Hii inasikitisha watanzania

Quinty

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
462
74
Hii hali ya Ubungo Bus Terminal inasikitisha sana kuona kuko giza kila umeme unapokatika. Nimeshuka hapo mara kadhaa usiku ni giza nene. Sipendi kuamini kuwa uongozi wa hapo umeshindwa kugharamia generator wakati wa usiku. Hayo makusanyo ya sh. 200/- kila kichwa, 500/- gari ndogo na gharama za kulaza mabasi zinafanyia kazi gani? Wageni wanataabika hawaoni mwelekeo, hawaoni wenyeji wao, wenyeji pia hivyo hivyo hawajui hata mabasi yanayoingia. Wabeba mizigo Na vibaka hawaonekani maana giza. Huduma ya matangazo nayo hamna. Wanaokusanya pesa wanatumia mishumaa..! Watanzania lini tutaachana Na hii dhuluma ya viongozi wetu Na kunyanyasika Na kodi zetu kuliwa bila kupata huduma stahili...?
 
Inasikitisha sana ila hicho ndio halali yetu Watanzania. Ukipeleka bidhaa zako sokoni lakini ukashindwa kuongea na mnunuzi ili mkubaliane bei, basi jamaa atakupa bei yoyote atakayojisikia. Unaweza kulalamika kuwa umepunjwa?

If you don't bargain, you always get what the buyer wishes to offer!
 
Mkuu, ni mradi wa mafisadi huo wala hawana machungu na maisha ya watu!

Kweli huu mradi wa mafisadi c kulikuwa na wale watoto Wa kigogo walipigwa chini sasa sijui wamewekwa fisadis ganii?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom