Hii imemtokea mhasibu wetu hapa ofisini

Obama wa Bongo

JF-Expert Member
May 10, 2012
5,414
4,867
Dear friends

Leo nimeona ni vyema nika-share nanyi kisa hiki cha kutekwa mfanyakazi
mwenzetu ambaye ni cashier siku ya jumatano jioni wiki iliyopita.

Ni kama movie lakini ni ukweli, cashier wetu aliomba ruhusa siku hiyo ya
tukio aende kwenye mkutano wa wasabato uliokuwa uliendelea viwanja vya
biafra. Yeye pia ni msabato aliyeishika dini ya Sabato haswa, kwa hiyo
aliondoka saa kumi kamili badala ya saa kumi na moja

Baada ya dakika 40 tulianza kupokea sms zinazosema mwenye namba xxx
amepata ajali na kufa papo hapo na kwa taarifa zaidi twende muhimbili
hospital. Baada ya kutazama hiyo namba xxx ilikuwa ni ya cashier wetu.
Tulijaribu kuipiga iliita tu bila kupokelewa, na pia tulipiga namba
iliyotutumia sms iliita bila majibu. Ilipofika saa kumi na moja tuliamua
kuelekea muhimbili, ma baada ya kufika pale emergence tukaambiwa tuelekee
chumba cha kuhifadhia maiti. Tulioneshwa mwili wa mtu aliyepata ajali
lakini haukuwa wa cashier wetu, tukawatuma wenzetu waende hospitali zote
lakini hapakuwa na taarifa zake

Baada ya kuzunguka bila mafanikio tulitoa taarifa makao makuu ya usalama
barabarani na baada ya dk kumi wakatwambia kuwa hakuna taarifa za ajali
mbaya iliyotokea jioni hiyo. Hatua iliyofuata ilikuwa ni kutoa taarifa
polisi juu ya tulio hilo na ndipo waliposema kwa kuwa ni mtu mzima
tusubiri hadi siku inayofuata. Wakati huo huo ndugu zake pamoja na
wafanyakazi wenzetu walikuwa pamoja wakiendelea na jitihada za kumtafuta
hadi saa sita usiku. Kilichokuwa kinatia wasiwasi zaidi ile namba
iliendelea kutumia sms namba takribani zote zilizokuwa kwenye phonebook
yake na ndugu zake hawakuwahi kuona ndugu yao akichelewa kiasi hicho.

Ilipotimu mida kama ya saa sita na nusu walisikia mtu akigonga mlango,
alikuwa kaumizwa na amejaa matope, hakuwa na uwezo wa kuzungumza sana,
ilibidi wampeleke kituo cha polisi na baada ya muda hospitali ya
mwananyamala.

