hii kaz ya uandish ndo maana cipendi...

Rog3rz

Member
Jun 21, 2012
44
26
Mkulima amejiwa na mwaandishi wa
magazeti kumuhoji ... kuhusu maisha ya
shambani,na mkulima huyu hawapendi
waandishi wa habari akaona bora
amchoshe katika kujibu maswali,
na mambo yakawa hivi; MWANDISHI: Wewe unawalisha ng'ombe
chakula gani?,
MKULIMA: Ng'ombe yupi Mweupe au
Mwekundu?
MWANDISHI: Ng'ombe mweupe
MKULIMA: Ninamlisha nyasi na viguta vya mahindi,
MWANDISHI: Na mwekundu??
MKULIMA: vilevile nyasi na viguta vya
mahindi,
MWANDISHI: ahaa sawa,na sehemu ya
kulala ni wapi? MKULIMA: Ng'ombe yupi mweupe au
mwekundu?
MWANDISHI: Mweupeee!!!
MKULIMA: Mweupe ninamlaza bomani
kulee,
MWANDISHI: na mwekundu? MKULIMA: vilevile ninamlaza na
mwenziwe!!!!
MWANDISHI: Hii sehemu yote
majumbamengi,Na wakienda
kulisha unafanyaje?
MKULIMA: Yupi mweupe au mwekundu? MWANDISHI: Woooteeee!!!! {kwa hasira}
MKULIMA: Mweupe nina mfunga kambana
kumzungusha
malishoni na kumrudisha,
MWANDISHI: na mwekundu vilevile?
MKULIMA: Mwekundu?,mweku ndu ninamfunga kamba na
kuzunguka nae kama mwenziwe!!!
MWANDISHI: Kwanini kila mara nikikuuliza
huduma
za ng'ombe zako unaniuliza mweupe au
mwekundu halafu inatokea kuwa kazi zao wote ni
sawa?????,
MKULIMA: Kwasababu Ng'ombe mweupe
ni wangu,
MWANDISHI: Na mwekundu?
MKULIMA: Ni wangu vilevile!!!!!! MWANDISHI HOI..!!
 
Back
Top Bottom