni kwa nini ameandika barua kama hii kwa sababu, tunataka fedha hizi zijulikane ni za akina nani na zirejeshwe nchini."

Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni na Naibu Katibu Mkuu Chadema, alisema kuwa Watanzania walioficha zaidi ya Sh340 bilioni hawazidi 50 hivyo ni lazima wajulikane na fedha hizo zitaifishwe.
"Wamezificha fedha hizi nje wakati sheria za nchi zinakataza," alisema na kufafanua kuwa sheria ziko wazi kuwa hakuna Mtanzania anayeruhusiwa kuwa na mali nje ya nchi bila kuwa na kibali cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hivyo fedha hizo ziko huko kinyume cha sheria.


"Wenzetu wa Senegal wamefanya hivyo, India pia wamefanya hivyo….; Ujerumani na Marekani wao wameamua kuwatoza kodi watu wenye fedha za aina hiyo, lakini sisi tunataka kujua hizi fedha zimetokana na nini kwa sababu zipo ambazo zimetokana na wizi na ufisadi," alisema.

Alidai kuwa sehemu ya fedha hizo imetokana na wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya BoT, ufisadi katika Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Meremeta iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na uchimbaji wa gesi katika baadhi ya mikoa nchini.

Mbunge huyo alienda mbali akisema: "Tunataka kiongozi yeyote wa kisiasa wa Tanzania anayejijua kwamba ana mali nje ya nchi ajitangaze mapema na aseme amezipataje hizo mali, kwa sababu njia pekee ya kupambana na ufisadi ni uwazi."
Agosti 15 mwaka huu, kambi rasmi ya upinzani bungeni, iliitaka Serikali kuwataja kwa majina viongozi na wafanyabiashara wakubwa walioficha Sh315.5 bilioni nchini Uswisi.


Akiwasilisha hotuba ya kambi hiyo, Waziri Kivuli wa Fedha, Kabwe Zitto alisema endapo Serikali itashindwa kuwataja watu hao, kambi hiyo itawataja kwa majina katika Bunge linaloanza wiki ijayo.
Zitto alisema mmoja wa viongozi wa juu wa Tanzania (hakumtaja), baadhi ya mawaziri wa Serikali za awamu zilizopita na wafanyabiashara wazito ni miongoni mwa wamiliki wa fedha hizo.

Alisema taarifa ya Benki Kuu ya Uswisi ya Juni mwaka huu, inaonyesha kuwa fedha hizo Sh315.5 bilioni zimetoroshwa na kufichwa kwenye benki mbalimbali nchini humo.
Alidai kuwa fedha hizo zinatokana na biashara zilizofanywa na watendaji wa Serikali na wafanyabiashara kadhaa kwenye sekta za nishati na madini.
Sehemu kubwa ya fedha zililipwa na kampuni za utafutaji mafuta na gesi katika pwani ya Mkoa wa Mtwara zilizopewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006.
Baada ya Zitto kumaliza kuwasilisha hotuba yake, Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole-Sendeka (CCM) aliomba mwongozo wa Spika kuhusu suala hilo.


Sendeka alisema Zitto alisema miongoni mwa walioficha fedha hizo ni kiongozi wa juu kabisa wa Tanzania, lakini akashangaa Serikali kutohoji juu ya kauli hiyo.

Naibu Spika, Job Ndugai alisema kuwa angetoa mwongozo huo baada ya kuipitia hotuba hiyo ya kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na kuona kama ina matatizo.

Hata hivyo, uchunguzi zaidi wa gazeti hili baadaye ulibaini kuwa fedha hizo zilikuwa na uhusiano na ufisadi kupitia Meremera, unaohusisha Dola za Marekani 132 milioni wastani wa Sh211.2 bilioni.
 
Mkulu alinukuliwa akisema:"Ni upepo tu,utapita!"

Sisi kama watanzania tunafanya mambo na hata kufikiri au kufuatilia yanayojiri kwa mtindo wa vikosi vya zimamoto au povu la coca cola.
 
Mkulu alinukuliwa akisema:"Ni upepo tu,utapita!"

Sisi kama watanzania tunafanya mambo na hata kufikiri au kufuatilia yanayojiri kwa mtindo wa vikosi vya zimamoto au povu la coca cola.

Ujasiri kama wa Zitto ni kitu cha kuigwa na kupewa support bila hivo kwa wabungu wa CCM tu wataongea na kisha watakaa kimya..
 
Ujasiri kama wa Zitto ni kitu cha kuigwa na kupewa support bila hivo kwa wabungu wa CCM tu wataongea na kisha watakaa kimya..

Nakubaliana na kauli yako.
Zitto aliahidi pia kuwataja ,je ameshafanya hivyo?

Lakini hata akiwataja, inasaidia nini?

Wametajwa Mafisadi papa(list of shame)
Sakata la rada(ufisadi katika ununuzi wa rada), wahusika wametajwa.
Rais Kikwete alisema anayo orodha ya wauza unga.

Kuna mtanzania ambaye hajui kuwa nchi imegeuzwa shamba la bibi? Wahusika wanachukuliwa hatua?
EPA, RICHMOND,DOWANS, Utoroshaji wa wanyama kutoka mbuga zetu. Orodha ni ndefu.

