Hii imekaaje ya kuja kulipia daraja la Kigamboni?

Mpaka Daraja La Kigamboni linakuwa kama Babu wa Loliondo? Is it real a big deal kulipia kupita kwenye daraja? Politik imeharibu Bongo za Watanzania!!!

Haya ndiyo matatizo ya kuzoea kuchangia harusi badala ya kuchangia ada ya mtoto kwenda shule!!!
 
Suala la bei (214bn) na muda wa kumaliza(2015).......another financing mechanism by CCM...na Magufuli ni one of the contenders.Ndio maana mwaka huu kaamkia Kigamboni

Kazi kweli kweli.
Ulitaka lijengwe lini ili wewe ufurahi.
OTIS
 
Labda mimi sielewi! Sijawahi kusikia dunia hii kunanchi inatoza hela ya kutumia barabara au daraja, zaid ya kodi, fines. Hii ya daraja la kigambon kuja kulipia kila unapotumia/kupita mi naona haijakaa sawa. Kwan kodi tunazolipa zinafanya nn? Panton tunalipia sababu ya kulipia gharama za uendeshaji kama. Mafuta, spare nk. Sasa daraja tunatalipia kwa sababu gan? Jana nilikuwa nasikiliza BBC hadi mtangazaji akashangaa kusikia litakuwa la kulipia. Wana jf naomba mnieleweshe sababu ya kuja kulipia hilo daraja ni nn? Na je huo utaratibu kuna nchi nyingine unatumia? Na nin maana ya public goods?
Nawakilisha

Karibu nchi zote duniani zitatumia mtindo huu wa BOT (Building Operate Transfer), jaribu kusoma soma kidogo siyo kila kitu ni cha kupinga. Wewe unafikiri NSSF watarudishaje hela zao. Dezo mbaya mkuu kuwa makini.
 
Labda mimi sielewi! Sijawahi kusikia dunia hii kunanchi inatoza hela ya kutumia barabara au daraja, zaid ya kodi, fines. Hii ya daraja la kigambon kuja kulipia kila unapotumia/kupita mi naona haijakaa sawa. Kwan kodi tunazolipa zinafanya nn? Panton tunalipia sababu ya kulipia gharama za uendeshaji kama. Mafuta, spare nk. Sasa daraja tunatalipia kwa sababu gan? Jana nilikuwa nasikiliza BBC hadi mtangazaji akashangaa kusikia litakuwa la kulipia. Wana jf naomba mnieleweshe sababu ya kuja kulipia hilo daraja ni nn? Na je huo utaratibu kuna nchi nyingine unatumia? Na nin maana ya public goods?
Nawakilisha

Tatizo lako ni dogo sana ujaona! sasa jibu ni kwamba zipo nchi nyingi tu, na kwa mtindo wa projects za PPP au BOT ni lazima kwasababu aliyedumbukiza senti zake atazihitaji na kafaida!
 
Serikali legelege Imeshindwa kila kitu nssf ni muwekezaji wa Ndani.

Serikali legelege haikusanyi kodi- D. Kafulila akinukuu maneno ya Baba wa Taifa
 
Tembea duniani uone ndio uanze kupiga kelele.
Hiyo dunia uliyotembea ni ipi?>
Nchi nyingi sana zina huu utaratibu na wewe ndio wa kwanza kushangaa.
Kweli ushamba ni mzigo mkubwa.
OTIS

Samahani wakubwa zangu nimekuwa mtamaji kwa muda ila katika hili naomba kuchangia.UTURUKI ni nchi moja iliyo katika mabara mawili (ULAYA na ASIA)na ni mji 1 tu(ISTANBUL) ambao upande 1 uko ASIA na Upande mwingine ulaya na pande hizi mbili zinatenganishwa na bahari kama vile feri na kigamboni.Napa kuna madaraja mawili (BOAZ KOPRUSU na SULTAN AHMET)ambayo yanaungani pande hizi mbili.Na utaratibu wakupita katika madaraja haya ni lazima ulipie kwa wenye magari ingawaje ukilipa mara moja ni kwenda na kurudi hivyo huu si utaribu mgeni hata katika nchi zilizo endelea upo.Cha msingi sisi kama watanzania Kupigania kiasi kitakacho wekwa kiendane na hali zetu za KITANZANIA
 
Labda mimi sielewi! Sijawahi kusikia dunia hii kunanchi inatoza hela ya kutumia barabara au daraja, zaid ya kodi, fines. Hii ya daraja la kigambon kuja kulipia kila unapotumia/kupita mi naona haijakaa sawa. Kwan kodi tunazolipa zinafanya nn? Panton tunalipia sababu ya kulipia gharama za uendeshaji kama. Mafuta, spare nk. Sasa daraja tunatalipia kwa sababu gan? Jana nilikuwa nasikiliza BBC hadi mtangazaji akashangaa kusikia litakuwa la kulipia. Wana jf naomba mnieleweshe sababu ya kuja kulipia hilo daraja ni nn? Na je huo utaratibu kuna nchi nyingine unatumia? Na nin maana ya public goods?
Nawakilisha

