Hii fimbo ni muhimu kwa jeshi la polisi?

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,950
711
Wadau,
Naamini wengi wetu tumekuwa tukiipa uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki kipa umbele. Ndiyo, uchaguzi huo ni wa muhimu ili kuwapa fursa wananchi wa eneo hilo kumchagua kiongozi wamtakaye.

Mimi nitawaamisha kwenye hiyo mada na kuwaleta kwenye hii kuhusu matumizi ya hiki kifimbo kwa jeshi letu la polisi. Nimekuwa nikijiuliza ni
1. nini umuhimu wake hawa maafande wetu kutembea na hivi vifimbo?
2. Watapungukiwa nini kama wasipokuwa navyo?
3. Je hatuoni umuhimu wa kuwapunguzia hawa maafande kubeba vitu ambavyo havisaidii lolote?

Kwa mtazamo wangu nilifikiri hawa maafande hawahitaji hivi vifimbo katika kuwajulisha vyeo au utendaji kazi wao. Wana JF, nyie mna mawazo gani?


Kamanda+wa+Polisi+wa+Polisi+mkoa+wa+Ilala,+Faustine+Shilogile+akikagua+hali+ya+usalama+katika+eneo+la+tukio.JPG
 
Back
Top Bottom