kaburunye
JF-Expert Member
- May 12, 2010
- 672
- 74
Wadau; naomba ni-quote kutoka gazeti la majira la leo:
"MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imesema pamoja na juhudi zinazofanyika kupunguza uchanganyaji wa mafuta ya taa kwenye dizeli na petroli, tatizo hilo halitakoma kama kodi na ushuru wa mafuta hayo utaendelea kutofautiana". Mwisho wa kunukuu
Je ni kweli kuwa tatizo ni kodi ya mafuta na eti kodi ikiwekwa vizuri hapatakuwa na kachumbari kwenye mafuta? au hawa jamaa wanatafuta visingizio tu? Mi nahisi wameshindwa kazi na wanatafuta "escape route". Vituo vinavyochanganya mafuta vinajulikana na hawawezi kukwepa kuwajibika. Ni sawa na kusema ili ufisadi maofisini basi wafanyakazi wapewe mishahara minono. Hata kama kodi ikirekebishwa tatizo litaendelea kuwepo maana wafanyabiashara wanajua hata wakichanganya mafuta hakuna hatua itakayochukuliwa - maana wao wanajali faida kubwa tu haijarishi imepatikanaje.