Samahani wakubwa ugeni kitu kibaya.Nimekuwa mtazamaji ila katika hili naomba kuchangia.Uturuki nchi 1 iloyo katika mabara mawili(ULAYA naASIA)na ni mji 1 tu ndio uko katika mabara 2 ambao ni ISTANBUL na unatenganishwa na BAHARI KAM ILIVYO KIGAMBONI NA FERI mji huu unaunganishwa na madaraja makubwa mawili(BOAZIC na SULTAN AHMET) kama lnavyotaka kuunganishwa FERI na KIGAMBONI.Utaratibu wa upitaji katika madaraja twaja hapo juu ni wa kulipia na hii ni kwa wenye magari na hulipa mara 1 kwa ajili ya kwenda na kurudi.Hivyo utaratibu huu si mgeni hata nchi zilizo endelea unatumika kikubwa ni kupigania kiasi kitakacho wekwa kiendane na MTANZANIA
 
Tatizo lako ni dogo sana ujaona! sasa jibu ni kwamba zipo nchi nyingi tu, na kwa mtindo wa projects za PPP au BOT ni lazima kwasababu aliyedumbukiza senti zake atazihitaji na kafaida!
Ni daraja gani na nchi gani wanalipia wananchi kupita.. naomba tafadhali nijifunze na mimi..
 
Mbona kulipia katika madaraja na barabara (TOLL WAY) ni jambo la kawaida. Waswahili tuna msemo. 'Tembea uone'.
 
Labda mimi sielewi! Sijawahi kusikia dunia hii kunanchi inatoza hela ya kutumia barabara au daraja, zaid ya kodi, fines. Hii ya daraja la kigambon kuja kulipia kila unapotumia/kupita mi naona haijakaa sawa. Kwan kodi tunazolipa zinafanya nn? Panton tunalipia sababu ya kulipia gharama za uendeshaji kama. Mafuta, spare nk. Sasa daraja tunatalipia kwa sababu gan? Jana nilikuwa nasikiliza BBC hadi mtangazaji akashangaa kusikia litakuwa la kulipia. Wana jf naomba mnieleweshe sababu ya kuja kulipia hilo daraja ni nn? Na je huo utaratibu kuna nchi nyingine unatumia? Na nin maana ya public goods?
Nawakilisha

It's actually about time The Government brings this PPP idea into its development plans. A lot of highways and bridges in the so-called developed parts of the world operate that way. Usually the contract is set for so many years. When done properly its an excellent way to improve infrastructure especially in a case like ours where the government is not exactly swimming in money. It also encourages for really good quality projects, since the private investor is usually keen to maintain the project for however long it takes for them to get thier return. Downside is though that the average citizen has to bleed through the nose for what should be public service.
 
Kina Mnyika, Ndungulile and company, wamelivamia suala la Kigamboni kisiasa, huku Mnyika akienda mbali zaidi katika maoni yake kutufanya tuamini kwamba, uwepo wa daraja ungeleta nafuu. Uongozi ni upeo na uthabiti katika kauli na msimamo. Muda si mrefu waheshimiwa hawa hawa wataanza kupigia kelele gharama za wananchi kutumia daraja kwa kufananisha na unafuu wa kivuko cha ferry ambacho leo hii wanatolea macho nauli mpya. Ni suala la muda tu, tusibiri.
 