Alipopata nguvu alianza kuwasimulia nduguze kilichotokea. Alipotoka
ofisini alikwenda moja kwa moja kwenye kituo cha daladala cha karakana,
pale kituoni walikuwa abiria wawili yaani yeye na mama mmoja. Baada ya dk
chache ilikuja coaster iliyoandikwa mbele Kawe na ilikuwa na tinted
nyeusi, yule mama hakupanda sababu alikuwa anaelekea posta ila yeye
alipanda. Ndani ya gari kulikuwa na watu watatu pamoja na dereva, wawili
wakiwa wamekaa nyuma na mmoja akiwa amekaa karibu na driver. Gari hiyo
hiyo ilikuwa ni mpya, mmoja wa abiria alimumba simu cashier apige simu
moja kwa jamaa yake maana alidai kuwa simu yake illiishiwa charge na
walikuwa wametoka mtwara kupeleka maiti, alimuuliza cashier umri wake na
kama ameoa na anafanya kazi wapi, cashier akamjibu hajaoa na hana kazi pia
ana miaka 32. Walipofika Tazara hawakutaka kupakia abiria yoyote na
walikuwa wote wamevaa miwani myeusi, na ndipo akaanza kuingiwa na mashaka
akaomba ashuke, wao wakamwambia watapita biafra na hawana mpango wa
kusanya kwa kuwa hata yeye walimpa lifti tu. Gari ilipokaribia taa za
buguruni akainuka ili ashuke, jamaa wale wa nyuma wakamkalisha chini kwa
nguvu, na sio kwenye viti yaani chini kabisa. Mmoja wao akafunga kitambaa
cheusi kwenye macho na mikono ikafungwa kwa nyuma na mipira, baada ya muda
akasikia kama wamempulizia perfume. Akihisi fahamu kumtoka polepole na
neno lamwisho analokumbuka alisikia kuwa waelekee misitu ya Kibaha
wakamalize kazi. Kilichomwamsha ni kofi zito alilopigwa na kusukumwa hadi
nje ya gari. Alianza kulia na kuwasihi wasimdhuru, wakaanza kumrusha
kichurachura huku wakimkanyaga. Walikuwa wameshamfungua kitambaa machoni
na waliacha gari umbali kama wa dk kumi na lilikuwa ni pori zito na giza,
wao walivaa vitu usoni na walikuwa wamevaa gloves. Wakamwekea simu yake
mfukoni wakiwa wametoa simcard, walichomwambia wanachohitaji ni sehemu
zake za siri na sio kitu kingine. Mmoja wao akaambiwa alete kisu kikali
wanachokitumia, na walipompigia boss wao akawasisitiza nyeti zinazotakiwa
lazma ziwe za mtu wa miaka 40 na kuendelea. Mwenzao mmoja akasema cashier
alisema alikuwa na miaka 32, baada ya kumkagua wakakuta card yake
inaonyesha kazaliwa mwaka 1979. Kulingana na yeye asemavyo ndicho
kilichomwokoa ila waliendelea kumkung'uta kwa hasira. Wakamrudisha kwenye
gari na baada ya mwendo wakampakia kwenye gari nyingine ndogo iliyokuwa na
watu wawili ambao walimchukua na kumtelekeza maeneo ya sayansi.
Hawakuchukua kitu hata kimoja wala kumwambia lolote,siku iliyofuata
alipelekwa agakhan kwa uchunguzi zaidi na kwa sasa anaendelea vzr.

Kwa ufupi ni hayo, ukweli mwenyezi Mungu atulinde na tumwombe pia
abadilishe mioyo ya watu ambayo imekuwa migumu mno kwa ajili ya kupata
vyeo na utajiri wa haraka
 
Duu, Kama "movie" vile.

Anyway inasikitisha sana na jamii inapaswa kuwa "extra care" kwani Ibilisi kaamua kujikita zaidi kwenye fedha!!!
 
i knw this story, nadhani ni ulozi huo! na hivi 2015 inakaribia, watakata mpaka makwapa yetu wayapeleke kwa waganga! MUNGU WETU UTULINDE!
 
i knw this story, nadhani ni ulozi huo! na hivi 2015 inakaribia, watakata mpaka makwapa yetu wayapeleke kwa waganga! MUNGU WETU UTULINDE!

Tena ulivyo na macho mazuri chunga sana..wakimaliza vikwapa wanakuja hapo
 
Inabidi kuwa makini sana na hizi gari zinazochukua abiria. Haya matukio yamekuwa mengi sana sasa hivi!
 
Ni mara ya tano naona post ya maelezo kama haya!! Sijui inakuwaje hapo!!
 
Nashukuru kwa Story ya huyo Jamaa,Pia nashukuru kwa kunifungua macho kwa yanayojiri Mjini.Mungu ni Mwema atakuwa naye kwenye Matatizo ya Kujiuguza.
 
Hii story mbona kwa mtazamo wangu inakosa ushawishi kuwa ni tukio la kweli. Katika mazingira ya kawaida, inakuwaje unapanda kwenye gari liko tinted, vioo vyote vimefungwa, kuna abiria watatu wote wamevaa miwani myeusi na zaidi unaulizwa umri na mtu usiyemjua na bila ya wasiwasi unajibu. Kama ni kweli imetokea, basi huyo aliyepatwa ana jambo anaficha.

Hii story haina tofauti na ile ya mkono wenye manyoya ambayo watu waliamini lakini mwisho wa siku hakuna aina yeyote ya ushahidi kuwa jambo hilo kutokea.
 
Back
Top Bottom