Hii imekaaje wanajamvi nani ana kosa kati ya hawa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Wanafunzi wamvaa DC kupinga mwenzao kupigwa na mwalimu

Wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Siha, Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro, wameandamana hadi kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, kupinga mwenzao kupigwa na mwalimu makofi, mateke na ngumi hadi kupoteza fahamu.
Pia waligoma kuingia madarasani, badala yake walimbeba mwenzao kwa machela hadi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Annarose Nyamubi, ili kumuonyeshea hali halisi kabla ya kumpeleka hospitali.
Mwanafunzi aliyepigwa na mwalimu huyo, ni Baraka Munuo, anayesoma kidato cha sita.
Inadaiwa kuwa kipigo dhidi ya mwanafunzi huyo, kilitokana na kutovaa sare za shule na kukaidi amri ya mwalimu iliyomtaka kwenda kuvaa sare halisi za shule.
Hata hivyo, maandamano ya wanafunzi hao, yalizimwa na polisi walipokaribia kufika katika ofisi hizo na kushauriwa kumpeleka mwenzao hospitalini wakati suala hilo likiendelea kushughulikiwa.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina wakati wa maandamano hayo, baadhi ya wanafunzi, walisema mwenzao alipigwa na mwalimu huyo (jina tunalo) Januari 31, mwaka huu asubuhi wakati wakiwa katika ukaguzi.
Mkuu wa Wilaya, Nyamubi, ambaye alikwenda katika shule hiyo, aliwataka wanafunzi kuwa watulivu wakati serikali ikiwa inalifanyia kazi suala hilo na kuwataka kurejea madarasani.
 
unajua nimeangalia mtiririko wa hiyo habari nikaona kwamba mwanafunzi hakuvaa sare za shule,then karudishwa akavae akakataa,then akapigwa mateke na vibao wao wakaamua kumbeba na kumpelekea mkuu wa wilaya kwanini wasianze na headmaster?halafu hata hivyo kwanini huyu mwanafunzi alimgomea mwalimu kwenda kuvaa sare za shule?mie sikuona sababu ya maandamano kwa hapo sema sababu tu umeshakua ni mtindo ndio maana wameandamana
Hii ndi bongoland, kila sehemu maandamano!!
 
Kijana na mwalimu wote wamevuma mazao ya walichopanda. Kijana hana adabu na mwalimu amevamia fani kuganga njaa. Mwalimu hapaswi kupiga mtoto kwa mateke na magumi. Watoto watukutu wanahitaji busara kuwashughulikia.
 
hivi viboko viliishafutwa sasa njia mbadala walipendekeza iwe nini?maana zamani kulikua na adhabu balaa kuchimba mashimo,kubeba matofali nk
Kijana na mwalimu wote wamevuma mazao ya walichopanda. Kijana hana adabu na mwalimu amevamia fani kuganga njaa. Mwalimu hapaswi kupiga mtoto kwa mateke na magumi. Watoto watukutu wanahitaji busara kuwashughulikia.
 
Back
Top Bottom