Hii inasikitisha sana

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
SHULE ya msingi Mazizi iliyoko kata ya Gwata, tarafa ya Mikese, wilaya ya Morogoro imefaulisha mwanafunzi mmoja katika kipindi cha miaka saba iliyopita ilipoanzishwa shule hiyo.


Akizungumza katika mkutano na wanachama wa Umoja wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali mkoani Morogoro (UNGO) waliotembelea shule hiyo, mkuu wa shule hiyo Chalo Chalo alisema kuwa mwanafunzi aliyefaulu darasa la saba kwenda kidato cha kwanza alihitimu mwaka 2008.
Alisema kuwa kitendo cha shule hiyo kushindwa kufaulisha wanafunzi kimetokana na changamoto nyingi zinazoikabili ikiwa ni pamoja na uhaba wa walimu, vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, huduma za kijamii na nyinginezo.


Alisema kuwa kwa miaka mitano toka ilipoanzishwa shule hiyo kulikuwa na mwalimu mmoja ambaye alikuwa akilazimika kufundisha wanafunzi wote hali ambayo alidai kuwa isingewezesha watoto kuendelea kielimu.


Chalo aliongeza kuwa kwa sasa shule hiyo inajumla ya walimu wanne huku wawili kati yao wakidaiwa kuondoka kwa ruhusa maalum katika kipindi kisicho julikana.
“Mazingira ya kazi huku yanakatisha tamaa kwa walimu kuja kufundisha, kwa vile hakuna huduma muhimu ya kijamii huduma tunalazimika kuzifuata mbali, hakuna nyumba za walimu ndiyo maana walimu wanakuja na kuondoka,” alisema mwalimu mkuu huyo.


Mwalimu huyo ameiomba serikali kuboresha mazingira ya kazi katika shule hiyo na kuongeza idadi ya walimu, kujenga nyumba za walimu, kuongeza vyumba vya madarasa, kuboresha miundombinu ili kuimalisha elimu katika shule hiyo.


Nao wanachama wa UNGO waliotembelea shule hiyo na kukutana na kamati na walimu wa shule hiyo kama sehemu ya mafunzo yao kwa vitendo baada ya kujifundisha darasani juu ya utawala bora walisema bado yako mambo yanayohitajika kufanyika.


Charles Mengere mkurugenzi wa taasisi ya Greenbelt Secondary school alisema kuwa kukosekana kwa ushirikishwaji miongoni mwa jamii ni kikwazo cha utawala bora.


Alisema kuwa katika shule hiyo kamati ya shule na walimu wamekuwa hawashirikishwa sawia na halmshauri ya wilaya katika mipango mbalimbali ya maendeleo.
 
tupeni ridhaa yenu, na tutafanya zaidi...

tutafanya zaidi mkitupa ridhaa zaidi...
tupeni ridhaa yenu na tutfanya zaidi
tutafalakjso[a[ajaaaaa...a zaiidiama/....a

tfvdklal [KISHINDO]

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Inapendeza sana.

Lakini tutafika, Imani yangu ni kwamba, Mungu hajatuacha watanzania kabisa kabisa.
Ipo siku atatukumbuka, ipo siku Mungu ataingilia kati na kushiriki katika kuweka viongozi sahihi katika nchi yetu, Mungu atatupa nafasi Watanzania kufarijika japo kidogo. Atasitisha washirikina kutuchagulia viongozi

Haya yote yanayofanywa na CCM, Mungu anayaona,Elimu ni ufunguo wa Maisha, Binaadamu asiyekuwa na ufahamu ni kama mnyama kabisa, CCM Hawajali hili, wanafurahia hali hii.kwao, hii inawapa fursa ya kututawala zaidi zaidi

Watanzania tunapaswa kupiga kulele na kulia sana, tunapaswa kugalagala chini na kujipaka majivu, tumulilie Mungu, tumueleze Mungu Mbona ametuacha, Mbona sisi tu.

Labda ni Sasa
 
Usishangae wanakijiji hicho wengi kuipigia kura CCM - sijui watu wamelogwa huko vijijini?
 
Si lolote si chochote hizi ni mbinu tu za kutaka watoto wao waendelee kututawala. nikiwa na maana kwamba watoto wao tu ndio watakao pata elimu bora na si vinginevyo. Ili kulithibitisha hili angali kama kwenye shule hiyo kuna mtoto hata mmja wa kigogo. Mmmmh!!!!!!!!! inauma sana lakini tusemenini ili hali wao ndio walioshikilia nchi. Yangu mi sala tu!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kidumu Chama Cha Mapinduzi, Zidumu Fikra za Mwenyekiti.

Mapinduzi Daima, Tutawapindua Tuendelee Kuwatawala.

CCM OYEEE!!!
 
Back
Top Bottom