Hii hapa ni List ya Mapedeshee/Papaa wa Tanzania na Kazi zao

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Kwa Watanzania walio wengi jina Mapedeshee au Mapapaa ni maalufu lakini natumaini watanzania baadhi hawajui Mapedeshee ni aina gani ya watu na wanafanya kazi gani kama sehemu ya maisha yao,manake sifa zao kubwa zilianza kutajwa kupitia miziki ya dansi lakini sasa wameamia kwenye ubongo wa fleva [Kizazi kipya].Majina maalufu kwenye kutajwa huko ni kama Papaa Msofee,Pedeshee Ndama Mtoto wa Mbuzi nk.

Nimeeandika thread hiii baada ya kumuona Mama mmoja mjane akilalamika kwenye taarifa ya habari ya ITV kuwa Pedeshee au Papaa Msofe amemdhulumu Mjane huyo kiwanja chake chenye nyumba juu yake ambayo mumewe alijenga ikiwa na thamani ya Shilingi Millioni Ishirini na Nne.

Mama huyo analalamika kuwa amepeleka malalamiko polisi lakini ajabu Polisi wakishaonana na Pedeshee au Papaa Msofe [Marijani] basi wanasepa kimya kimya na mjane huyo akiwafuatilia wanauchunu.Hivyo kupitia msaaada wa TAMWA [Tanzania Media Womeni Association] anaomba msaada wa Waziri Mkuu kumsaidia kukabiliana na Pedeshee huyo ili apate mali hiyo aliyoachiwa na marehemu mumewe.

Kwa wanajamii tujuzeni list ya hao Mapedeshee na Kazi zao manake uenda wengine humu jamvini tukajifunza kitu kuhusu hawa mapedeshee na kazi zao.Nlipatwa kudokezwa lakini dokezo ilo sikulipa tafsiri lasmi kwa kuwa kupitia jamvi, nilichoambia uenda kikawa na msaada kwa wanajamii ambao wameshapata kuathirika au wanategemea kuathirika na vitendo vya Mapedeshee hao.


Nawasilisha
 
Ukisikia papaa,pedeshee hawa watu ni wabaya sana mara nyingi hujipatia mapesa kwa njia haramu,kama kudhurumu na mambo mengine mengi ya kishetani ili mradi wapate pesa.
 
hebu rekebisha heading yako kwanza........................by the way hao mapedeshee ni WAPIGAJI tu wa mjini
 
Pedeshee is another word of "Tapeli",
Yaani ili kutumia tafsida, badala ya kuita Tapeli Shark, ndio unaweza kutumia Pedeshee Shark!!!
 
PDG..kwa kifaransa..PRESIDENT DIRECTOR GENERAL..walianzia kongo,kukua kwa muziki wa dansi kukawabatiza watu maarufu hasa vijana wenye mafanikio(wamepataje hatujui) jina hilo...wanaimbwa kwa sababu hutoa sapoti kwa wanaowaimba katika kitu ambacho wazaire hukiita MABANGA(unalitaja jina la mtu ana biashara ama shughuli yake katika tungo zako) na baadaye anakupatia malipo...na wanawake huitwa MASHEBEDEE....NAWASILISHA...
 
hwafai na hela za dhuluma na biashara chafu tu huku wakiwatenda vibaya dadazetu wanaopenda pesa bila jasho
 
Hawa jamaa huwa wanafaidi watoto wakali mpaka napata hasira.

VIDEO Queen mwenye taito kubwa Bongo, Rehema Fabian, juzikati alinaswa akifanya mambo ya chumbani hadharani na pedeshee anayefahamika kwa jina la Jacob Best, kitendo kilichozua maswali kibao kutoka kwa wadau walioshuhudia uchafu huo na kutafsiri kuwa ni ufuska, Ijumaa Wikienda linakudondoshea.

Ishu hiyo ilinaswa live na paparazi wetu Oktoba 18, mwaka huu ndani ya New Maisha Club, Masaki jijini Dar es Salaam. Rehema na pedeshee huyo walitinga kiwanjani hapo wakiwa ameshikana mikono, wakajiweka mahali na kuanza kuchapa ‘matingas' kwa kasi.

Kilevi kilipokolea vichwani mwao, walianza kudendeka hadharani, bila kujali umati wa watu uliokuwa ukiwashuhudia.

"Sikutegemea kama bado Rehema ana tabia za kifuska kiasi hicho. Walichokuwa wanakifanya hakipaswi kufanywa eneo kama hili bali chumbani, ama kweli dunia imekwisha," alisema mmoja wa shuhuda wa tukio hilo.

Rehema alipotafutwa na kuwekwa mtu kati ili aeleze sababu za kufanya uchafu ule, alifunguka kuwa pedeshee huyo ndiyo mumewe mtarajiwa hivyohaoni ubaya kufanya chochote mahali popote.
 
Back
Top Bottom