Nionavyo mimi ni kuwa baada ya daraja kukamilika nafikiri wakazi wengi walalahoi wa Kigamboni wataondolewa kingamboni kwa ajili ya kupisha majengo makubwa cjui mahoteli, apartments Cjaelewa mradi ni wa bush au mwarabu lakini nackia ni la bush. Hivyo gharama ya kuvuka itakuwa juu ili washindwe na kuhama kigamboni na ukiangalia kupandishwa kwa gharama ya partoni ya ss ni katika kuwataka wakazi wa kigamboni waondoke. Mwenye akili timamu uwezi kupandisha baiskeli ya miguu mitatu ambayo engine kiuno kutoka sh. 300 hadi sh.1,500.00 yote haya ni katika mikakati ya kuwaondoa wanakigamboni. Nijuavyo au wanyavyo mataifa yaliyoendelea unapotaka kuwahamisha wakazi wanawaandalia sehemu na kuwajengea nyumba za aina moja kama ni flats au za chini na kuweka huduma zote muhimu halafu wanahamishwa na kupangiwa kulipia polepole mpaka watakapomaliza deni na nyumba linakuwa lako. Sasa kwa nchi yetu wao wanahamisha watu na kuwapeleka porini bila huduma zote muhimu baadae watakapojizatiti huko kwa nguvu zao serikali io io inakuja kuwahamisha tena. Mfano ni kigamboni yenyewe ilivyoanza hakukuwepo na watu na wengi walikuwa hawapapendi kigamboni lakini leo serikali linaona kigamboni mali baada ya kuaidiwa rushwa na ndio kisa cha kutaka kuwahamisha watu. Kama walijua kigamboni kitakuwa mali wangeweka au plan mapema kabla ya wakazi hawajajazana. na hata hayo maduka na mahoteli wanayosema yangelikuwepo kwenye ramani zao. lakini wao wanafanya kazi pasipo kuplan. Dar kumejaa kilichotakiwa ni kuhamisha baadhi ya huduma nje ya dar kwa mfano Temeke/ Kinondoni, Ilala huduma zote zijitegemee kama ofisi za maji ,Tra na nyingine ili ukitaka hizo huduma sio mpaka uende katikati ya mji. Kwa mfano tra wanaofisi karibu katika mikoa yote Dar Ilala,Kino,Temeke lakini ukitaka kulipia gari, conteiner ni lazima uende long room yote haya ni rushwa kwanini uclipie Ilala/Kino,Temeke na kwenda kutoa tu gari lako kwenye godown wanazosema zingine ziko nje ya bandari. Waweke tu rates zinazojulikana basi unajua kabisa kuwa toyota corolla kodi yake labda laki tano unalipia na kwenda kuchukua gari. Idara ya majihivyo, viwanja ndio usiseme. Hili litaondoa foleni ya kwenda town center co lazima tujenge izo mabarabara za juu ni miundo mbinu tu. Hata ikibidi tanzania kuna pori kubwa sana wanaweza wakatenga sehemu nje ya Dar na kuanza ujenzi wa huduma zote za kijamii, na wenye mpangilio mzuri inakuwa kama ni new dar na dar yenyewe inabaki kuwa old dar lakini ni ndani ya Dar io io. Bado tuna safari ndefu halafu serikali wanatumia pesa kibao kuwapeleka viongozi nje ya nchi kujifunza sasa wanaenda kujifunza nn
 
Labda mimi sielewi! Sijawahi kusikia dunia hii kunanchi inatoza hela ya kutumia barabara au daraja, zaid ya kodi, fines. Hii ya daraja la kigambon kuja kulipia kila unapotumia/kupita mi naona haijakaa sawa. Kwan kodi tunazolipa zinafanya nn? Panton tunalipia sababu ya kulipia gharama za uendeshaji kama. Mafuta, spare nk. Sasa daraja tunatalipia kwa sababu gan? Jana nilikuwa nasikiliza BBC hadi mtangazaji akashangaa kusikia litakuwa la kulipia. Wana jf naomba mnieleweshe sababu ya kuja kulipia hilo daraja ni nn? Na je huo utaratibu kuna nchi nyingine unatumia? Na nin maana ya public goods?
Nawakilisha

Kwani limeshaanza kutumika? Kama bado hatuna haja ya kuzozana hapa! Subiri lisimame tutajua tufanyeje!
 
Labda mimi sielewi! Sijawahi kusikia dunia hii kunanchi inatoza hela ya kutumia barabara au daraja, zaid ya kodi, fines.
Nawakilisha
Hapo kwenye nyekundu..... ondoa neno labda, kwa kuwa ushapewa data sasa.
 
Hiyo ndio hali halisi. Na magufuli si mjinga kusema kwamba 'kama hauna nauli piga mbizi', ingawa lugha yake ilitakiwa iwe ya ufafanuzi kuliko alivyofanya. Inaweza kuchukua miaka 50 kwa watanzania kumwelewa magufulil, lakini waziri huyu yupo sahihii licha ya kina Mnyika to dramatise as if yeye ni punguani. Kwa wale watakaojaliwa na mwenyezi mungu kuishi miaka mingi zaidi, watajionea wenyewe uhalisia wa mambo.
 
Serikali legelege Imeshindwa kila kitu nssf ni muwekezaji wa Ndani.

Serikali legelege haikusanyi kodi- D. Kafulila akinukuu maneno ya Baba wa Taifa

Kodi inayopotea kila mwaka ni karibia sawa na 25% ya bajeti ya serikali, kwa takwimu za mwaka jana ambazo zinaonyesha kwamba bajeti ya tanzania ilikuwa trilioni milioni 13.
 
Back
Top Bottom