JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,202
- 5,012
Posted by queenkami | May 15, 2012
Hello wapendwa wangu.
Kuna ndugu yangu wa damu alinifanyia jambo ambalo kawaida ndugu hawezi kumfanyia ndugu yake,ni kitendo cha laana,abomination,kwa jinsi nilivyo sikujua kamwe kama naweza ku expirience kitu kama hichi,siku zote nilizani hufanywa na watu kutoka kwenye koo zenye laana.
Nilikuja kujua siri hii baada ya ndugu yangu huyo kugombana na rafiki yake ambaye ndiye aliyeitoa siri,niliugua depression,nilifikia hadi kufikria kujiua,maisha yangu yote nikayaona hayana thamani,nilikua najisikia vbaya sana.
Hata hivyo nilifikia sana na kwa vile mim nimeokoka nikaona kwa vile kilichotokea kimeshatokea nikachagua kumsamehe ndugu yangu,nikaona siko tayari kumpoteza ndugu yangu japo nilijua ana roho ya ajabu.
Hii siri sikumweleza mtu yeyote bali nilimweleza mama yangu tu ili ajue mambo ambayo mwanae nimefanyiwa.
Basi yule ndugu yangu aliposikia kuwa nimemueleza mama akanipigia kuwa kuanzia dakika hiyo tunayoongea nijue kuwa siko katika list ya ndugu zake,hanijui nisimjue.Pmaoja ya kwamba mim ndiye niliyetendwa nikambembeleza huku nikilia kuwa sisi ni ndugu tusiruhusu kitu chochote kitutenganishe.
Katika simu hiyo sikutaka kuongea kwa hasira wala kwa kugombana bali yeye ndo aliyekua yuko juu as if mim ndiye mkosaji,akisisitiza kuwa nisimjue.
Sikutaka aniombe msamaha wala nini nilitaka tu maelewano,tuwe tu kama jinsi ambavyo ndugu wanatakiwa kuwa lakini jinsi nilivyojishusha alichukulia sijui kama mim najiona ndiye mkosaji au vipi na ndivyo alivyozidi kunionesha chuki na kujitahidi kuongea uongo watu wanione mim ndiye mbaya na katu hakulegeza moyo wake.
Nikikutana naye mjini huwa nasimama kwa lengo lakusalimiana naye ila yeye ananipita kama vile ni invisible sionekani,wakati mwingine nampigia simu anavyonijibu naishia kujisikia vibaya.
Sasa ikafikia wakati niasema kutendwa nitendwe mim kujimbembelezesha nijibembelezeshe mim,nikasema kama noma na iwe noma nimechoka,na mim nikaamua kukaa kimya.
Kinachoniumiza ni kwamba,anawaambia watu eti mim najifanya mlokole lakini siongei na ndugu yangu wa damu.
Pili kwa vile yeye ndiye mkubwa watu wananilazimisha nimuombe yeye msamaha eti ili tu yaishe lakini naona nikimuomba msamaha itakua wa unafiki sababu ndani ya moyo wangu najua sijamkosea.
Wakubwa wa hapa naombeni mniambie nyie mngefanyaje hapa.
Shukrani

Last edited by a moderator: