Hii Inawahusu Wanaume Wa Dar

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,077
17,207
Waraka wangu kwa Wanaume wenzangu especially
mnaoishi Dar...Kuweni makini sana na Wanawake wa
mji wa dar.... Wana uongo kuliko Dibaji kwenye
Kamusi ya Ibilisi, wanajua kukuchota akili
balaa, ilimradi uingie kwenye 18 uoe...Ukimtokea
anajifanya kama vile we ndo Mwanaume wake wa Pili, wa kwanza wa shule ya msingi we ndo wa pili.
Ukimuuliza Hobby zake utamsikia, ''Uum ,halafu
analamba Lips, napenda kusoma Biblia,Napenda
kwaya ya Kijitonyama Uinjilisti, Napenda kufundisha
watoto Sunday School, napenda nyimbo za Bahati
Bukuku na kucheza na watoto, yaani I love sana Babies'' Basi ataji-position utajiona una bahati
umekutana na wadogo zake bikira maria waliobakia
Tanzania, utajua umeokota Embe dodo chini ya mti
wa mpera.. Mkitoka Outing anavaa mgauni mrefu
kama Shemasi wa Parokia ya Sinza ukimuuliza
unakunywa nn utamsikia,'naomba maji ya Dasani please'...Umetegwa Baba!
Ni Kiruka njia
mtakatifu, Mlevi mkubwa, yuko bize Usiku kama Kigofu
cha Polisi kinasaka Wazururaji kuanzia Tegeta mpaka
Black Tomato anajulikana, ana vaa visketi vifupi kama
Kibwaya ukiwa haupo.. Ila kwako anakuektia mzee
unatangaza ndoa, kasheshe ukifika nae ndani sasa ndo unakuta Gypsum hadi chooni, Sebule kama uwanja wa
Taifa, hapo ndo utajua umeoa Dalali!
 
kuna watu wanashida sana dunia hii
1: mashabiki wa arsenal
2; mashabiki wa kiba
3; wanaume wa dar
pole za dhati kwa hawa watu
 
Back
Top Bottom