Kuna aliyechukuliwa hatua?....Nini kifanyike?
 
Nakubaliana na kauli yako.
Zitto aliahidi pia kuwataja ,je ameshafanya hivyo?

Lakini hata akiwataja, inasaidia nini?

Wametajwa Mafisadi papa(list of shame)
Sakata la rada(ufisadi katika ununuzi wa rada), wahusika wametajwa.
Rais Kikwete alisema anayo orodha ya wauza unga.

Kuna mtanzania ambaye hajui kuwa nchi imegeuzwa shamba la bibi? Wahusika wanachukuliwa hatua?
EPA, RICHMOND,DOWANS, Utoroshaji wa wanyama kutoka mbuga zetu. Orodha ni ndefu.

Kuna aliyechukuliwa hatua?....Nini kifanyike?

List ya mafisadi bado haijapatikana rasmi! lakini hata kama hela hazitarudi ila inasaidia kuwatisha wengine ambao
walikua na mpango kama huo in future!
 
Six people owning money hiden in Swiss
  1. Zuberi Zitto Kabwe
  2. awataje wanzake.......
  3. ....
  4. ,,,,
  5. ----
  6. äää
 
zito hana ubavu wa kuwataja wote walioficha pesa nje،saana atawataja wawili au watatu wadogowadogo au asiwataje kabisa،hatadhubutu kugusa vigogo،subirini muone.
 
ZITTO ASISITIZA NYARAKA ZIPO, DK HOSEAH NDIYE ANAYEZIZUIA

VIGOGO 10 wametajwa kuhusika katika kashfa ya kuficha Sh303.7 bilioni katika benki mbalimbali nchini Uswisi.
Katika orodha hiyo inadaiwa kuwa yupo kiongozi mmoja mwandamizi mstaafu, maofisa watatu wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mawaziri wastaafu ambao baadhi yao bado ni wabunge na aliyewahi kuwa kiongozi mwandamizi wa Benki Kuu Tanzania (BoT).

Majina hayo ambayo mwandishi wetu amefanikiwa kuyaona, yamo katika orodha ya mchunguzi mmoja wa kimataifa wa masuala ya ufisadi (jina tunalo).
Juzi, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alimshukia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah akimtuhumu kuandika barua Uswisi akisema Tanzania haina masilahi na mabilioni ya fedha yaliyofichwa katika benki zilizopo nchini humo. Hata hivyo, Dk Hoseah alikanusha madai hayo akisema hajawahi kufanya hivyo.

Akizungumza jana Zitto alisisitiza kauli yake akisema: "Sijawahi kumsema Dk Hoseah kwa lolote, kwa nini leo nimsingizie? Yeye mwenyewe anajua ushirikiano niliompa wakati wabunge wanapinga yeye asichunguze malipo ya posho mara mbili kwa wabunge."

"Nilisimama kidete kusema Takukuru wapo sahihi na mimi nilikwenda mwenyewe kwao kuhojiwa na kuagiza wajumbe wa kamati yangu (Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma), waende kuhojiwa. Spika aliyestaafu (Samuel Sitta) akaizima kashfa ya wabunge kupokea posho mara mbilimbili. Mwulizeni amesahau? Sasa leo nimzushie ili iwe nini?."

Alisema orodha ya Watanzania wenye fedha huko Uswisi, ipo na ameiona na nyaraka zinaweza kutolewa kwa taasisi za Serikali tu.

"Dk Hoseah kazuia nyaraka hizo. Akitaka nimwonyeshe mtu anayeweza kutoa nyaraka hizo, nipo tayari isipokuwa aahidi kuiweka wazi," alisema Zitto.
Alisema katika orodha ambayo Waziri wa Fedha wa Ufaransa anayo, kuna Watanzania lakini akaituhumu Serikali akisema haitaki kufuata njia halali za kupata orodha hiyo kwa kuwa viongozi wengi na wafanyabiashara wakubwa wana akaunti katika benki za Uswisi.


Juni 26, mwaka huu gazeti hili lilichapisha habari kuhusu utoroshwaji wa fedha hizo na kueleza kuwa Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kwa kushirikiana na Takukuru inachunguza suala hilo.
Kiasi hicho cha fedha kimedaiwa kuingizwa katika akaunti za Watanzania na kampuni moja ya uchimbaji mafuta na kampuni kadhaa za uchimbaji madini ambazo zinafanya kazi Tanzania.

Chanzo hicho kiliongeza kwamba kiasi hicho cha fedha kipo katika akaunti sita tofauti zinazomilikiwa na Watanzania wakiwamo wanasiasa wakubwa.
Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa tangu akaunti hizo zifunguliwe, wamiliki wake halali hawajawahi kuingiza hata shilingi.
"Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa fedha hizo zipo katika akaunti sita tofauti ambazo zinamilikiwa na wanasiasa wakubwa nchini na wenzetu wa Uswisi wameeleza fedha hizo zimeingizwa na kampuni kadhaa ambazo zinahusika na mafuta pamoja na madini hapa nchini," kilidokeza chanzo hicho.

Kugundulika kwa kiasi hicho cha fedha katika benki za Uswisi ni kutokana na ripoti ya Benki ya Taifa ya Uswisi (SNB) iliyotolewa mwaka huu.

SOURCE: Mwananchi
 
Back
Top Bottom